Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Namuombe Mungu Lowassa asikatwe,,,maana hakuna kiongozi mwingine atakaye weza fanya mabadiliko Tanzania.
 
Ukilinganisha huyu wa kufunga cctv mitaa ya Dar na huyu wa wizara nani ana nafuu?
 
namuunga mkono, matatizo la Dar yanahitaji wizara! tukianza na foleni, uchafu, maji, ualama, sewage na ujenzi holela
 
Bogus statement..

Dareslaam now lina meya sita
wakuu wa wilaya watatu na mkuu wa mkoa mmmoja na mawaziri wote wako dar
kuongeza tena waziri wa Dar ni ujinga na utumiaji mbaya wa nafasi
 
Ni ili kurahisisha utatuzi wa matatizo lukuki ya jiji la Dar, kwamba waziri akilala akiamka anatoa maamuzi ya haraka kwa manufaa ya wananch. Sambamba na hilo kila mwaka zitajengwa nyumba millioni moja kuendana na sera itakayotungwa kwa ajili ya jiji hilo. Nipashe siku ya leo.

Kweli hayo yatakuwa ni maamuzi magumu.. kuongeza ukubwa wa baraza lamawaziri kwa kuongeza waziri wa mkoa,

Kwanini asiwatumie vizuri mkuu wa mkoa? mkuu wa wilaya? wakurugenzi wa halmashauri? Na wateule wengine wa Raisi wapo kibaaaaaaaaaaaaaaaao... after all wizara zote office zao zipo dar!!
 
Nani kampa mamlaka ya kupiga kampeni? Chama kina utaratibu wa kutafuta udhamini na si unasimama tu barabarani then unaropoka unayoona yanafaa
Kwani kuna mtangaza nia gani ambaye hajasema atakachofanya Akiwa raisi?
Membe mbona alisema atafunga kamera za Siri dsm, hukusikia?

CCM hamumuwezi Lowasa.
 
Ukilinganisha huyu wa kufunga cctv mitaa ya Dar na huyu wa wizara nani ana nafuu?

Kufunga CCTV ni jambo la lazima, kwa usalama lakin hili la kuwa na wizara ni la anasa tu kama tuna pesa za kuchezea.
 
Kwani hela za ziara za rais wako anazopigia misele kila siku kwenye nchi za watu bila faida yoyote kwani nani anazilipia? ungetoka nje ya 18 kabla ya ku comment

Your point being?! Just because upuuzi unafanyika basi watu waendelee kufanya upuuzi?
 
Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam, Lowassa alirejea kauli iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 1995, kwamba watu wanataka mabadiliko na wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya chama hicho.

“Mimi nitayaleta haya mabadiliko nikiwa ndani ya CCM. Nagombea urais kwa sababu nauchukia umasikini na nitaunda serikali ya kusaidia wanyonge, kuwafukuza machinga, mamantilie na waendesha bodaboda ni upuuzi. Watu wanatafuta riziki tunawafukuza inatakiwa tuwawekee mazingira mazuri,” alisema na kushangiliwa kwa nguvu.

Alisema anauchukia msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na iwapo atakuwa Rais atalimaliza tatizo la foleni katika jijini Dar es Salaam kwa miezi sita.

“Kutakuwa na waziri anayeshughulika na jiji la Dar es Salaam tu kama ilivyo kwa nchi jirani ya Kenya. Yeye akiamka tu akili yake yote ni kushughulikia changamoto za jiji hili,” alisema Lowassa ambaye mara kwa mara alikuwa akiwaimbisha wananchi wimbo wa ‘mchakamchaka’, huku akisisitiza kuwa ataiongoza serikali yake kwa mtindo wa mchakamchaka akisema ambaye hataweza atakaa pembeni.

Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura ili wapate fursa ya kumchagua iwapo atapitishwa na chama hicho kugombea urais, huku akiwataka wamuombee kwa maelezo kuwa Mungu ndiye anayepanga kila kitu.

“Mrema (Augustine) alikuwa maarufu sana mwaka 1995 mpaka gari lake likawa linasukumwa na wananchi, lakini katika kura za urais hakushinda. Jiandikisheni ili tufanikishe safari ya matumaini,” alisema.

Lowassa alisema kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaomuunga mkono anaona kama tayari ameshashinda huku akisisitiza kuwa ameshawafunga goli wagombea wenzake kama anavyofanya mchezaji wa timu ya soka ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

“Kati ya wagombea wote hakuna mwenye uzoefu ndani ya CCM kama mimi. Kumbukeni rais ndiye mwenyekiti wa CCM,” alisema.

Aiteka Dar

Lowassa aliwasili katika uwanja wa ndege wa zamani (Terminal 1), saa 2:00 asubuhi akitokea mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa CCM wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wanachama wa mkoa huo waliojitokeza kumdhamini ni 212,150, kati yao kutoka Kinondoni ni 95,251, Temeke (72,100) na Ilala (44,799).

Afananishwa na mtume, Yesu

Akimkaribisha Lowassa Dar es Salaam, Madabida alimfananisha waziri mkuu huyo wa zamani na Mtume Muhammad ambaye alikuwa akitangaza dini lakini alikuwa akipingwa na watu wake wa karibu na kufafanua kuwa kutokana na hali hiyo Mungu alimueleza kuwa hatamuacha na atakuwa pamoja naye.

Laana ipo juu yako
 
Madabida lazima ajue kuwa Yesu hakuwa na kashfa ya ufisadi...Kama huyo anayemfananisha naye.....
 
Mbona sijaona sehemu yeyote aliyomfananisha na "Mtume" Yesu?

Au wewe mwandishi "Mtume" Yesu ni sawa na Mtume Muhammad?
 
Huyu Ramadhani Madabida ndiye aliye wauzia Watanzania ARV fake !
Kweli ndege wafananao huruka pamoja
Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Na atapigwa tu, hakuna jinsi !
 
Madabida lazima ajue kuwa Yesu hakuwa na kashfa ya ufisadi...Kama huyo anayemfananisha naye.....

Hivi huyu Ramadhani Madabida kesi ya kuiuzia MSD ARVs fake imeishia wapi?

Birds of the same feather flocks together!
 
Ukitaka kujua kuwa Lowasa ni mtu wa aina gani....tazama marafiki zake....
 
Akacheze na vitukuu vyake huko!!
Anaanza kuwa "dogo" tena, anaongea pumba sana!
Sikapendi sana haka kababu siku hizi, kwanza kalianza kuniboa kwenye bunge maalum la katiba na bado kanaendelea kuniboa kila kanapofungua mdomo! Si kakae kimya tuu!!! aaarrggghhhhh!!!
Wewe humpendi Kama nani, wewe subiri aibu yako, sauiti ya wengi wape..toa hoja za msingi Kama kweli umesoma na unajua, acha kunya kunya
 
Hivi huyu Ramadhani Madabida kesi ya kuiuzia MSD ARVs fake imeishia wapi?

Birds of the same feather flocks together!

Si unaona mzee msocialist a.k.a.mganga wa jadi nae kawa fisadi damu.
 
Back
Top Bottom