Badala ya kuita ILANI (Hii ni kwa vyama vinavyotaka dola) wangeita orodha ya vipaumbele. Nadhani wangepunguza mzozo na wanasiasa.
mimi nahsi mzee kingunge amesema kweli. kwani amesema ndani ya waraka huo uansema " kanisa litahakikisha linaweka watu wake na kuwadhibiti" sasa jee kanisa litapofanikiwa kuweka watu wake na kuwadhibiti . itakuwa kwa manufaa ya nani?
So wat z ua arguiment? The roman catholic as a church or the message?And as wise men, should we judge the person/institution or the content? ROMAN CATHOLIC'S PAPER IS IT THE ADVICE OR THE LAST SAYRepent Kingunge now tells Catholics
UNLIKE the hypocrites and demagogues in CCM and the parliament I am for the first time, fully behind Mzee Kingunge and now more ever than before believe in his sound judgement and admirable foresight.
Countrymen, let us pull back, and take a looong look at the mishaps that have deliberately or accidentally befell our people and land because of SOME VERY CLERGY MEN who think they are anointed by God to be the choosers of our leaders.
I say this because I have never seen anywhere in the world where a president, chairman of political party and the rulling party in fact being subordinated to the Church or any other religion for that matter in a true democractic country.
There is no way in Africa where we can let sheikhs or bishops HAVE THE LAST say in how the government decides and operates and at the same time GUARD PEACE AND UNITY in a country?
Wherever you see such thing happen, that is, a leader being led by those whom he is leading then the leader is weak and useless.
For those CCM members and parliamentarians who believe there is nothing wrong with the recent position adopted by the Catholcs one thing is for sure -they are demagogues. They believe they can hunt with the foxes and run with the hare at the same time. Something neigh impossible....at least for me!
If we let the church preach politics then what will political parties do? Become jobless? And which religion will ever back a man from a rival sect or faith order ? Will not things be like at TBC- a national broadcaster who is competing with religious station and actually is outdoing even the private faith station in spreading the word of God? Directionless? Overzealous Board members and Management at TBC ? Nowdays, after the 7 a.m. news the TBC has 5-7 minutes dedicated to a single religion announcements/advertisements. What is this Mr. Director? After the announcement expect one or two gospel songs? What an entertainment in a national broadcasting Organ ?
Watanzania katika miaka hii ya vituko na maajabu ni kwamba mwizi mkubwa ndiye anayetaka kuwa Mkuu wa Polisi ili akiiba pasiwe na wa kumshuku; mzinzi mkubwa ndiye anayetaka kuwa mwalimu wa shule au chuo chenye wasichana wengi ili afanye biashara yake; wajinga, mabahili, wabinafsi wakubwa na mabaradhuli wasiokuwa na nia yoyote ya kumsaidia mwananchi wa kawaida wanakimbilia siasa ili kudanganya kuwa wana kitu wanachotoa; malaya mkubwa hutaka kuwa na kazi au cheo chenye heshima ili umalaya wake usijulikane; na ndivyo ilivyo kwa wauaji, wavunja nchi na wasambaratisha jamii wakubwa nao hutaka kuwa viongozi wa dini ili wanapofanya kazi yao ya kuikokota jamii kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe pasiwe na anayewashuku. Tujihadhari, tujihadhari, tujihadhari au tutakuja lia na kusaga meno kwa miaka mingi katika muda mrupi tu kutoka sasa!
kingunge yuko sawa ila wenye ajenda za siri ndio wanaotaka kumchafua
anasema kama mwalimu angedai uhuru kwa kutumia biblia au waislamu kwa kutumia quraan pasingepatikana umoja wa kitaifa
nchi zenye dini nyingi dini haiwezi kutumika kama chombo cha kuwaunganisha WATU maana kila imani inaamini kivyake
mambo ya ilani ni mambo ya vyama vya siasa wakubali wakatoliki wamechemsha
Sioni mahali popote ambapo waraka huo wa Katholiki unashabikia kwa namna yoyote uwakilishi wa kidhehebu. Waraka huo haujasema kiongozi bora ni lazima awe mkristu, au ni lazima aamini lolote linaloaminiwa na wakristu, wala anaeshiriki katika mambo yanayoshirikisha ukristu.
Waraka uko kamili na hauna ahadi za kampeni kwa wagombea wowote kama wataamua kuufuata, hauna hata nia ya kulazimisha ufuatwe. Unabaki kuwa ni mapendekezo na matamanio ya waliyouandaa kuhusiana na aina ya uongozi wanaodhani unafaa kwa Taifa letu.
Sioni mahali popote katika kauli wala mapendekezo ya waraka uliotolewa na Katholiki unaotaka au kukusudia kuingilia serikali katika kupata viongozi wake. Nadhani iko wazi kuwa waraka huo unatamani serikali itakayosaidia kuwafanya wananchi waweze kufuata maadili mema na si vinginevyo.
Kwa mtazamo wangu hakuna taasisi zozote ambazo hazina siasa ndani yake. Hata Taasisi za dini zina siasa zake, nazo ndizo zinazofuatwa na viongozi na waumini wao. Siasa ni utaratibu ambao unahusisha watu kila wanapobidi kushirikiana kwa umoja wao.
Serikali haiwezi kushinikiza kuwa dini zisiwe na kauli yoyote kama inaona mambo yanakwenda mrama katika uongozi wa serikali hizo. Ni vigumu kwa kuwa, waumini wao ndio hao hao wanaoshiriki katika serikali na ndio wanaokuwa affected na siasa za vyama na serikali inayokuwa madarakani. Inawezekana dini ikaachana na siasa za vyama na serikali endapo tu, wanachama wa vyama na wanaohusika na serikali watakuwa ni tofauti na wale wanaoamini katika dini hizo.
Mkuu umesema vizuri sana kwamba wewe HUONI popote penye matatizo.. Mimi naona sehemu nyingi sana kwani siku zote ktk Uongozi wa nchi, taasisi za kidini zinapoingilia kati ndipo utata huanza.
Unajua nchi za kiarabu kuna mengi ya wahubiri wa dini huzitaka serikali zao kufanya mema kwa faida ya wananchi wote lakini utata huja pale sisi tunapotazama nafasi ya dini na uongozi wa nchi hizo pamoja na kwamba population ya nchi hiyo ni 99 waislaam. Kifupi kanisa wala Msikiti hautakiwi kabisa kuingiza hoja zake serikalini unless swala hilo linahusiana na waumini wake.
Ni makanaisa na misikiti ilotuchanganya akili wakati wa uchaguzi wa Mkapa na huyu JK..ni hao hao waliowatukuza na kuwaona viongozi bora, leo hii tunapewa somo jingine tena wakati wa uchaguzi ukikaribia.
Trust me mkuu wangu hakuna mtu hata mmoja asiyefahamu nani kiongozi mzuri hata iwe jangwani au kijijini ndani kabisa Umasai...wote hawa walikuwa na mila za kuchagua viongozi wao na walitoa sifa au kashfa kutokana na kiongozi aliyepo.
Tatizo ni kwamba, kiongozi mzuri hana alama usoni nahata siku moja huwezi kukisia ila kwa ahadi zake..Kinachomtangulia kiongozi ni mfumo bora wa utawala.. Maadili na miiko ya Uongozi ndio road signs za kiongozi yeyote yule..kisha wananchi nao wapate somo la haki za uraia wao na sii somo la kumchagua kiongozi mzuri ambaye hajawahi kuongoza. zaidi ya hapo Mbunge sii kiongozi hata siku moja ila ni mwakilishi wa wananchi..
Hivi kweli unaweza kunipa sifa za kumchagua mtu kati Mwakyembe na Mwakalinga kwa kutumia vigezo hivyo?.. Mwakyembe tunamjua na mapungufu yake, mtu kama Mwakalinga hatumjui hivyo.. somo linatuambia nini kuhusu watu kama hawa?.. Je, linazungumza nini kuhusu wagombea wa vyama vya upinzani..Tunatazama mtu au chama? maanake nashindwa kuelewa inaonyesha kama waraka huu unataka tuishague CCM lakini tuwachuje viongozi wake badala ya kutazama upana na sera za vyama..
Siku zote uchaguzi wa viongozi hutokana na sera za chama sasa tukianza kuweka macho yetu kwa watu na tabia zao sijui nani mbora kuliko mwingine...
Hivyo pamoja na makosa ya mzee Kingunge ktk mtazamo wa wengi bado mzee huyu ana haki sawa ya kuelezea yale anayoyaona yeye kuwa ndio safi na tumkosoe kwa alosema tukizingatia kwamba tupo radhi kupokea maagizo kama haya ya waraka toka dini tofauti..
Binafsi sipo radhi kabisa na itajenga uhasama zaidi inapofikia viongozi wa dini kuitumia serikali kujenga kitu chochote kile..
Siasa za bongo hizi. Watu wa media nao, si ndio anawapa ulaji? si tunapomshangaa mzee anavyofulia, wao mana'make' (wanaendelea kuuza habari).
I still dont know why media inaendelea kumpa nafasi wakati wakijua wazi kwamba inaweza kuwa counter-productive kwa kingunge na CCM
.Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.
Huu ndio uwezo wako wa kuchambua mambo? Niko tayari kuchangisha pesa kukupatia za kuiachia familia yako ili ujitoe mhanga pale mjengoni uli uondoke na watu hatari na wasio na msaada kwa taifa kama wewe. The amount of vernom you are spitting is twice that of a cobra..
Mimi nafikiri ungeweka bayana nini kingunge amesema badala ya kumuhukumu na kumwita kachanganyikiwa.
Hakika hata mimi nilipousoma niliona kuna athari kubwa sana katika jamii ya watanzania. Athari hizo ni :
1. Kwa kuwa umetolewa na madhehebu ya kidini, ulikuwa na lengo la kuelimisha waumini wake nini wafanye katika kuchagua viongozi wa kisiasa. Sasa nilijiuliza vipi wao viongozi wa kikatoliki, je walichaguliwa na nani kuwa viongozi, je waumini walishiriki katika kutoa mapendekezo au hata kuwachagua? au Pope aliwachagua ?
2. sasa nilijiuliza kama wao wliingia katika madaraka ya kuwa mapadr au hata maaskofu kwa kuchaguliwa na Pope , sasa vp waingile mambo ya kisiasa?
3. je kama Padre au Askofu anafundisha kuhusu Yesu vipi mtu huyu atasema achaguliwe mtu wa dhahebu lingine?
4. waraka ulikuwa na mengi yaliyojificha na yenye viashiria za ubaguzi ingawa yalipambwa na maneno mazuri sana.
Kijumla waraka ule ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa hususan kipindi hichi cha kupamba kwa UDINI huko Tanzania.
Namuunga mkono mzee Kingunge. maneno yake kuntu
.
Mimi nafikiri ungeweka bayana nini kingunge amesema badala ya kumuhukumu na kumwita kachanganyikiwa.
Hakika hata mimi nilipousoma niliona kuna athari kubwa sana katika jamii ya watanzania. Athari hizo ni :
1. Kwa kuwa umetolewa na madhehebu ya kidini, ulikuwa na lengo la kuelimisha waumini wake nini wafanye katika kuchagua viongozi wa kisiasa. Sasa nilijiuliza vipi wao viongozi wa kikatoliki, je walichaguliwa na nani
Mapadre wa Kanisa katoliki hawachaguliwi na Askofu wala Papa na wao hupatikana kwa kuitikia wito .Jambo la kwanza wana angusha ile mbaya then wana faulu mitihani na mwisho tabia zao hatimaye wana pewa daraja la Upadre.Hakuna kura na hakuna padre kihiyo kwa taarifa yako .
kuwa viongozi, je waumini walishiriki katika kutoa mapendekezo au hata kuwachagua? au Pope aliwachagua ?
2. sasa nilijiuliza kama wao wliingia katika madaraka ya kuwa mapadr au hata maaskofu kwa kuchaguliwa na Pope , sasa vp waingile mambo ya kisiasa?
Sikia mpayukaji .Papa na Maaskofu wote ni ma padre .Uaskfu na U papa ni cheo ama title ambayo hawawezi kupewa wote .Wana kazi maalumu , kusimimamia Kanisa kwa maeneo yao hao maaskfu , ikiwa ni pamoja na kuhimiza , Elimu , maendeleo, nk .Ni askofu pekee huteuliwa na Papa na uteuzi huja baada ya mchujo mkali si lele mama .Papa unajua sasa kwamba ma kardinari sasa ambao bado ni ma padre kwa asili hukutana Rome na kufanya mambo kama ulivyo ona wakati ule .
3. je kama Padre au Askofu anafundisha kuhusu Yesu vipi mtu huyu atasema achaguliwe mtu wa dhahebu lingine?
Nonsense hueleweki maana sijaona mahali ambapo uchaguzi wa aina hii umesema nadhani una matatizo wewe
4. waraka ulikuwa na mengi yaliyojificha na yenye viashiria za ubaguzi ingawa yalipambwa na maneno mazuri sana.
Tutajie hayo yalioyo jificha na useme yamejificha wapi il tukayashuhudie kama yako tutaupinga hadharani bila ya ificho .Tanzania ni ya wote . Na useme hatari unayo iona wewe .Hakuna hatari kuliko ile ya smz kuwanyima watu haki ya kupiga kura kaka .
Kijumla waraka ule ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa hususan kipindi hichi cha kupamba kwa UDINI huko Tanzania.
Namuunga mkono mzee Kingunge. maneno yake kuntu
.
Mimi nafikiri ungeweka bayana nini kingunge amesema badala ya kumuhukumu na kumwita kachanganyikiwa.
Hakika hata mimi nilipousoma niliona kuna athari kubwa sana katika jamii ya watanzania. Athari hizo ni :
1. Kwa kuwa umetolewa na madhehebu ya kidini, ulikuwa na lengo la kuelimisha waumini wake nini wafanye katika kuchagua viongozi wa kisiasa. Sasa nilijiuliza vipi wao viongozi wa kikatoliki, je walichaguliwa na nani kuwa viongozi, je waumini walishiriki katika kutoa mapendekezo au hata kuwachagua? au Pope aliwachagua ?
2. sasa nilijiuliza kama wao wliingia katika madaraka ya kuwa mapadr au hata maaskofu kwa kuchaguliwa na Pope , sasa vp waingile mambo ya kisiasa?
3. je kama Padre au Askofu anafundisha kuhusu Yesu vipi mtu huyu atasema achaguliwe mtu wa dhahebu lingine?
4. waraka ulikuwa na mengi yaliyojificha na yenye viashiria za ubaguzi ingawa yalipambwa na maneno mazuri sana.
Kijumla waraka ule ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa hususan kipindi hichi cha kupamba kwa UDINI huko Tanzania.
Namuunga mkono mzee Kingunge. maneno yake kuntu