Wabunge wa CCM Tusiyumbe.
Nimeanza kwa Wabunge wa CCM kwa sababu kubwa kwanza sisi chama chetu ndicho kilicho na dhamana ya kuwaongoza watu wa nchi hii.
Lobbing zimeanza za Makampuni makubwa ya Migodi kupinga sheria ya Fao la kujitoa.makampuni binafsi nayo yataanza soon kupinga uamuzi huu kwa maslahi ya wachache Maslahi yasiyozingatia maono ya nchi na Usalama wa Taifa.Maslahi yanayoangalia siasa za muda za kuwafurahisha wanaharakati huku taifa likikosa nguvu ya kiuchumi.
Nawatahadharisha wabunge wote na hasa wa Chama changu CCM,tuwe makini na kila move hasa kipindi hiki ambacho Rais Magufuli amekuja na mwanga juu ya hatma ya viwanda vya nchi hii;Magufuli ameamua nchi iwe ya viwanda kupitia Mifuko hii ya kijamii,Lakini naona mapandikizo yakutaka kuidhoofisha mifuko hii,Mipango hii wanajua wanaoiratibu nia yao lakini wabunge wenzangu na wana CCM fao lakujitoa ni miongoni mwa mipango ovu ya kutaka kumdhoofisha Rais Magufuli na kudhoofisha mapato ya mifuko hii iliyoelekezwa kusimamia mageuzi ya viwanda nchini.
Kwanini watanzania kila jambo tuliwekee siasa?Uimara wa mifuko.ya kijamii popote duniani ndio kiini cha Usalama wa Taifa,Usalama.wa nchi katika kila nyanja iwe ya dharura za kiulinzi au kukuza uchumi hii ni roho ya nchi hasa nchi Hizi zinazoendelea.
Tuwe makini sana juu ya hawa wanaotaka kuturudisha nyuma.Rais anadira ya viwanda,Mifuko hii imepewa jukumu hili kwanini tuanze kutaka kuwadhoofisha.Kwa haraka haraka NSSF wanaweza kuokoa karibu biln 60 pesa ambazo kwa nchi changa kama hii zikiwekezwa kwa busara na uzalendo zinalifanya taifa lipae kiuchumi.
Watanzania tuache siasa pesa hizi ni za watanzania wakifikisha umri unaostahili watalipwa nchi hii lazima itangulize maslahi ya wengi kwa faida ya vizazi,tuache harakati na siasa za kutaka sifa kwa mambo mazito yanayogusa ustawi na usalama wa nchi.
Tuache mifuko ikusanye pesa a kuwekeza kwenye viwanda .Tuache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja.
Kingu Elibariki
MP Singida West
Huyu huenda ana wendawazimu na unafiki fulani.
1) Kwa nini wabunge wanapomaliza muda wao wasiache mafao yao, wachukue kidogo kidogo ili kuendeleza sera ya Rais ya viwanda?
2) Kwa nini Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu wakimaliza muda wake asiache mafao yake, alipwe kidogo kidogo ili yaendeleze viwanda?
3) Kwa nini Mawaziri, maDC na maRC wasiache mafao yao, wachukue kidogo kidogo ili pesa hiyo iunge mkono dhamira nzuri ya Mh. Rais ya ujenzi wa viwanda?
Hivi wanaotakiwa kuunga mkono dhamira nzuri ya Rais ya ujenzi wa viwanda ni wafanyakazi tu na siyo Rais mwenyewe, Makamu wake, Waziri Mkuu, Mawaziri, maDC, maRC na wabunge?
Hii nchi imejaa watu wanafiki sana kama huyu mbunge. Kwa fikra zao, uzalendo na kujitolea kunatakiwa kufanywa na watu wa hali ya chini, yaani wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara ila viongosi wakubwa wa kisiasa, wao ni watu wa kutumikiwa, ni watu wanaotakiwa kuishi katika neema ya utajiri na ufahari. Watu wa chini wanatakiwa kuteseka ili wao waishi kifahari.
Waafrika, Baba zetu na Babu zetu, waliwaondoa wakoloni weupe kwa damu na jasho ili kuwa huru lakini baadaye tumetumbukia kwenye utumwa wa weusi wenzetu. Kama walivyojitoa Baba na Babu zetu kuutafuta uhuru, sisi nasi sasa tunahitaji kushiriki harakati mpya za kuuondoa ukoloni wa weusi wenzetu wanaojiita viongozi lakini ni watu wanafiki, waongo na waliojaa hila. Baadhi yao ni wabaya kuliko hata wale wakoloni wazungu waliowafunga wapigania uhuru weusi.
Hawa wakoloni wa sasa ni kazi kubwa sana kuwaondoa maana wengi wao ni walaghai wakubwa. Hujitokeza kwetu kama watu wenye huruma na upendo, wazalendo na wapenda maendeleo yetu lakini katika kificho, kila siku wanapanga na kutekeleza njama za kutuangamiza.
Tusiposhikamana watatuangamiza. Nao ni werevu maana wametutenganisha kwa fikra za siasa za vyama, na wakati mwingine hata kikanda na kikabila kwa sababu wanajua katika umoja wetu wa kudhulumiwa, wao hawatakuwa na nafasi. Nasi kwa ujinga wetu tumekubali kutenganishwa.