Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Kwa sababu yeye Kashiba na aliyekuwa na njaa ashamsahau!
Mtu wa ovyoo sana Huyu mb

Ova
 
Na kuna yule wa Ulanga
Mkuu, Wako wengi wa sampuli hiyo. Tulia vizuri katika hiyo position uliyopo sasa, utawatambua tu. Hiyo ndiyo CCM mkuu. Hoja ya Kingu hadi inachoma moyoni, bado tunasema tuna wawakilishi bungeni.
 
Ila mimi kama nimemwelewa mno lengo lake ni zuri mno mkuu
...anajua hili litaliangusha Jiwe mchana kweupe,na kwasabb naye anataka Jiwe lishindwe basi anachochea hasira za watu/wafanyakazi ili ziamke na kutoa majibu ambayo kamwe Jiwe hakuyatarajia
....yajayo yanafurahisha
Haaaaa Nilidhani Niko peke yangu Hongera kingu hiyo ndo siasa
 
Hebu wabunge wakatawe 50% ya mafao yao kwaajili ya ujenzi wa viwanda ili tuone uzalendo wao. Rubbish
 
Huyo Kingu anataka Watanzania wastaafu waishi maisha ya dhiki kama wapiga kura wa jimboni kwake, pesa ya kwangu kwa nini iwe eti ndo inajenga uchumi wa nchi wakati kodi kila mwezi nakatwa, hiyo kodi inafanya kazi gani?
Ni unyanyasaji na uonevu wa Hali ya huu Sanaa .poleni sana watumishi wa serikali hii.mko kwenye wakati mgumu sanaaa
 
Hivi huwa inakuwaje mtu anaomba awaongoze lkn akishapata huo uongozi anaanza kuwafanyia mabaya mliomchagua???.
Imagine MAGUFULI na Wabunge wake wa CCM wangelikuwa ni wafanyakazi wa kawaida tuu huku uraiani, ni kweli wangeifurahia hii sheria kandamizi kwa wafanyakazi wa nchi hii???.
Ni kwa nini CCM wanakuwa na roho mbaya kiasi hiki???.
Bora mjionee sasa msifanye makosa 2020
 
Hata mimi hasira niliyo nayo acha tu nijiepushe na ban, lkn huyu si ndio pia alileta hoja ya mtukufu kuongezewa muda magogoni!
 
CCM mna laana, Elibariki Kingu alivyochorwa na CAG Ufisadi wa 101M

52569.jpg

OKW BOBAN SUNZU
JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
rep.png
24,668
like.png
22,084
point.png
280
Apr 26, 2016#1
CCM mme laaniwa, mnaiba hela katika ngazi zote za nchi hii, mnaiba kuanzia ngazi za wizara mpaka mashinani,mpaka kimataifa kwa kuanzisha makampuni hewa ya kimataifa ya kuibia hela.

Leo nawaletea udondozi wa ripoti ya CAG huko Igunga Tabora , kuna mambo yamnistua. Hivi wizi ndio sifa kwa CCM kumpa mtu cheo?Kwa ufisadi ninaousoma hapa kwenye repoti ya Hamashauri ya Igunga, basi Elibariki Kingu, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na baadae kuwa mbunge wa CCM Singida,inasikitisha na kutia hasira.

Halamshauri imepata hati ya mashaka……………..CAG anasemaje katika ripoti yake? Yapo mengi, mengine zungumza wewe mimi najikita kwenye ufisadi wa SHS.101,174,585 unaomuhusu Mbunge huyo moja kwa moja.

1. Imepigwa milioni 95 fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

Katika ripoti ya CAG imeelezwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Pinda kupitia Wizara ya Habari na Michezo alitoa 90m kwa Halmashauri ya Igunga ili zikopeshwe kwa vikundi vya vijana. Kingu alikuwa mlezi wa vikundi hivi. Kama mnakumbuka kuna kipindi alianzisha vikundi vikawa maarufu sana vikijihusisha na kilimo cha vitunguu na mpunga. Halmashauri ilipopokea pesa ikaongeza na 5M kama mchango wake ikalipa kwa Vijana SACCOS milioni 95 tarehe 7/10/2013 kupitia vocha 1/9, Cheque No.804 kisha Vijana SACCOS ikakiri kupokea pesa hiyo tarehe 7/10/2013 risiti no.0135. Ikumbukwe kwamba SACCOS hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Kingu.

Ripoti inasema kwamba SHS.26,700,000 tu ililipwa kwa vikundi vitano vilivyokusudiwa. SHS.80,800,000 zililipwa kwa vikundi hewa ikiwepo akaunti ya Kingu SHS. 24,000,000 na mfanyabiashara Zengo SHS.15,000,000

Ripoti inaongeza kuwa Elibariki alidanganya mbele ya Waziri Mkuu Pinda, Mkuu wa Mkoa, Naibu waziri wa Michezo na makamera ya TBC kwa kuonyesha shamba la mpunga hewa. Lilionyeshwa shamba la mtu mwingine akidanganya kwamba ni la kikundi.Aidha ripoti inadokeza kuwa mpaka sasa hakuna hata senti iliyorejeshwa kwa kuwa vikundi hivyo pamoja na SACCOS viliyeyuka mara tu baada ya pesa kugawanywa.

2. Mkopo toka halmashauri kwenda kwa DC safari ya China SHS.6,174,585

Ripoti inasema kuwa Mh.DC alikopeshwa SHS.6,174,585 na halamshauri kwa ajili ya safari ya kwenda China kwenye mafunzo 2/8/2014 to 21/8/2014. Hata hivyo CAG anatilia mashaka kuna uwezekano safari hiyo ilikuwa hewa kwani pesa ililipwa 12/1/2015 wakati barua ya mwaliko ilisema ni mafunzo ya 2/8/2014 to 21/8/2014.

Hata hivyo mkopo huo haukuwahi kurejeshwa na bwana huyo. Haaaaa haaaaa huu si usanii wakuu?

PCCB wa Igunga mko wapi jamani, mpaka CAG atoke Dar aje kugundua yote haya na nyie mpo tu……..haya nawamegea huu udondozi toka kwenye Management Letter ya CAG 2014/2015.

CCM mna laana, Elibariki Kingu alivyochorwa na CAG Ufisadi wa 101M - JamiiForums
 
Aiseee Huyu Jamaa ana tatizo kweli na nadhani uelewa wake mdogo kweli!

Hivi kumbe lengo la kuzuia hayo mafao sio kufanya hiyo mufuko iwe imara sio kumsaidia mstaafu kama mnavyo inadi hiyo Sera?

Kwahiyo anaamini Tanzania ya viwanda itawezekana kwa kuzuia hayo mafao ya wastaafu?
Kingu haraka ya kutafuta sifa, mbona spika kasema bunge halihusiki? Ubinafsi huu wa watu kama kina kingu kwa tamaa ya madaraka ndio unaangamiza taifa.
*Bunge lajivua lawama*

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limejivua lawama juu ya kanuni mpya ya pensheni ambayo imetangazwa hivi karibuni ya mstaafu kulipwa asilimia 50 ya mafao yake baada ya ukomo wa ajira.

Kanuni hiyo iliyotangazwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pia inabainisha kuwa katika kiasi cha fedha kinachobaki, mstaafu huyo atalipwa kama mshahara kwa miaka 12.

Kutokana na suala hilo ambalo limeibua mjadala mzito kila kona huku wananchi na baadhi ya wanasiasa wakipinga, Spika wa Bunge, Job Ndugai, jana aliibuka na kuweka bayana ukweli huku akisema Bunge halihusiki katika suala hilo.

Sambamba na kuweka wazi suala hilo, Ndugai pia alisema bunge linaweza kuingingilia na kuagiza kanuni hiyo ifanyiwe mabadiliko kama inaonekana ni kandamizi.

Akizungumza na Nipashe Jumapili kwa njia ya simu, Ndugai alisema kanuni hiyo ambayo inalalamikiwa haijatokana na chombo hicho cha kutunga sheria kwa kuwa kazi ya kutunga kanuni ni ya serikali kupitia wizara husika na sheria iliyopitishwa.

“Hii si sheria bali ni kanuni na kwa kawaida bunge lilishatunga sheria, hatua inayofuata ni kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya kutiwa saini. Lakini kabla ya kuanza kutumika, wizara yenye dhamana na sekta husika inatunga kanuni na kuzitangaza katika Gazeti la Serikali,” alisema.

“Sasa kwa jambo hilo ambalo limeibua mjadala mzito, Bunge limetwishwa mzigo mzito lisioustahili na hata watu wamefikia hatua ya kunishambulia mimi binafsi. Ukweli ni kwamba katika hili, Wizara yenye dhamana na sekta ya hifadhi ya jamii (Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ndiyo iliyotunga kanuni hiyo,” aliongeza.

Ndugai pia alimsifu Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya, ambaye pia ni Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), aliyeibua suala hilo juu ya pensheni hiyo.

Alhamisi wiki hii, Bulaya aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kikokotoo hicho kipya kilichotungwa na serikali ni kitanzi kwa wastaafu kwa kuwa hawatanufaika na fedha zao ambazo wamezitolea jasho kwa miaka mingi.

“Kwa kweli alichokisema Mheshimiwa Bulaya ni kweli na ameweka wazi kwamba imetokana na serikali na Bunge halihusiki,” alisema.

Katika taarifa yake kwa wanahabari, Bulaya alikaririwa akisema: “Wabunge tulitaka kikokotoo kiwepo kwenye sheria, lakini kwa masikitiko makubwa bungeni tuliambiwa kuwa ni kanuni ambayo inampa waziri ambaye yuko kwa maslahi ya serikali.”

Bulaya aliongeza kuwa, hata wadau waliwataka wabunge wakijue kikokotoo hicho na waliomba kisiwe 1/580 bali kiwe 1/540 au pungufu, lakini kilifichwa na hakikujulikana kwa watunga sheria hao.

Pamoja na bunge kutowekwa wazi, kwa mujibu wa Bulaya, SSRA hivi karibuni iliweka bayana suala hilo na hatimaye kuibua mjadala mzito kila kona huku baadhi ya wananchi wakisema ni ukandamizaji dhidi ya wastaafu.

*ATOA MATUMAINI*

Spika Ndugai alitoa matumaini kuwa suala hilo si kwamba limefika mwisho bali Bunge linaweza kuliibua tena kwa mujibu wa kanuni yake na hatimaye kuagiza lifanyiwe mabadiliko.

“Bunge linayo nafasi ya kuingilia kati juu ya jambo hilo na lolote lile ambalo wananchi au wadau wanaona haliwatendei haki. Kamati ya Sheria Ndogo chini ya Mheshimiwa Andrew Chenge, inaweza kusimamia hilo kwa niaba ya Bunge na kukafanyika mabadiliko,” alisema.

Ndugai alisema hatua hiyo inaweza kufikiwa iwapo mbunge ataonyesha nia ya kufanya hivyo au kupokea malalamiko kutoka kwa wadau ambao ni wananchi.

“Baada ya kufikiwa hapo, bunge kupitia Kamati ya Sheria Ndogo itachambua na hatimaye kuiagiza serikali kufanyia marekebisho. Kwa hiyo wananchi wasione kama jambo hili limefika mwisho,” alisisitiza.

*MAONI YA WANANCHI*

Baada ya Bulaya kuibua jambo hilo, baadhi ya wananchi walionyesha kushangazwa huku wakilitupia lawama Bunge kwa kile walichadai kuwa limetunga sheria inayokandamaiza wastaafu.

Baadhi ya wananchi hao, wakiwamo wafanyakazi waliozungumza na Nipashe jana, walielezea kushtushwa na kanuni hiyo wakiielezea kuwa ikitekelezwa itaminya haki za wastaafu hasa baada ya kazi ngumu ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu.

Ali Dande, mkazi wa Sinza Moro, alielezea kushangazwa kwake na wabunge kukubaliana na kanuni hiyo iliyotangazwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakati wao wakistaafu wanalipwa kiinua mgongo chao chote, tena bila masharti.

"Leo hii hata ukikosa kazi huwezi kuchukua mafao yako hadi ufikishe miaka 60, sasa wakati bado hatujasahau machungu haya wanatuletea lingine kwamba tusilipwe mafao yetu yote tulipwe asilimia 25 tu jamani? Mimi nashauri mtu anapostaafu apewe stahili zake aende akafanye anachokijua mwenyewe maana hela ni zake si za serikali," alisema

Hellen Murya, mkazi wa Yombo Temeke, alisema atashangaa kuona kama wabunge watakaa kimya kuruhusu kanuni hiyo iendelee kutekelezwa kama ilivyo kwa sababu inakandamiza haki za Watanzania wanyonge.

"Kama wabunge wetu hawatapaza sauti kuhusu hili nitawashangaa sana na Watanzania wanawashangaa kwa sababu hiki ni kitu cha ajabu. Fedha za wanyonge zinataka kutumiwa kwenye mambo mengine kwa kisingizio cha kumlipa kidogo kidogo mshahara kwa miaka 12. Kwa nini umpangie matumizi mstaafu mafao ambayo ni stahili yake?" alihoji.

*Chanzo ni Gazeti la Nipashe*
 
CCM mna laana, Elibariki Kingu alivyochorwa na CAG Ufisadi wa 101M

52569.jpg

OKW BOBAN SUNZU
JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
rep.png
24,668
like.png
22,084
point.png
280
Apr 26, 2016#1
CCM mme laaniwa, mnaiba hela katika ngazi zote za nchi hii, mnaiba kuanzia ngazi za wizara mpaka mashinani,mpaka kimataifa kwa kuanzisha makampuni hewa ya kimataifa ya kuibia hela.

Leo nawaletea udondozi wa ripoti ya CAG huko Igunga Tabora , kuna mambo yamnistua. Hivi wizi ndio sifa kwa CCM kumpa mtu cheo?Kwa ufisadi ninaousoma hapa kwenye repoti ya Hamashauri ya Igunga, basi Elibariki Kingu, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na baadae kuwa mbunge wa CCM Singida,inasikitisha na kutia hasira.

Halamshauri imepata hati ya mashaka……………..CAG anasemaje katika ripoti yake? Yapo mengi, mengine zungumza wewe mimi najikita kwenye ufisadi wa SHS.101,174,585 unaomuhusu Mbunge huyo moja kwa moja.

1. Imepigwa milioni 95 fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

Katika ripoti ya CAG imeelezwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Pinda kupitia Wizara ya Habari na Michezo alitoa 90m kwa Halmashauri ya Igunga ili zikopeshwe kwa vikundi vya vijana. Kingu alikuwa mlezi wa vikundi hivi. Kama mnakumbuka kuna kipindi alianzisha vikundi vikawa maarufu sana vikijihusisha na kilimo cha vitunguu na mpunga. Halmashauri ilipopokea pesa ikaongeza na 5M kama mchango wake ikalipa kwa Vijana SACCOS milioni 95 tarehe 7/10/2013 kupitia vocha 1/9, Cheque No.804 kisha Vijana SACCOS ikakiri kupokea pesa hiyo tarehe 7/10/2013 risiti no.0135. Ikumbukwe kwamba SACCOS hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Kingu.

Ripoti inasema kwamba SHS.26,700,000 tu ililipwa kwa vikundi vitano vilivyokusudiwa. SHS.80,800,000 zililipwa kwa vikundi hewa ikiwepo akaunti ya Kingu SHS. 24,000,000 na mfanyabiashara Zengo SHS.15,000,000

Ripoti inaongeza kuwa Elibariki alidanganya mbele ya Waziri Mkuu Pinda, Mkuu wa Mkoa, Naibu waziri wa Michezo na makamera ya TBC kwa kuonyesha shamba la mpunga hewa. Lilionyeshwa shamba la mtu mwingine akidanganya kwamba ni la kikundi.Aidha ripoti inadokeza kuwa mpaka sasa hakuna hata senti iliyorejeshwa kwa kuwa vikundi hivyo pamoja na SACCOS viliyeyuka mara tu baada ya pesa kugawanywa.

2. Mkopo toka halmashauri kwenda kwa DC safari ya China SHS.6,174,585

Ripoti inasema kuwa Mh.DC alikopeshwa SHS.6,174,585 na halamshauri kwa ajili ya safari ya kwenda China kwenye mafunzo 2/8/2014 to 21/8/2014. Hata hivyo CAG anatilia mashaka kuna uwezekano safari hiyo ilikuwa hewa kwani pesa ililipwa 12/1/2015 wakati barua ya mwaliko ilisema ni mafunzo ya 2/8/2014 to 21/8/2014.

Hata hivyo mkopo huo haukuwahi kurejeshwa na bwana huyo. Haaaaa haaaaa huu si usanii wakuu?

PCCB wa Igunga mko wapi jamani, mpaka CAG atoke Dar aje kugundua yote haya na nyie mpo tu……..haya nawamegea huu udondozi toka kwenye Management Letter ya CAG 2014/2015.

CCM mna laana, Elibariki Kingu alivyochorwa na CAG Ufisadi wa 101M - JamiiForums
PCCB hawana uwezo wa kugundua wizi wa aina yo yote mpaka watumwe!
 
Acheni kuchochea chuki; dhalau zenu zidi ya wafanyakazi zimepita kipimo cha kawaida. Mmetusukuma mpaka kwenye kona na bado mnaendelea kututemea mate usoni.

Mmetufanya tuishi kama vijakazi katika nchi yetu wenyewe; Kiburi chenu zidi yetu kimetamalaki sana ;lakini kikombe hiki kalibu kinajaa.
 
Yaani Kingu ni kati wa wabunge wa hovyo kabisa kutokea nchi hii. Mbona wao wabunge hawasubiri wafikishe miaka 60 ndipo wapewe mafao yao? Wanataka wapewe baada ya kumaliza kipindi chao cha miaka mitano?
 
Kweli wabunge wa ccm ni janga la taifa. kwaiyo uyo boya hapo kaona kajenga hoja sana? sijui hata kama anaelewa anachosema
Hapa ndipo inadhihirika pasipo na shaka kwamba wabunge wa ccm ni wanafiki na waongo kwani kuna gazeti moja liliandika kwenye kichwa chake cha habari Eti wabunge wa ccm wanadai kuwa kipengele cha 25% kilifichwa wakati mswaada huo unapelekwa bungeni na kwamba na wao hawakiungi mkono, sasa haya anayosema Kiula ameyatoa wapi ?, au anamuwakilisha nani ?, Upi ndio msimamo wa wabunge wa ccm kwenye hili ??
 
Haya mliosema wabunge wa ccm hawajitambui. Je, huyu pia hajitambui?
 
Niliwahi kuambiwa na mtaalamu wa saikolojia kuwa mwendawazimu huwa anajiona yeye kuwa mjanja, ana akili sana, na mwerevu kuliko wengine wote.
 
Sasa wameamua kupiga kura ya wazi kusimamia kile watanzania walichohisi ni ujinga, ni upumbavu labda walifanya kwa bahati mbaya uu
 
Back
Top Bottom