Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Jamaa ni Lijizi Sana cha kushangaza fedha zote linahonga,limewekeza kwa mchepuko kamnunulia hadi Range Rover,Mchepuko wake full bata halafu linataka wazeee wapewe 25% tu wakistaafu wakati lenyewe ndio fisadi na jizi kweli kweli hadi ccm kupitia uhuru wakalikataaa!
Ngoja 2020 akatwe ubunge mbona huwa hamjali yule mchepuko ulio mzalia naona anamjali mmoja tu.
 
Wabunge wa CCM Tusiyumbe.

Nimeanza kwa Wabunge wa CCM kwa sababu kubwa kwanza sisi chama chetu ndicho kilicho na dhamana ya kuwaongoza watu wa nchi hii.

Lobbing zimeanza za Makampuni makubwa ya Migodi kupinga sheria ya Fao la kujitoa.makampuni binafsi nayo yataanza soon kupinga uamuzi huu kwa maslahi ya wachache Maslahi yasiyozingatia maono ya nchi na Usalama wa Taifa.Maslahi yanayoangalia siasa za muda za kuwafurahisha wanaharakati huku taifa likikosa nguvu ya kiuchumi.

Nawatahadharisha wabunge wote na hasa wa Chama changu CCM,tuwe makini na kila move hasa kipindi hiki ambacho Rais Magufuli amekuja na mwanga juu ya hatma ya viwanda vya nchi hii;Magufuli ameamua nchi iwe ya viwanda kupitia Mifuko hii ya kijamii,Lakini naona mapandikizo yakutaka kuidhoofisha mifuko hii,Mipango hii wanajua wanaoiratibu nia yao lakini wabunge wenzangu na wana CCM fao lakujitoa ni miongoni mwa mipango ovu ya kutaka kumdhoofisha Rais Magufuli na kudhoofisha mapato ya mifuko hii iliyoelekezwa kusimamia mageuzi ya viwanda nchini.

Kwanini watanzania kila jambo tuliwekee siasa?Uimara wa mifuko.ya kijamii popote duniani ndio kiini cha Usalama wa Taifa,Usalama.wa nchi katika kila nyanja iwe ya dharura za kiulinzi au kukuza uchumi hii ni roho ya nchi hasa nchi Hizi zinazoendelea.

Tuwe makini sana juu ya hawa wanaotaka kuturudisha nyuma.Rais anadira ya viwanda,Mifuko hii imepewa jukumu hili kwanini tuanze kutaka kuwadhoofisha.Kwa haraka haraka NSSF wanaweza kuokoa karibu biln 60 pesa ambazo kwa nchi changa kama hii zikiwekezwa kwa busara na uzalendo zinalifanya taifa lipae kiuchumi.

Watanzania tuache siasa pesa hizi ni za watanzania wakifikisha umri unaostahili watalipwa nchi hii lazima itangulize maslahi ya wengi kwa faida ya vizazi,tuache harakati na siasa za kutaka sifa kwa mambo mazito yanayogusa ustawi na usalama wa nchi.

Tuache mifuko ikusanye pesa a kuwekeza kwenye viwanda .Tuache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja.

Kingu Elibariki
MP Singida West
Huyu Ms3nge nini? Mafao yetu ndio ya kujenga viwanda? Unajua Kuna wapumbavu wanakera Sana nchi hii? Yeye si alimaliza miaka mitano anakula gratuity yake anasepa?
 
Ngoja 2020 akatwe ubunge mbona huwa hamjali yule mchepuko ulio mzalia naona anamjali mmoja tu.
Huyo Mshenzi harudi 2020 tunaminya MAMBUPU na kumsomea kisomo huyo mbweha,amewatukana wazeee na wafanyakazi nchini......Yule mchepuko naona MC pilipili alimzidi Kete.....Ila Huyu wa sasa naona katulia nae coz bado kabinti kabichi....chuchu saa 6 kasoro.
 
Huyo Mshenzi harudi 2020 tunaminya MAMBUPU na kumsomea kisomo huyo mbweha,amewatukana wazeee na wafanyakazi nchini......Yule mchepuko naona MC pilipili alimzidi Kete.....Ila Huyu wa sasa naona katulia nae coz bado kabinti kabichi....chuchu saa 6 kasoro.
Kazaa na nicole wa Mc pilipili Ila ndo kamtosa kabaki na huyo mmoja.
 
Hivi sikuwa najua hii ni sera ya ccm ili isiangushwe. Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!
 
Aisee, Mungu ndo anajua na ndiye atamlipa kila atungaye sheria kandamizi. Tz mishahara ya mfanyakazi wa chini kabisa inampa kula na kuvaa tu, mafao yalikuwa yanasaidia kama watoto kusoma na kupata angalau kibanda cha kuishi, wale wanaolipwa mamilioni wameamua kuchukua na kidogo hicho Mungu anawaona.
 
dah unajua unaweza kula ban ingawa nna miaka 7 jf siijui ban
Kwanini nanyie wabunge msipewe 25% ila wstumishi tu? Nyie wabunge wa ccm mtakuja kuiingiza nchi kwenye machafuko kabisa.
 
Wafanyakazi walimu na watendaji ndio vinara wa kuiba kula na kuipigia kula ccm
Acha wapate haki yao tuisome namba pamoja
 
Hivi huwa inakuwaje mtu anaomba awaongoze lkn akishapata huo uongozi anaanza kuwafanyia mabaya mliomchagua???.
Imagine MAGUFULI na Wabunge wake wa CCM wangelikuwa ni wafanyakazi wa kawaida tuu huku uraiani, ni kweli wangeifurahia hii sheria kandamizi kwa wafanyakazi wa nchi hii???.
Ni kwa nini CCM wanakuwa na roho mbaya kiasi hiki???.
 
Kwa kuwa wanaamini katika nguvu ya jeshi na dola hakuna namna watawaheshimu wapiga kura wao.Ila wanasahau kuwa hayo maflyover na madaraja yanajengwa na watumishi wa umma.Wakurugenzi wa halmashauri ni watumishi wa umma.Wastaafu na ndugunna familia zao ni watumishi wa umma.Ipo siku.
 
Tuache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja.
kingu, muache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja?nyie wabunge mnafanya kazi kipindi cha miaka mitano halafu unachukua kiinua mgongo chako chote huoniaibu unataka mfanyakazi mfanyakazi apewe asilimia ishirini na tano.
 
Back
Top Bottom