Kingereza ni lugha kama lugha nyingine tu. Wakati wa asubuhi salamu ni, "Goodmorning", kwa kihehe ni, "Kamwene", n.k. Tatizo ni kua Kiingereza tumekihukumu kua ni lugha ya "majuu" au ya "watu weupe-wazungu" hivyo si rahisi kuijua na wanaoijua wakiitumia popote pale tunawabeza kwamba "wanajifanya" wazuungu! Lakini kwa anayetaka kukijua ni rahisi tu kuliko hata bei ya peremende. Lengo lako ni nini katika kujua lugha hii? Hilo ni swali la gharama kubwa sana, tafuta jibu lake kisha jifunze si tu Kiingereza bali hata Kichina, Kijerumani, Kichaga, Kiafrikaan, nk.