King'amuzi cha Abu Dhabi Sports ni vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

King'amuzi cha Abu Dhabi Sports ni vipi?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Ibrah, May 21, 2012.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kuna fundi wa madishi amenijulisha juu ya King'amuzi cha Abu Dhabi Sport. Ameniambia kuwa ni cha michezo tu na kupitia Abu Dhabi sports decorder nitapata hata ligi za soka za Amerika Kusini. Amedai kuwa king'amuzi hicho ni nafuu sana kwa kuwa kinalipiwa Usd 100/- kwa mwaka, ingawa gharama zake za awali ni kubwa kama usd 400/- (pamoja na ada ya mwaka), amenitaka ninunue na sat. dish la futi 8 ambalo ni maalumu kwa ajili ya Abu Dhabi Sports tu na litatazama magharibi.
  Mlofunga hilo dish, je kuna ukweli?
   
 2. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,768
  Likes Received: 7,076
  Trophy Points: 280
  yah ni kweli na watu wanaoonesha soccer kwenye mabanda wanatumia abudhabi sport badala ya dstv ligi ya uingereza unaona mechi zote kwa wiki

  -ila kuna tetesi hazijawa confirmed kua aljazeera sport nae anataka umiliki kama wa abudhabi sport so huenda ikatokea yale ya g-sport na super sport ya kugawana mechi so endelea kuuliza uliza mkuu
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Ipo mkuu na infanya kazi fresh kwa kadi moja au mbili kwa pamoja na Aljazeera.ila ukiagiza Dubai utapata kwa around 300$
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sasa huyo fundi hakukueleza utapata vipi?

  humu kila siku tunaulizia hiko king'amuzi
  but kila mtu anasikia sikia tu kama wewe
   
 5. m

  mekwedweet Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Naomba namba ya huyo fundi/agent na mini nahitaji
   
 6. Mchana

  Mchana Senior Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 181
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  +255754012513
   
 7. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hicho King'muzi ni kweli kipo,gharama kubwa ni ya awali lakini malipo yake ya mwezi ni nafuu sana ukilinganisha na Dstv,Dstv kwa mwezi Usd 89 wao kwa mwaka usd 120 angalia tofauti ilivyo kubwa ,mimi ninazo zote ya Dstv Na Abudhabi (ADD),Abudhabi kwa sasa wanaonyesha ligi ya Uingereza tu ligi ya Spain na zingine hawaonyesha labda upate kadi ya pili ya Aljazeera. Ambacho na mashaka nacho ni haki ya kuendelea kuonyesha ligi ya Uingereza msimu huu watapewa tena? Kua makini kidogo kabla ya kununua gharama za kununua ni kubwa .Channel zingine ambazo siyo za michezo na pia za free ziko nyingi tu japo ni za Kiarabu.
   
 8. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Jaribu Dar mtaa wa Livingstone na Udowe dukani kwa Levi.
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kinaitwa Ad Sports Abudhabi. Kama una jamaa yako anaenda Dubai waweza kumwagiza ila ukinunua hapa Bongo kunaongezeka dola 100/-. Au tafuta kwenye search engine labda wanaweza kukutumia kwa posta.
  Nimesikia unaweza kutumia kadi mbili kwa wakati mmoja, Abudhabi Sports na Aljazeera Sports au moja kati ya hizo.
   
 10. T

  Thugnificent New Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilifikiria kujiingiza huku lakini nasikia hivi karibuni mkataba wa kuonyesha premiership utaisha. Huenda ikapata haki ya matangazo kampuni nyingine ukabaki umedodewa na king'amuzi na dish lako la Abu-Dhabi. Wenye information zaidi waendelee kuzimwaga hapa, lakini sasa hivi bado ni vizuri kuangalia upepo unaendaje kwanza kabla ya kuwekeza hizo dola.
   
Loading...