Kinana unasema Demokrasia imekua. Ni Demokrasia ipi unayoiongelea?

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Umejitokeza kwenye Kongamano linalohusisha ukuaji wa Demokrasia na unasema demokrasia imekua kwa kiwango kikubwa nchini. Je, ni demokrasia ipi unayoiongelea wewe?

Wakili Madereka yuko akishikiliwa na Polisi huko Arusha kisa amekosoa na kupinga Mkataba wa DP-WORLD.

Ni Demokrasia ipi hiyo iliyokua, wakati Dkt. Slaa, Wakili Mwabukusi na Mwanaharakati Mdude Nyagali bado wanasumbuliwa na Polisi kwa sababu wametoa maoni yao na kupinga Mkataba mbovu wa DP-WORLD? Ikafikia mahali hata wanakamatwa kwa mfumo wa "utekaji"!

Hapa tunaandika, wao hata simu na laptop zao bado zimeshikiliwa na Polisi ingawa imeshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao na kulazimika kuwaachia baada ya sauti huru kuwazidi nguvu kutoka ndani na nje ya nchi.

Tunayo mifano mingi sana ya kuzuia wananchi kutoa maoni yao. Ila pia unakumbuka ile clip yenu ovu enzi mkiwa benchi?

Mfano halisi ni huu wa sasa ambapo serikali imezuia vyombo vya habari kuchapisha waraka wa maaskofu wa madhehebu ya kikatoliki nchini TEC, kwa kupewa amri na Serikali kupitia Waziri wa habari huyu ambae ni Nape Nnauye.

Kinana hana hata aibu mbele ya watanzania anasimama kuongea pumba. Watanzania wa sasa sio wa jana!
 
Hakika.
Hadi kuifikia angalau demokrasia nusu, itatuchukua miaka mingi sana ijayo😎

Hili la viongozi wa dini wanapoisifu CCM, kuwa hawachanganyi dini na siasa!

Ila pale viongozi hao hao wa dini wanapousema ukweli kuhusu kulinda rasilimali za nchi, wanaambiwa wanachanganya dini na siasa!
 
Hawa jamaa wamejisahau ndani ya kipindi kifupi sana!

Ila wanachokosea ni kudhani watanzania wa leo ni sawa na wale wa 2010.
 
Back
Top Bottom