Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,405
- 114,358
Tuliambiwa kwamba Rais Samia karejesha demokrasia, amani, utulivu, haki, n.k.
Twende mbele mpaka leo hii ambapo kuna watu waliandamana kupinga mkataba wa serikali na kampuni ya DP kutoka Dubai.
Vijana wamejitokeza na mabango yao na wakaingia barabarani ili kuonyesha kutokufurahishwa kwao na matakwa ya huo mkataba.
Hiyo ni haki yao kabisa inayolindwa na katiba. Ni haki yao ya kikatiba.
Lakini cha ajabu, wameishia kuchezea virungu vya polisi wa Samia na wengine wamekamatwa na kupandishwa kwenye Difenda za polisi.
Kosa lao ni lipi? Eti ni kuandamana!
Sielewi! Toka lini haki iliyopo kwenye katiba ikawa ni kosa?
Demokrasia aliyoirejesha Samia ni ipi hasa?
Wakishindwa hoja, wanaanza kutumia mabavu.
Kama huo mkataba hauna ubaya wowote, basi waache kutumia mabavu.
Hoja hujibiwa kwa hoja.
Ukianza kujibu hoja kwa mabavu, basi ni ushashindwa. Unalazimisha tu.