Niliandika barua kwenda kwa wafadhili wa serikali ya Samia nikilalamika kuwa misaada yao inakandamiza demokrasia na mfumo wa haki nchini

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Tarehe 25 November 2023 Niliandika barua kwenda kwa wafadhili wa serikali ya Tanzania wakiwemo USA, bunge la Ulaya na wengine nikilalamikia ufadhili wao kuuwa demokrasia na mfumo wa utoaji haki nchini.

Katika barua hiyo ambayo nimeambatanisha kivuli chake hapa nimelalamikia mambo saba ambayo yanagusa bunge, serikali na mahakama.

Miongoni mwa mambo hayo ni fukuza fukuza ya wananchi katika maeneo yao ya asili bila kufuata sheria sehemu mbalimbali ya nchi ikiwemo Loliondo Arusha, Ndolezi Mbozi mkoani Songwe, Mbarali Mbeya na Tanganyika Rukwa.

Katika hoja nyingine nimelalamikia mawakili wa kujitegemea wanavyofanyiwa hila na vyombo vya dola ikiwemo kuvuliwa uwakili hasa wale watetezi wa haki za Binadamu. Nimeeleza pia namna ambavyo mahakama nayo imekuwa ikitumika kuchelewesha na kukwamisha haki katika kesi zote ambazo serikali ina maslahi dhidi ya wananchi.

Nimeeleza pia namna ambavyo utawala wa Samia hauheshimu sheria na katiba ya nchi ikiwemo kukumbatia wabunge 19 ambao hawana sifa ya kuwa wabunge kikatiba, kudharau maamuzi ya mahakama ya Africa Mashariki kuhusu kuhamisha watu Ngorongoro n.k.

Nimeeleza pia kuhusu namna polisi walivyotumika kuzuia maandamano ya amani kwa bunduki za kivita yaliyotarajiwa kufanyika Mbeya 9 November 2023.

Tunashukuru kwa kuwa wote tuliowapelekea barua hii walitupa ushirikiano. Hatuna namna tutaendelea kuandamana huku tukiwashtaki kwa wafadhili wao mpaka pale tutakapokuwa na katiba mpya bora yenye mifumo mizuri na taasisi huru.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Screenshot_20240229-174751_1~2.jpg
Screenshot_20240229-175134_1.jpg
Screenshot_20240229-175154_1.jpg
 
Back
Top Bottom