Kweli mkuu,
Hakuna gazeti lolote lililotoa hii taarifa, ila ukweli ni kwamba Kinana amefungua mashtaka dhidi ya Msigwa rasmi. Habari zaidi nitaendelea kuweka, na kama kuna mtu anaweza kuzileta pia itakuwa ni jambo jemba kwa maslahi ya wanaJF wote.
Cheki ulivyo mshamba bavicha hata akili hamnazo...siyo UMBEYA ni UMBEA hili vipi.
Baada ya masahihisho yako umepata ushahidi wowote kutetea hoja yako kwamba msigwa amropokaji? Marangapi na katika mahakama zipi ametibitishwa kuwa mropokaji?
Umbeya au umbea vyovyote vile ujumbe umekufikia
Kwa hiyo Lumumba imeshapanga matokeo. Mnatapa tapa kama kuku aliyekatwa shingo.
Kwa hiyo Lumumba imeshapanga matokeo. Mnatapa tapa kama kuku aliyekatwa shingo.
WanaJF. Hakuna cha kujadili hapa kwa kuwa mleta mada hana uhakika na taarifa yake wala source. Funga hii mada mpaka utapopata habari kamili na yenye reliable source - then ujipange tena upya.
Mkuu, sidhani kama Kinana angukuwa na ujasiri wa kwenda mahakamani na kufungua mashtaka kwa Msigwa kama kweli angekuwa jangili au kujihusisha na vitendo hivyo kwa nama yoyote ile.
Mtu mzima akiumbuka huchutama, mkuu wewe umeumbuka kwani umeshindwa kutofautisha kati ya "UMBEYA" na "UMBEA", mimi ningekushauri huchutame.
Mkuu,
Kwa wanasheria wataelewa hapa, kuna hii ishu inaitwa defarmation, nadhani ndio litakuwa shitaka namba moja kwa mchungaji Msigwa, na utakumbuka kutokana na kashfa hiyo kuwa Kinana ni jangili, ili sababisha Kinana avunje makubaliana na partners wake na ili m-cost si chini ya milioni 300 pesa za Tanzania. Sasa unaweza kupata picha ya hiyo fidia atakayolipa Msigwa kwa Kinana.
Mbona Rostam alitishia kumshtaki Mengi kwa kumuita Fisadi papa lakini mpaka leo kesi haipo na Mengi hakuomba msamaha sijui huyu HAMY-D akili amepeleka wapiSasa angefanyeje ilhali keshautangazia umma kwamba asipoombwa msamaha ataenda mahakamani? Hizi tabia za kukimbilia mahakamani zinawahusu CCM wote. Hujiulizi walipata wapi ujasiri wa kuwapeleka mahakamani akina Lwakatare, Kileo na makamanda wengine kwa mashitaka ya ugaidi huku wakijua ni mashitaka ya kutunga? Hiyo ni hulka tu ya CCM kuamini kwamba mahakama ni ya kwao hivyo itawatetea.
Sasa kama Kinana ana ubia na TOLL, na mkurugenzi wa TOLL kakamatwa na pembe za ndovu, kama Kinana anamiliki meli ambazo ndiyo zinaaminiwa kusafirishwa pembe za Ndovu, ni kwa vipi yeye asihusishwe? Kwanini hazijawa meli za watu wengine au bandari ya nchi kavu ya mtu mwingine? Naamini ataifuta tu hii kesi kabla hata haijafika pabaya, maana ushahidi wa mazingira tu unatosha kumtia hatiani.
Mbona Rostam alitishia kumshtaki Mengi kwa kumuita Fisadi papa lakini mpaka leo kesi haipo na Mengi hakuomba msamaha sijui huyu HAMY-D akili amepeleka wapi
Mbona una kichwa kigumu wewe?
Sijasema Kinana anatishia kumpeleka Msigwa mahakamani, nimesema Msigwa kafunguliwa mashtaka rasmi na bwana Kinana mahakamani, sio kutishia.