Kinana amburuza Msigwa kortini

Kinana amburuza Msigwa kortini

Inafahamika Dr W. P Slaa ni safi na makini.

Kama unaushahid kinyume chake peleka mahakamani sio kututapikia matapishi ya maneno na mipasho isiyo na vielelezo wala uShuhuda
Uko kiujumla sana jaribu kubainisha umelenga usafi gani wa mwili au kitabia kwangu mimi sijaona usafi wowote alionao mzee slaa.
 
Msigwa tabia ya kuropoka hajaanza leo ni kitambo tabia hii amekuwa nayo.
Lini ameshawahi kushitakiwa na kuhukumiwa kwa kusema maneno ya uongo?kama hili halijawahi kumtokea basi wewe ndiye mzushi uliyebobea na mropokaji usiyekuwa na haya!
 
Kama unataka kutumia hoja hiyo kumtia hatiani bwana Kinana basi nisewe umepotoka, mahakamani kesi haziamuriwi kwa kutumia ushahidi mwepesi hivyo.

Itakumbukwa kuwa Kinana ni shareholder wa hiyo kampuni ya Sharaf shipping, na ukiwa shareholder haimaanishi una husika na day to day operations za kampuni. Kampuni inakuwa na management na shareholder wapo kwa ajili ya ku-finance na ku-enjoy dividends, sasa iweje Kinana ahusishwe na ujangili au usafirishaji wa pembe za ndovu?, hapo wa kuhusishwa moja kwa moja ni watendaji wa kampuni ya Sharaf shipping na watu wa TRA.

Kuhusu mfano wako; pale Bilicanas kuna vijana uwa wanakamatwa na polisi kwa kubwia unga, je nikisema Mbowe ahusishwe na unga kwa kuwa yeye ni mmiliki wa bilicanas utanielewa?, ni sawa sawa na ndege inavyo wasafirisha "punda" au wabeba unga, huwezi kumuhusisha owner wa ndege kuwa yeye ana husika, ila utawahusisha wale wakaguzi wa airport, nadhani umeelewa mkuu.

Hivi kweli unatumia akili yako! Ninapata mashaka kidogo? Hivi ukiwa transporter gari yako ikikamatwa inasafirisha mali ya magendo ama wizi imekuwaje? Kwa nini kesi nyingine anakuta mwanasheria Mkuu anahusishwa? Huwezi kumiliki ama kuwa na hisa bila kujua chombo hicho kinafanyaje kazi. Yaani wewe ununue hisa tu lakini hujui utapataje gawio lako!
 
aaaah sasa we unampa sifa za nini huyo jangili mpaka mtu anafikia hatua ya kumuita mtu jangili ujue ana evidence za kutosha,nawe umekosa pakupeleka sifa mbona kuna vitu ving tu vizur vinavyotakiwa kupewa sifa sio hilo jangili
 
Naomba sana mahakama itende haki na ikiwezekana hukumu iharakishwe, kwa maana Tanzania nzima inapaswa ielewe kuwa ndani ya CHADEMA hakuna wanasiasa bali kuna wazushi, magaidi na watekaji wa raia, haya yote wanayafanya wao na kisha wanaisingizia serikali kuwa ndio imefanya. Hii ina ingia akilini?

Mahakama imewaumbuwa hakuna ugaid wala kesi ya kigaid

Wewe na kichwa cha savimbi endeleeni na kujishauwa na hiyo ccm-mufilisi
 
Lini ameshawahi kushitakiwa na kuhukumiwa kwa kusema maneno ya uongo?kama hili halijawahi kumtokea basi wewe ndiye mzushi uliyebobea na mropokaji usiyekuwa na haya!
Kichwa chako mkuu ni sawa na nazi tu hakina kitu kabisa.
 
Political strtergist watakwamba this is bad timing...mjadala unafufuka....na unafufuka wakati kuna meno ya tembo yamekamatwa airport....una fufuka wakat TALL kuna matatizo hayo hayo....mjadala utafufuka wakati mbaya...madawa ya kulevya na ujangili umeshamiri....bad bad timing...CCM hamna mwenye AKILI HATA MMOJA...
 
Huku ni kujadili upuuzi,badala uje na habari za uhakika kwamba Msigwa amefungiliwa kesi nambari kadhaa,yenye kumtaka afanye kadhaa, wewe unakuja na urojo eti Ulimwona Msigwa na Tundu mahakamani sii ujinga huu.
Anyway, usiwatoe kwenye mada za msingi watu. Kama zile za kusambaratika CCM Kagera, Aibu ya aina yake kwa Chama na yule jamaa yako kule Iramba jana, kuendelea kufichuka kwa uhusiano wa vigogo na biashara ya madawa/nyara za serikali.
Pia usisahau swali wanalojiuliza wengi,mbona biashara ya madawa na pembe imepamba moto sana kwa kipindi hiki baada ya Katibu Mkuu Mukama kuondolewa na tukielekea uchaguzi wa 2014/15? Jee hii biashara ini mbinu mpya ya kupata pesa za kuendesha kampeni baada ya zile mbinu za EPA kushtukiwa na Upinzani hasa CDM na kukomaa?
Mwisho wanajiuliza, kumrudisha mzee wa mikakati AK ulingoni licha ya yeye kutangaza kustaafu ni kwa vile yeye hizi biashara yeye ni Gwiji kama anavyotuhumiwa na WENGI(sio Msigwa pekee)?

Wewe labda ujaelewa, nimesema Kinana amefungua mashtaka dhidi ya mchungaji Msigwa, na mashtaka hayo yanahusu kauli ya Msigwa dhidi ya Kinana kuwa ni jangili au ana jihusisha na ujangili. Pia hatua hii imefuata baada ya Msigwa kupuuza fursa aliyopewa na kinana ya kwenda kuomba radhi.

Nadhani umeelewa?, hayo mengine uliyojaribu kupotosha hapo ni wazi kuwa una tapatapa kwa kuchomwa na hii thread.
 
Kwani Ndg Kinana yeye ni malaika? Tuvute subira tutakuja ona kama alihusika au hakuhusika. Kwangu mimi nakumbuka msemo wa wanasheria, ''Tatizo si haki kutendeka bali ionekane imetendeka.'' Tutafurahi tukiona HAKI ikionekana kutendeka maana wale majaji aliowasema Mh. Lissu wapo kazini.
 
Naomba sana mahakama itende haki na ikiwezekana hukumu iharakishwe, kwa maana Tanzania nzima inapaswa ielewe kuwa ndani ya CHADEMA hakuna wanasiasa bali kuna wazushi, magaidi na watekaji wa raia, haya yote wanayafanya wao na kisha wanaisingizia serikali kuwa ndio imefanya. Hii ina ingia akilini?
Mkuu kwanini unataka kesi iharakishwe wakati kuna watu wengi mbaka leo hii hajapata haki zao kwa ajili ya msongamano wa kesi,au haki hiko zaidi kwa wanaCCM?

mkuu ndani ya chadema nani ameshawahi kutiwa hatiani kwa kosa la ugaidi?kesi ngapi za CCM dhidi ya CHADEMA zinazohusu ugaidi zimetupwa na mahakama?Mkuu wewe una akili timamu kweli au ni mbayuwayu anayeshabikia siasa bila kuelewa kinachoendelea?
 
Hawajasahau ila wamempuuza, maana ukiongelea list of shame bila ya Dr Slaa kuwa ndani ya list basi hiyo inakuwa sio list of shame tena, maana ni nani asiyejua vitendo vya wizi alivyofanya Dr Slaa ndani ya CHADEMA (kuanzia ule wizi wa milioni 140 mpaka ule udanganyifu wa kwenda Israel na Ujerumani na mchumba wake kwa kutumia pesa za chama).

Nikuulize kitu tafadhali HAMY-D. unapopiga ngumi ukuta nani anaumia. Kadri mnavyojaribu kumchafua Slaa ndivyo anavyoendelea kusikilizwa na kufuatwa kwenye mikutano. Kwanini msijiulize kama hizi slander kwa Slaa zina tija? au la. Mi naona kama hazina tija. You are NOT making a difference guys. kwa nini hamuoni?
 
Naomba sana mahakama itende haki na ikiwezekana hukumu iharakishwe, kwa maana Tanzania nzima inapaswa ielewe kuwa ndani ya CHADEMA hakuna wanasiasa bali kuna wazushi, magaidi na watekaji wa raia, haya yote wanayafanya wao na kisha wanaisingizia serikali kuwa ndio imefanya. Hii ina ingia akilini?

Mkuu haya maneno "Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana kesi hii ya kumshtaki mchungaji Msigwa kwa tabia yake ya kuropoka ovyo ovyo"yameshemwa na nani?acha kutufanya sisi wajinga1ni vema kujenga hoja kuliko kuleta mada ili upate mkate wako wa siku,unakera sana!
 
Nikuulize kitu tafadhali HAMY-D. unapopiga ngumi ukuta nani anaumia. Kadri mnavyojaribu kumchafua Slaa ndivyo anavyoendelea kusikilizwa na kufuatwa kwenye mikutano. Kwanini msijiulize kama hizi slander kwa Slaa zina tija? au la. Mi naona kama hazina tija. You are NOT making a difference guys. kwa nini hamuoni?
Mkuu inawezekana hawa jamaa wakiandika thread ya kumchafua Dr Slaa huwa wanalipwa,huvyo huendelea kufanya hivyo ili wapate ujira wao wa siku bila kujali yalisemwa kwa Dr Slaa yana madhara gani kisiasa!
 
Kweli mkuu,

Hakuna gazeti lolote lililotoa hii taarifa, ila ukweli ni kwamba Kinana amefungua mashtaka dhidi ya Msigwa rasmi. Habari zaidi nitaendelea kuweka, na kama kuna mtu anaweza kuzileta pia itakuwa ni jambo jemba kwa maslahi ya wanaJF wote.

WanaJF. Hakuna cha kujadili hapa kwa kuwa mleta mada hana uhakika na taarifa yake wala source. Funga hii mada mpaka utapopata habari kamili na yenye reliable source - then ujipange tena upya.
 
Uko kiujumla sana jaribu kubainisha umelenga usafi gani wa mwili au kitabia kwangu mimi sijaona usafi wowote alionao mzee slaa.

Unadhani uchafu wa wanaccm umejificha

-Rada chenge na vijisenti

-Richmond lowasa,Kikwete nk

-EPA ccm na Kikwete

-udin ccm na kikwete na uporaji madaraka

- ukabila na ukanda siasa chafu za kibagzi Nape, Mwigulu, Wassira, kikwete na Kinana

-Ujangili, kinana na meno ya tembo

Hiyo ni mifano michache ipo mingi michafu na mauwaji kwa baadhi ya viongozi wa juu serikalini yaani wa ccm
 
Hivi kweli unatumia akili yako! Ninapata mashaka kidogo? Hivi ukiwa transporter gari yako ikikamatwa inasafirisha mali ya magendo ama wizi imekuwaje? Kwa nini kesi nyingine anakuta mwanasheria Mkuu anahusishwa? Huwezi kumiliki ama kuwa na hisa bila kujua chombo hicho kinafanyaje kazi. Yaani wewe ununue hisa tu lakini hujui utapataje gawio lako!

Mbona umerukia mifano mingine mkuu?

Ningependa ujenge hoja ya kuipinga mifano yangu kuhusu madawa ya kulevya!.
 
Kichwa chako mkuu ni sawa na nazi tu hakina kitu kabisa.

Mkuu hili ndiyo jibu la swali nililokuuliza [Lini ameshawahi kushitakiwa na kuhukumiwa kwa kusema maneno ya uongo?]

Mkuu unaakili timamu kweli au naongea na mgonjwa wa akili?
 
Back
Top Bottom