Kinana amburuza Msigwa kortini

Kinana amburuza Msigwa kortini

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana ....

".Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangili ni organized Crime. Ni mtandao wa Kimafia, uko duniani kote, unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea..."

HabariLeo

Hivi na wewe Kinana utajiita mzalendo kweli? katika jambo hili linalohusu rasilimali za taifa badala ya kutoa msaada wako "basi kama hukuhusika watu waliohusika" kukodi meli yako kusafirishia mali za watanzania wote zenye thamani ya mabilioni ya shilingi unadai kusafishwa jina baada ya biashara yako kuyeyuka??????

kwani hukuangalia impact ya kukubali kusafirisha hayo mapembe yetu nje kuwa yakikamatwa itakuwaje?

Acha kutufanya sisi wajinga, kitu kilichofanyika ni kuwa ulijua vizuri zilipitia wapi zilikuwa mali ya nani na wewe ulihusika ndo mana ukatumia mwamvuli wa jina na cheo chako usikaguliwe hapo bandarini.. but kwenye nchi za wenzetu waadilifu UKASHIKWA SHATI!

'swali la kizushi, ''yale madini yaliyokamatwa kwa kuibiwa yaliyotoka nchi jirani wale watu walitiwa ndani kuanzia mmiliki wa bandari kavu na wahusika wooote, kwa nini hili la Tanzania yetu huyu mtu yupo huru na anauhuru wa kufungua kesi???" CCM mna macho? mnadhani watanzania tumelala?
 
Hii ni janja ya nyani ili kumfunga mdomo msigwa asiendelee kuzungumzia sualia la ujangili kwakisingizio kezi iko mahakamani
 
Eti kinana ana uadilifu, kama angekuwa mwadilifu angeshinikiza mh. Tungu lisu akatiwe rufaa dhidi ya ubunge wake wakati muda wa rufaa umepita? Je kinana kama ni muadilifu angeendelea kufanya biashara kwa kutumia wadhifa wake kujitangaza wakati ni kiongozi wa umma? Je kinana kama angekuwa muadilifu na mzalendo angekubali kuwa kampeni meneja wa kikwete mwaka 2010 wakati anajua jk na wenzake walitumia mlungula ili kuwashinda wenzake ndani ya ccm mwaka 2005? Sijajua kama wanasiasa wetu wana vichwa vya aina gani! Wanadhani watanzania ni mazuzu!
 
Ukichunguza sana simba ni mlokole ingawa yeye kula wanyama pori anawaudhi watu. Sasa kama yeye alifunzwa kula nyama taishije?
 
Msigwa pesa yake yote itaishia kumlipa Kinana na asipoangalia kama ana nyumba itauzwa,atutaki longolongo alisema anaushaidi alidai wanamzibia,kwasababu ushahidi anao basi aumwage Mahakamani tunategemea kesi itaisha mapema sana.
 
Mhesh. Msigwa usiogope nipe maendeleo ya kesi inavyokwenda mimi niko tayari kuja kutoa ushahidi live! tumemsitiri sana huyo haramia, inauma sana.
 
WanaJF!

Katibu mkuu wa CCM, bwana Kinana, amefanya kweli kwa kuitimiza dhamira yake ya kumpeleka mchungaji Msigwa mahakamani endapo mchungaji huyo atakaidi fursa ya kumuomba radhi bwana Kinana.

Bwana Kinana alitoa fursa hiyo ya kuombwa radhi kufuatia kuchafuliwa taswira yake kwenye jamii, baada ya kudaiwa kuwa yeye ana jihusisha na masuala ya ujangili, jambo ambalo amelikanusha vikali.

Mchungaji Msigwa ameonekana mahakamani siku ya tar 14 akiwa na mawakili Tundu Lissu na Bwana Kibatala kama watetezi wa upande wa mshtakiwa.

My take,

Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana kesi hii ya kumshtaki mchungaji Msigwa kwa tabia yake ya kuropoka ovyo ovyo. Shukrani bwana kinana kwa hatua uliyo chukua. Sasa kazi kwa Msigwa kuthibitisha tuhuma zake za ujangili kwa bwana Kinana.
 
Kwa hiyo Tundu Lissu na Msigwa wakionekama mahakamani tayati wameshashitakiwa??? Mbona sijaona gazeti lolote?
 
Kwisha habari yake hiyo fidia atakayolipia chadema. watamkopesha kweli ?kutoka kwny ruzuku Kama
 
Kwa hiyo Tundu Lissu na Msigwa wakionekama mahakamani tayati wameshashitakiwa??? Mbona sijaona gazeti lolote?

Kweli mkuu,

Hakuna gazeti lolote lililotoa hii taarifa, ila ukweli ni kwamba Kinana amefungua mashtaka dhidi ya Msigwa rasmi. Habari zaidi nitaendelea kuweka, na kama kuna mtu anaweza kuzileta pia itakuwa ni jambo jemba kwa maslahi ya wanaJF wote.
 
Kwisha habari yake hiyo fidia atakayolipia chadema. watamkopesha kweli ?kutoka kwny ruzuku Kama

Mkuu,

Kwa wanasheria wataelewa hapa, kuna hii ishu inaitwa defarmation, nadhani ndio litakuwa shitaka namba moja kwa mchungaji Msigwa, na utakumbuka kutokana na kashfa hiyo kuwa Kinana ni jangili, ili sababisha Kinana avunje makubaliana na partners wake na ili m-cost si chini ya milioni 300 pesa za Tanzania. Sasa unaweza kupata picha ya hiyo fidia atakayolipa Msigwa kwa Kinana.
 
Back
Top Bottom