Kinana amburuza Msigwa kortini

Kinana amburuza Msigwa kortini

Ungewashauri na wale waliotajwa na Dr.Slaa, (ile list of shame),pale Temeke-Mwembeyanga nao waende mahakamani,maana kama wamesahau vile.

Hawajasahau ila wamempuuza, maana ukiongelea list of shame bila ya Dr Slaa kuwa ndani ya list basi hiyo inakuwa sio list of shame tena, maana ni nani asiyejua vitendo vya wizi alivyofanya Dr Slaa ndani ya CHADEMA (kuanzia ule wizi wa milioni 140 mpaka ule udanganyifu wa kwenda Israel na Ujerumani na mchumba wake kwa kutumia pesa za chama).
 
ndio akili yako imeishia hapo? Poor you and your master

Nyie jipeni moyo tu nahao mabwana zenu muone mnavyoaibika watu wako makini sana na hilo unafikiri watz wa leo niwale mliowazoea? tujipe mda mtakuja kuyaona
 
Kwani thread yangu ni hukumu?

Taarifa ni kwamba Msigwa amefunguliwa mashtaka na bwana Kinana juu ya tuhuma zake kuwa Kinana ni jangili. Sasa kinachotakiwa mahakamani ni ushahidi na sio porojo.

Kwahiyo kwa ufaham wako unataka kutuambia msigwa hawezi kuthibitisha na hana ushahidi?
 
Ungana na Msigwa ukathibitishe uhusika wa kinana na kufa kwa Tembo wetu.

Kama hujui tu; kwa sasa Msigwa ameiweka CHADEMA kikaangoni kwa maana huo upuuzi alikuwa akiuropoka kwa niaba ya chama chake, hivyo CHADEMA italazimika kuitoa hiyo faini endapo Kinana ataibuka kidedea kwenye hii kesi. Na ikumbukwe, lengo hapa ni kuwaonya na kuwafunza wanasiasa hasa waupinzania kuwa kuropoka kuna gharama yake.

Ndio utakapo jua kwamba "MSHIKWA NA NGOZI NDIO MUIBA NG'OMBE". Ngoja ukashuhudie Kagesheki akimliza Kinana mahakamani. Au hujajua kwamba mzungu wa TALL kesha mwaga mboga kule POLICCM?
 
Na mimi sijasema ni hukumu lakini kama mtu makini bila shaka unategemewa kuwa na taarifa zenye kiwango cha kuaminika lakini ukianza kusema "sidhani" kama vile unatoa maoni wakati thread umeleta mwenyewe then credibility inapotea ndg yangu. Jifunze writing skills utafaidika tu sio kulalamika.

Kwani thread yangu ni hukumu?

Taarifa ni kwamba Msigwa amefunguliwa mashtaka na bwana Kinana juu ya tuhuma zake kuwa Kinana ni jangili. Sasa kinachotakiwa mahakamani ni ushahidi na sio porojo.
 
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.

Hicho chama chako kwani kimeanza kuchafuka leo? Chama chako ni kichafu toka enzi za nabii NUHU; angalia uchafu wenu jinsi mlivyoliibia Taifa fedha za BOT kupitia ile kashfa ya EPA mpaka mkamuingiza huyo DHAIFU ikulu!!! Nyie ni wachafu na mnanuka na hamsafishiki!!!
 
du hi kitu imetokea j.4 umeleta leo, kama ni kweli basi ccm inakwenda pata pigo lingine. na kama hi habari ikiwa ya uongo tegemea ban la maana kama yule mwenzako aliyeleta habari za uongo arusha.
 
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.

Unachekesha sana, nani kakwambia chama chako ni kisafi? Mbona ni kichafu siku zote? kichafuke vipi tena ilhali ni cheusi tiiiii kwa uchafu
 
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.

Hamy -D

Kwanini unamwita Msigwa mropokaji kabla hata ya kesi kutolewa hukumu?? unakumbuka bungeni alimwambia Dr Nchimbi kuwa badala ya kumwita mpotoshaji wamwombe ushahidi, lakini Nchimbi hajafanya hivyo???

Yaani mtu anayetetea rasilimali zetu (tembo wetu) wewe unamwita mropokaji?? au kwa kua kamhusisha Kinana?? Mimi binafsi nimefurahi kama Kinana kaenda mahakamani kwasababu ni nafasi ya pekee kwa Msigwa kudhihirishia Watz mbele ya mahakama tuhuma zake dhidi ya Kinana.

Tanzania miaka 80 tulikuwa na tembo wengi sana sasa hivi wanakadiriwa kuwa pungufu ya 70,000 kwa sababu ya ujangili, nchi imegeuka shamba la bibi kila mtu anakuja kuchota tu, kwanini Msigwa asipige kelele???. Mara mzungu wa TALL kamamatwa na meno, mara Mvietnam kakamatwa na meno mara polisi, mara mwanajeshi mara fulani na fulani wewe bado huthamini kelele za watu kama akina Mch Msigwa??

Kumbe Tanzania imekosa wenyewe ndio mana wageni wanachuku chao, yaani hata kwenye rasilimali wewe bado unaleta uchama???? AIBU SANA
 
Hawajasahau ila wamempuuza, maana ukiongelea list of shame bila ya Dr Slaa kuwa ndani ya list basi hiyo inakuwa sio list of shame tena, maana ni nani asiyejua vitendo vya wizi alivyofanya Dr Slaa ndani ya CHADEMA (kuanzia ule wizi wa milioni 140 mpaka ule udanganyifu wa kwenda Israel na Ujerumani na mchumba wake kwa kutumia pesa za chama).

Inafahamika Dr W. P Slaa ni safi na makini.

Kama unaushahid kinyume chake peleka mahakamani sio kututapikia matapishi ya maneno na mipasho isiyo na vielelezo wala uShuhuda
 
mkuu,

kwa wanasheria wataelewa hapa, kuna hii ishu inaitwa defarmation, nadhani ndio litakuwa shitaka namba moja kwa mchungaji msigwa, na utakumbuka kutokana na kashfa hiyo kuwa kinana ni jangili, ili sababisha kinana avunje makubaliana na partners wake na ili m-cost si chini ya milioni 300 pesa za tanzania. Sasa unaweza kupata picha ya hiyo fidia atakayolipa msigwa kwa kinana.
kwahiyo ameshapandishwa mahakamani na hukumu imeshatolewa kuwa amlipe fidia? Kama bado mbona kamaunajua hakimu atahukumu nini, acha sheria ifanye kazi, umesahau kesi ya zombi?
 
Acha uongo,ninyi magamba mnavyomtafuta Dr.Slaa,mngekuwa na ushahidi wa wizi,wa hizo 140M faster mngeshampeleka mahakamani kupitia yule DPP wenu kilaza..Pia wale waliotajwa kwenye list of shame,wanachoogopa ni kuumbuka zaidi na si kwamba wamempuuza,,CCM hakuna msafi,..mara UDA,Rada,EPA,Kagoda,Richmond,Deep green,....
 
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.
Mkuu mbona umeshatoa hukumu kabla ya Mahakama haijatoa hukumu?umejuaje kama yaliyosemwa hayana ukweli?Au umeamua kujipunguza ufahamu?
 
Msigwa tabia ya kuropoka hajaanza leo ni kitambo tabia hii amekuwa nayo.
 
Mkuu, sidhani kama Kinana angukuwa na ujasiri wa kwenda mahakamani na kufungua mashtaka kwa Msigwa kama kweli angekuwa jangili au kujihusisha na vitendo hivyo kwa nama yoyote ile.
Huku ni kujadili upuuzi,badala uje na habari za uhakika kwamba Msigwa amefungiliwa kesi nambari kadhaa,yenye kumtaka afanye kadhaa, wewe unakuja na urojo eti Ulimwona Msigwa na Tundu mahakamani sii ujinga huu.
Anyway, usiwatoe kwenye mada za msingi watu. Kama zile za kusambaratika CCM Kagera, Aibu ya aina yake kwa Chama na yule jamaa yako kule Iramba jana, kuendelea kufichuka kwa uhusiano wa vigogo na biashara ya madawa/nyara za serikali.
Pia usisahau swali wanalojiuliza wengi,mbona biashara ya madawa na pembe imepamba moto sana kwa kipindi hiki baada ya Katibu Mkuu Mukama kuondolewa na tukielekea uchaguzi wa 2014/15? Jee hii biashara ini mbinu mpya ya kupata pesa za kuendesha kampeni baada ya zile mbinu za EPA kushtukiwa na Upinzani hasa CDM na kukomaa?
Mwisho wanajiuliza, kumrudisha mzee wa mikakati AK ulingoni licha ya yeye kutangaza kustaafu ni kwa vile yeye hizi biashara yeye ni Gwiji kama anavyotuhumiwa na WENGI(sio Msigwa pekee)?
 
WanaJF!

Katibu mkuu wa CCM, bwana Kinana, amefanya kweli kwa kuitimiza dhamira yake ya kumpeleka mchungaji Msigwa mahakamani endapo mchungaji huyo atakaidi fursa ya kumuomba radhi bwana Kinana.

Bwana Kinana alitoa fursa hiyo ya kuombwa radhi kufuatia kuchafuliwa taswira yake kwenye jamii, baada ya kudaiwa kuwa yeye ana jihusisha na masuala ya ujangili, jambo ambalo amelikanusha vikali.

Mchungaji Msigwa ameonekana mahakamani siku ya tar 14 akiwa na mawakili Tundu Lissu na Bwana Kibatala kama watetezi wa upande wa mshtakiwa.

My take,

Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana kesi hii ya kumshtaki mchungaji Msigwa kwa tabia yake ya kuropoka ovyo ovyo. Shukrani bwana kinana kwa hatua uliyo chukua. Sasa kazi kwa Msigwa kuthibitisha tuhuma zake za ujangili kwa bwana Kinana.

Una mshukuru Kinana kwa lipi sasa?hv mkuu hauna taaluma yoyote inayoweza kuku keep busy na kufanya fikra zako ziwe active?
 
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.
Tatizo mnasahau kuwa hukohuko mahakamani ndiko watu wanakoshinda na kushindwa kesi. Msijifanye mmesahau ya ugaidi...
 
Kwani thread yangu ni hukumu?

Taarifa ni kwamba Msigwa amefunguliwa mashtaka na bwana Kinana juu ya tuhuma zake kuwa Kinana ni jangili. Sasa kinachotakiwa mahakamani ni ushahidi na sio porojo.
Katika thread yako umeshasema bila shaka kuwa huyu Mchungaji ni mropokaji,ukimaanisha kuwa aliyoyasema hayana usahihi hata kidogo,mkuu wewe huwezi kuujua ukweli mbaka hapo mahakama itakapotoa hukumu!Hata kama ni mke wa Bwana kinana kamwe huwezi kujua huu ukweli,ni vema kusubiri hukumu ya mahakama!
 
Msigwa tabia ya kuropoka hajaanza leo ni kitambo tabia hii amekuwa nayo.

Naomba sana mahakama itende haki na ikiwezekana hukumu iharakishwe, kwa maana Tanzania nzima inapaswa ielewe kuwa ndani ya CHADEMA hakuna wanasiasa bali kuna wazushi, magaidi na watekaji wa raia, haya yote wanayafanya wao na kisha wanaisingizia serikali kuwa ndio imefanya. Hii ina ingia akilini?
 
Back
Top Bottom