Kinana amburuza Msigwa kortini

Kinana amburuza Msigwa kortini



Pia Mahakama itoe zuio la kudumu kumzuia Msigwa, au wakala wake kutoa au kuchapisha taarifa zozote za kashfa dhidi yake. Katika hati ya madai amenukuu baadhi ya kauli za Msigwa, ikiwemo "Kinana (naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi."


HabariLeo


Woga wa nini?
 
Sijui wanasheria wa kinana wamemshauri vizuri... hakuna contradiction kati ya Bunge, Mahakama na Serikali. Kauli za bungeni zinashughulikiwa na kanuni za bunge siyo mahakamani au serikalini.

Mzee kinana, mimi ningekuwa wewe, kwa kweli nisingekubali wadhifa huo ulioupokea. kama kula umekula ya kutosha nasasa ungebaki na heshma yako unayosema umeijenga kwa miaka mingi. Hii damu ya Vijana iko kasi sana na nyakati zenu za Babu yetu Mzee Ml. Nyerere, THUBUTU HII YA VIJANA KWENDA KASI HAIKUWEPO. HUNA NGUVU TENA YA KUPAMBANA NA DAMU HII. Ungewaachia vijana akina Nape, Mwiguru na wezao.... Jiuzuru mzee.. Aibu si kitu chema kabisa..

Napita tu jamani..
Wamemshauri vizuri sana! Wanasheria wataila vipi hela ya kinana kama sio kwa kumuingiza humo?
 
Kinana hata ukifungua kesi 1000000000000000000000000 wewe ni jangili wala huna namna ya kujiokoa kisiasa na ccm wakitaka angalau kuongoza kambi ya upinzani kuanzia 2016 hawana budi kukuweka pembeni. Wewe ni nani asiyekujua kuwa makapi? Ulikuwa ukimtafutia kura mshua 2010 lakini matokeo yake wewe uliona kama sio kufanya approximates na kuchakachua kura kwa njia ya mtandao mlikuwa mmekwenda na maji maana tulishawagundua mlikuwa na mashine wakati walipokuwa wakituma matokeo kwa njia ya mtandao kutoka mawilayani mashine zenu mlizowapa tume ya ccm ya uchaguzi zilikuwa zinaconvert matokeo, you are impotent people hamstahili kuwepo katika taifa hili tukufu la jamhuri ya muungano wa tanzania. Mnatujambia kwa shibe zitokanazo na raslimali za taifa letu ila mkumbuke jasho la mtu haliliwi ipo siku mtaingia kwenye 18 zetu mtaipata.
 
Afadhali tembo watulie, Kinana hutaki kuona tembo jamani walikufanya nini haswa
 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba radhi.

Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Aidha alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014. Katika hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma hizo ameharibiwa tabia yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na kumfanya achukiwe na kudharauliwa katika jamii.

Anadai jina lake na heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu, vimeharibiwa na Msigwa kwa nia mbaya, pia kwa tuhuma hizo anazosisitiza kuwa ni za uwongo, licha ya kumsababishia maumivu ya kisaikolojia, pia zimemsababishia hasara ya fedha.

Anadai kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha mboga na mwekezaji kutoka kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha kampuni hiyo kuvunja majadiliano hayo.

Kinana anadai kuwa sababu iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo ni kutajwa kwake na mbunge huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na biashara hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Mradi huo ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni nne, Hisa za ushiriki wa Kinana zilikuwa ni asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano hivyo anatathmini kuwa amepata hasara ya Sh milioni 350.

Kinana anaiomba Mahakama hiyo imwamuru Msigwa amlipe fidia ya Sh milioni 350 kama hasara rasmi, pamoja na fidia ya maudhi na fidia ya hasara ikiwemo gharama za kesi.

Aidha anaiomba Mahakama imwamuru amlipe riba kwa kiwango kitakachopangwa na Mahakama, tangu tarehe ya hukumu hadi malipo ya mwisho, imwamuru kufuta tuhuma dhidi yake na kumuomba radhi kwa kuchapisha katika magazeti mawili ya Kingereza na mawili ya Kiswahili yanayosambazwa nchini.

Pia Mahakama itoe zuio la kudumu kumzuia Msigwa, au wakala wake kutoa au kuchapisha taarifa zozote za kashfa dhidi yake. Katika hati ya madai amenukuu baadhi ya kauli za Msigwa, ikiwemo "Kinana (naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi."

"Hata kwenye Nassaco, Shirika la Meli Tanzania kuna harufu ya ufisadi ndani yake; ajibu hoja...Kinana meli zake ndizo zinazohusika kubeba pembe za ndovu nchini. hajajibu hoja hizo! Kwa siku nchi hii tembo 67 wanauawa.


"Hao ndio wanaokifadhili Chama Cha Mapinduzi, halafu wanakuja eti kuwashawishi Watanzania muwasikilize na kwamba Chama Cha Mapinduzi eti ni kizuri."

"Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangili ni organized Crime. Ni mtandao wa Kimafia, uko duniani kote, unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea..."

HabariLeo



 
Hapa fedha za walala hoi zinazidi kutafunwa kwa kesi ambazo hazina kichwa wala miguu..
 
Hapo patamu. Makamanda mliosome sheria sasa ndo kazi ya ukombozi imeanza. Ikumbukwe Mh. Kagasheki majuzi tu alitoa kauli nzito kwamba baadhi ya watendaji wakubwa nao wanahusika na mambo haya. Tutafika tu.

Ebu tusubirie make haya ni makubwa sasa.
 
wanaowashauru viongozi wa CCM hawana akri zuri.

wapelekwe hospitali wakapimwe

kama amepeleka kesi mahakamani nampongeza kwa hilo,ili nayale ambayo hatuyajui juu ya huyu JANGIRI na HARAMIA LA KIMATAIFA watu wayajue.

hatuwezi kukaa kimya wakati

1. tembo wanaisha

2.watu wanabambikiwa kesi za ugaidi

3. watu wanang'olewa kucha na meno kwa koleo

4. watu wana mwagiwa tindikali na kitembezwa kwenye majukwaa ya kisiasa

5. maisha bora kwa kila mtanzania hatuyaoni

6. wafanya kazi wa idara zote wanakatwa BIMA ZA AFYA wakati dawa hakuna mahospitalini

shame on you KINANA, TENA UMEFANYA LA KHERI KWENDA MAHAKAMANI ILI GARAMA ZOTE ZA TEMBO ULIOWAUA UZIRUDISHE.

MWISHO ,HONGERA SANA PETER MSIGWA KWA KULIUMBUA HILI JANGILI LA CCM
 
Ameharibiwa tabia?!!!! Kwa hiyo sasa hivi ana tabia mbovu kutokana na Msigwa?!!!
Yap nw kinana Hana tabia njema,pia si mwaminifu Hana weledi coz ya msigwa ndo mana yake na pole yake ataisoma namba tunataka tembo wetu
 
Well done kinana,

Hizi sifa za "kitoto" za hawa wabunge wetu lazima ziwatokee puani.

Kinana ni mtu makini sana na kwa muda aliotafakari na wanasheria wake lazima MCHUNGAJI wa chadema atajuta.

View attachment 97630

Piga ua Kinana hapa lazima aaibike. Kesi imeshaisha kabla haijaanza. Alishakiri Meli iliyokuwa imebeba pembe za Ndovu ni ya kwake lakini mzigo sio wa kwake. "Anybody who participate in a murder is a murderer".
 
ya ndani ya bunge hamna kesi hapo ,labda hayo ya jukwaani huko mwanza.... ila hiyo ni nafasi nzuri kwa Msigwa kumzika huyo kinana na ujangili wake.
 
Ni jambo jema kwenda Mahakamani maana ni utawala wa Sheria. Kama Msigwa alilopoka itajulikana mahakamani na Kama Kinana ana kajitabia kabaya bila shaka itabainika. Lengo liwe ni kuheshimiana katika jamii, aidha wewe ni mlopokaji ujulikane na sheria ichukue mkondo wake au wewe ni mwizi wa Raslimari za nchi na tukujue katika hilo ili tukuadhibu.
 
Mbona kesi ni rahisi sana...kwani kinana ndio Abdullaman Kinana??
 
Back
Top Bottom