Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,779
1,304
Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ametaja siri ya chama hicho kupoteza majimbo mbalimbali ya uchaguzi likiwamo la Iringa Mjini kuwa ni makosa yaliyofanyika wakati wa uteuzi wa wagombea.

Alisema jambo jingine linalowapa kiburi wapinzani lilitokana na vitendo vya rushwa vilivyofanyika ndani ya chama hicho kwa upande mmoja na kwa watendaji serikalini kwa upande wa pili.

Kinana alisema chama hicho kimeshajisahihisha na kimejipanga kudhibiti vitendo hivyo ndani ya chama na pia kitadhibiti rushwa kwa viongozi na watendaji serikalini kwa kuwachukulia hatua watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu.

Alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mwembetogwa Iringa katika siku ya mwisho ya ziara ya siku tano mkoani hapa.

"Chadema wasidhani wana wanachama hapa, CCM tumejua sababu zilizotufanya tupoteze majimbo kadhaa likiwamo hili la hapa Iringa Mjini, mosi ni makosa yaliyofanyika wakati wa uteuzi wa wagombea, watu walitaka mabadiliko hawakuyapata ndani ya chama ndiyo sababu wakalazimika kupiga kura za hasira kwa kuchagua upinzani," alisema Kinana na kuongeza:

"Chadema wasipate kiburi kwa kudhani wana watu… watu wote waliosimama kule juu si wanaChadema ni wanaCCM wamekwenda huko baada ya sisi ndani ya chama hususan ngazi za juu kufanya makosa, tulifanya makosa katika suala zima la uteuzi wa wagombea.

"Kwa sasa niwahakikishie wananchi wote na wakazi wa Jimbo la Iringa kuwa tumejisahihisha, hatutarudia makosa … natoa wito kwa wakazi wa jimbo hili kutuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao ili tuweze kupata mbunge atakayewasaidia kutatua kero zinazowakabili wananchi."

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Frederick Mwakalebela alishinda kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini, lakini jina lake likakatwa katika vikao vya juu vya chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimtuhumu Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuwa alishirikiana na Chadema kutumia vibaya picha za tukio la mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten, Daud Mwangosi kwa kuziuza nje na kujipatia kipato.

Akijibu tuhuma hizo, Msigwa alisema:

"Kiukweli nimeumizwa sana na propaganda hii, nasema kweli imeniuma sababu hata familia ya marehemu Mwangosi tumeendelea kushirikiana nayo, wale ni jirani zangu na yule mtoto mdogo mara nyingi anakuja kushinda pale nyumbani kwangu," alisema Msigwa.


Alisema suala hilo pamoja na mambo mengine, chama chake kitayajibu kwenye mkutano wake wa Oktoba 18, mwaka huu utakaofanyika mjini hapa.

Chanzo: Mwananchi
 
Kupitia Taarifa ya habari ITV nimemuona na kumsikia Kinana katibu mkuu wa CCM akihutubia mkutano kule Iringa akisema kuwa CDM haikutakiwa kuwa na nguvu kama ilivyo sasa kilichosababisha hayo ni UPUUZI WETU yaani upuuzi wa CCM kwa kutotekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ndio maana baadhi yao wanakihama chama hicho na kuingia upinzani.
 
Kupitia Taarifa ya habari ITV nimemuona na kumsikia Kinana katibu mkuu wa CCM akihutubia nkutano kule Iringa akisema kuwa CDM haikutakiwa kuwa na nguvu kama ilivyo sasa kilichosababisha hayo ni UPUUZI WETU yaani upuuzi wa CCM kwa kutotekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ndio maana baadhi yao wanakihama chama hicho na kuingia upinzani.
Kuna ukweli fulani hivi!
 
Ukweli mtupu... wengi wetu tulilishwa sumu ya kuipenda CCM ile iliyokuwa na itikadi ya ujamaa na kujitegemea toka tukiwa kinda... a moment walipogeuka walaghai tuliwadis kwa sanaa... kwa sasa CCM haina wapenzi tena bali wachumia tumbo ... nimewahi kumuuliza NAPE itikadi ya CCM kwa sasa ni ipi akaigia mitini bila aibu ...
 
amesema ukweli tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa JK na ujinga wa wabunge wa ccm ni wapuuzi na wataendelea kuwa wapuuzi kinana anapoteza muda wake kuzunguka nchi nzima kuilalamikia serikali ya ccm ambayo ni viziwi hawasikii ccm hawana hoja nakumbuka nape na kinana walikuwa wanazunguka mikoa wanalalamika mawaziri mizigo walioteuliwa na mzigo mwenzao ni aibu kumdhalilisha bosi wake ccm ni janga la taifa
 
Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.

Namsubiri mwanadiwani aje hapa jukwaani atufafanulie zaidi kauli hizo tata za kiutendaji chini ya chama tawala.
 
Kupitia Taarifa ya habari ITV nimemuona na kumsikia Kinana katibu mkuu wa CCM akihutubia mkutano kule Iringa akisema kuwa CDM haikutakiwa kuwa na nguvu kama ilivyo sasa kilichosababisha hayo ni UPUUZI WETU yaani upuuzi wa CCM kwa kutotekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ndio maana baadhi yao wanakihama chama hicho na kuingia upinzani.

Mbona humaliziii kaka,

Ameendelea zaidi akadai viongozi wengi wa CCM ni wala rushwa ndio maana CDM inapata umaarufu!!
 
Ukiona amefika kusema hivyo mjue kuwa kishachoka kukinadi chama ambacho hakiuziki tena kwa wananchi ,ccm inachapa ya Expire date ambayo imeshapita wakati wake.

Ushauri wa bure kwa Vyama vya upinzani muwaambie wananchi wanapochagua vyama basi waangalie EXPIRE date ,kwani Kinana anajaribu kuificha japo haifichiki ,akisaidiwa na Mh.Kikwete kwa kufungua roadcrossing ,nimestaajabu sana Raisi anakuja kufungua roadcrossing kwa kishindo ? Jambo ambalo lingeweza kufanywa na mkuu wa Manispaa au imezidi sana mkuu wa wilaya ,halafu sikiliza bei iliyotumika kujenga road crossing ,inakatisha tamaa.
 
'CCM wajanja sana. Wakati wengine wamelala usingizi, Kinana yupo busy akipiga kampeni kimtindo kwa kisingizo cha ''ziara za kukuza chama''. By April 2015, atakuwa ameshatembelea na kucover kote zote za nchi hii. Then, from nowhere, CCM wanaamua kumsimamisha kugombea uRais (kama njia bora kabisa ya kuvunja makundi ya akina 6, Membe & Lowassa).
 
Somo la mantiki ni nzuri sana.

Iko hivi.

1. Kana kinana anasema "...ccm niwa puuzi..." na kinana ni katibu wa ccm na ni mwana chama wa ccm maana yake ni kwamba kinana naye ni sawa na ccm kwa kuwa na yeye ni ccm na amesema ccm ni wapuuzi. Maana yake na yeye ni sehemu ya puuzi. Kwa hiyo na yeye ni.....

2. Kama ccm ni wabadhirifu na wana viongozi wabadhirifu kama anavyo sema kinana maana yake ni kwamba hata kinana naye ni mbadhirifu kwa kuwa naye ni kiongozi wa ccm na ameamua kuanika ubadhirifu wao.

Swali, je kinana ni sawa na namba 1 hapo juu na ni sawa na namba mbili baada ya namba moja?!

Kama sio mbadhirifu anaweza kusema yale meno ya tembo yaliyo kamatwa China yakiwa kwenye meli yake haikuwa sehemu ya ubadhirifu?!; Na zile mashine za kufulia zilizo takiwa kuwa za Mount Meru hospital ndio huo anao ita ubadhirifu wenyewe?!

Weka mbali na kinana
 
Habari hio hio,Tbc: Kinana awapongeza wabunge kwa kutimiza ahadi. Please startimes rudisheni Itv wateja wa madish tbc hatufaiiiiiiiii
 
somo la mantiki ni nzuri sana.

Iko hivi.

1. Kana kinana anasema "...ccm niwa puuzi..." na kinana ni katibu wa ccm na ni mwana chama wa ccm maana yake ni kwamba kinana naye ni sawa na ccm kwa kuwa na yeye ni ccm na amesema ccm ni wapuuzi. Maana yake na yeye ni sehemu ya puuzi. Kwa hiyo na yeye ni.....

2. Kama ccm ni wabadhirifu na wana viongozi wabadhirifu kama anavyo sema kinana maana yake ni kwamba hata kinana naye ni mbadhirifu kwa kuwa naye ni kiongozi wa ccm na ameamua kuanika ubadhirifu wao.

Swali, je kinana ni sawa na namba 1 hapo juu na ni sawa na namba mbili baada ya namba moja?!

Kama sio mbadhirifu anaweza kusema yale meno ya tembo yaliyo kamatwa china yakiwa kwenye meli yake haikuwa sehemu ya ubadhirifu?!; na zile mashine za kufulia zilizo takiwa kuwa za mount meru hospital ndio huo anao ita ubadhirifu wenyewe?!

weka mbali na kinana

teeeeembo!!!!!!!....

 
Back
Top Bottom