Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.

Wana CCM kwa muda mrefu tumekuwa tukisema hivo.
Hongera Kinana kwa kuliweka hadharani tatizo hilo ili lishugulikiwe.
Haisaidii kukaa kimya wakati tatizo ni dhahiri.
 
CCM ni wapuuzi kama Kinana na Nape. Hongera Kinana kwa kutufungua mimacho, tongotongo zilitujaa yakhee. Ukiona wenye nyumba wanatoka nje wamefunga pua zao weye waenda fanya nini mle. Si tayari ushasikia huo uvundo?
Tokeni humo mje huku. Hewa bado safiii, 2015 ni kiama chenu ccm. Kama mshaanza kujikaanga wenyewe kwa mafuta yenu nnani atabaki kuhesabu kura??
 
Ni kweli wapuuzi ndo mana chadema na wapinzani wengine wanapata umaarufu la cvyo hawana akili hizo uhai wao ni kuitukn ccm.
 
Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.
Hawa kwa sasa ni kama wajenzi wa mnara maarufu wa BABELI. Ni kiasi cha kusoma maandishi ukutani tu.
 
Bado tunasubiri miezi 6 ya Mangula aliyosema atasafisha wala rushwa na wale wa magamba heh heh ,kama kiongozi mkuu anasema kuongo tutarajie nini,hiyo miezi 6 sasa ishakuwa mwaka na ushee na hakuna lolote .
 
AKIONGEA LEO HUKO IRINGA KATIKA VIWANJA VYA MWEMBE TOGWA KATIKA ZIARA ZAKE, KINANA KATIBU MKUU WA SISIEMU AMESEMA " SISI CCM NI WAPUUZI NDIO MAANA CHADEMA WANAPATA UMAARUFU SASA KWA ZAIDI YA MIAKA 3, SISI TUMEKALIA RUSHWA, RUSHWAAA, KUJILIMBIKIZIA MALI, TUKIAHIDI HIVI TUNATENDA VILE, VIONGOZI WA SERIKALI HAWAJI KWA WANANCHI, WAMEJIFUNGIA OFISINI, HATUTAUI KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI, TUNA SIASA ZA MAKUNDI... BRA BRAAAA...."

Source; Itv news; 8 Pm 12 October 2014.

Cc; Pasco, Chabruma, Paul Makonda, Ritz, Simiyu Yetu, Laki si Pesa, Mwigulu Madelu, Nape Mwandosya, Wingu, Msalani, Juliana wa Madelu na Zitto.. Lumumba et al....
 
wana ccm kwa muda mrefu tumekuwa tukisema hivo.
Hongera kinana kwa kuliweka hadharani tatizo hilo ili lishugulikiwe.
Haisaidii kukaa kimya wakati tatizo ni dhahiri.

mkuu so unakubaliana na kinana kuwa sisiemu ni wapuuzi including u, wewe ni mpuuzi na lumumba yote mliko humu ni wapuuzi eti...n akinana mwenyewe pia ni mpuuzi ?? Siyo maneno yangu ni ya kinana wenu... Kuwa sisiemu ni wapuuzi, wafikishie buku 7 wenzako hapo lumumba kuwa nyinyi ni wapuuzi..... Na pia amekiri kuwa chadema ni maarufu, ila nyinyi wapuuzi mmekalilishwa na mzee wa gombe kuwa chadema itakua 2013 .... Sisiemu ni wa puuzi....by kinana...ova.
 
Wana CCM kwa muda mrefu tumekuwa tukisema hivo.
Hongera Kinana kwa kuliweka hadharani tatizo hilo ili lishugulikiwe.
Haisaidii kukaa kimya wakati tatizo ni dhahiri.

Nani wa kulishughulikia mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
ni kweli wapuuzi ndo mana chadema na wapinzani wengine wanapata umaarufu la cvyo hawana akili hizo uhai wao ni kuitukn ccm.

kama uko sisiemu wewe ni mpuuzi kama kinana alivyo mpuuzi, na chadema ni maarufu. Ova.
 
amesoma wakati bila kujijuwa

mkuu ukweli utabaki ukweli, sisiemu ni wapuuzi, including kinana, jk, mangula, nape , na misukule yao yoote ya humu, ni mipuuzi, na inanuka rushwa, na inapswa kukiri kuwa chadema ni maarufu...ova.
 
mmmmmmmmmmm
ama kweli siasa mchezo mchafu

UNAKISIKITIKIA CHAMA CHA WAPUUZI, NA WALA RUSHWA?? POLE SANA, SIAMINI KAMA NAWE NI MMOJA WAO.

CCM ni wapuuzi kama kinana mwenyewe alivyo mpuuzi, CCM ina nuka Rushwa na chadema ni maarufu-By Kinana. Ova.
 
Si rushwa tu pekee yake bali ufisadi wa kutisha, uhuni, kuongoza nchi kwa mabavu kupitia mgongo wa jeshi, polisiccm, FFU na mahakama, uchakachuaji wa chaguzi mbali mbali na katiba mpya, maamuzi mbali mbali ambayo hayajali maslahi ya Tanzania na Watanzania kwa mfano misamaha ya kodi, mikataba ya madini, wizi wa kura kwenye Bunge la posho n.k.

Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.
 
sasa yeye anafanya nini na wapuuuzi kama naye sio mpuuuzi na mla rushwa
 
TAFAKURI CHOKONOZI: CCM NIWA PUUZI.

Jana katibu mkuu wa ccm (Mh Abrahaman Kinana, ambaye Mh Peter Msigwa anamuita "...Weka mbali na tembo..) akiwa anahitimisha ziara yake kwenye uwanja wa Mwembe togwa mjini Iringa; alitumia maneno ambayo mtu makini hawezi kuyapuuza.

Alisema yafuatayo.

1. "...Ccm niwa puuzi na tumefika hapa kutokana na upuuzi wetu..."

2. "...Chama chetu kina viongozi wabadhirifu na wezi, tumekalia rushwa..."

3. "...Viongozi hawatatui kero za wananchi, wao wanajiona wakubwa wanajifungia ofisini tu..."

4. "...Tuna siasa za makundi,..haya ndio yamewapa CHADEMA umaarufu Kutokana na upuuzi wetu..."

MANTIKI YA KAULI HIZO.

Kama CCM niwa puuzi, na Kinana ni kiongozi wa ccm maana yake na yeye ni sehemu ya kile anacho kisema (mpuuzi), kwa maana hiyo mwana ccm anayeshabikia chama chenye viongozi wapuuzi kama alivyosema katibu wao mkuu na yeye atakuwa mpuuzi (hapa unaweza kufikiria kidogo kuhusu mchakato wa katiba namna ulivyokwenda).

2. Kwa kuwa Kinana ni mtendaji mkuu na kwa maana hiyo anajua yaliyopo ndani kuliko sisi, ni sawa na kutangaza kuwa ndani kuna uvundo, kuna nuka, na kuna uozo wa rushwa na ubadhirifu (fikiria kidogo ya Epa, Escrow akaunti, na hata yeye mwenyewe meli yake kukamatwa na meno ya Tembo huko China).

3. Kama Kinana anakiri kuwa viongozi hawatatui kero za wananchi maana yake ni kwamba wako kinyume na 'peoples power', wao ndio wanaongoza serikali, na kwa mujibu wa katiba ya sasa ibara ya 8 inasema "...Mamlaka na madaraka ya serikali yako mikononi mwa wananchi na serikali itapata mamlaka na madaraka yake kutoka kwa wananchi..".

Kauli za Kinana zina mwangwi wa kuwa amsha wananchi wasio elewa kutoka kwenye lindi la usingizi mzito. Kauli hizo zingetoka kwa kiongozi wa upinzani zingekuwa na fafsiri nyingine. Lakini kwa kuwa zimetoka kwenye kinywa cha mtendaji mkuu wa chama, pamoja na upuuzi wake si kauli za kupuuza.

Jamaa amekiri na kuthibitisha kauli ya John Mnyika aliyo wahi kuitoa bungeni kuwa nchi yetu imefika hapa kutokana na udhaifu wa Kikwete na upuuzi wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Weka mbali na chama cha wapuuzi.
 
Mkuu Sasa subiri wapuuzi kutoka chama cha wapuuzi I mean wapuuzi fc a.k.a team Lumumba watakavyokuja na upuuzi wao hapa ndio wanabadilishana shift saa hizi.
 
Back
Top Bottom