Tarehe 12/10/2014 katibu mkuu wa ccm (Mh Abrahaman Kinana, ambaye Mh Peter Msigwa anamuita "Weka mbali na tembo") akiwa anahitimisha ziara yake kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, alitumia maneno ambayo mtu makini hawezi kuyapuuza.
Alisema yafuatayo:
1. "...CCM ni wapuuzi na tumefika hapa kutokana na upuuzi wetu..."
2. "...Chama chetu kina viongozi wabadhirifu na wezi, tumekalia rushwa..."
3. "...Viongozi hawatatui kero za wananchi, wao wanajiona wakubwa wanajifungia ofisini tu..."
4. "...Tuna siasa za makundi,..haya ndio yamewapa CHADEMA umaarufu kutokana na upuuzi wetu..."
MANTIKI YA KAULI HIZO
1. Kama CCM niwa puuzi, na Kinana ni kiongozi wa ccm maana yake na yeye ni sehemu ya kile anachokisema (mpuuzi). Kwa maana hiyo mwanaCCM anayeshabikia chama chenye viongozi wapuuzi kama alivyosema katibu wao mkuu na yeye atakuwa mpuuzi (hapa unaweza kufikiria kidogo kuhusu mchakato wa katiba namna ulivyokwenda).
2. Kwa kuwa Kinana ni mtendaji mkuu na kwa maana hiyo anajua yaliyomo ndani kuliko sisi, ni sawa na kutangaza kuwa ndani kuna uvundo, kunanuka, na kuna uozo wa rushwa na ubadhirifu (fikiria kidogo ufisadi wa Epa, Escrow akaunti, na hata yeye mwenyewe meli yake kukamatwa na meno ya Tembo huko China).
3. Kama Kinana anakiri kuwa viongozi hawatatui kero za wananchi maana yake ni kwamba wako kinyume na 'Peoples' Power'. Wao ndio wanaongoza serikali, na kwa mujibu wa katiba ya sasa ibara ya 8 inasema "...Mamlaka na madaraka ya serikali yako mikononi mwa wananchi na serikali itapata mamlaka na madaraka yake kutoka kwa wananchi..".
Kauli za Kinana zina mwangwi wa kuwaamsha wananchi wasioelewa kutoka kwenye lindi la usingizi mzito. Kauli hizo zingetoka kwa kiongozi wa upinzani zingekuwa na fafsiri nyingine. Lakini kwa kuwa zimetoka kwenye kinywa cha mtendaji mkuu wa chama, pamoja na upuuzi wake si kauli za kupuuza.
Jamaa amekiri na kuthibitisha kauli ya John Mnyika aliyowahi kuitoa bungeni kuwa nchi yetu imefika hapa kutokana na udhaifu wa Kikwete na upuuzi wa viongozi wa CCM na serikali yake.
Weka mbali na chama cha wapuuzi!
:israel:
View attachment 194784 View attachment 194785 View attachment 194786