Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Kinana toka jamaa wa CEO ROUNDTABLE Wamuambie akigombe urais watamsupport amekuwa kama kichaa
 
Sisi wenyewe, wana CCM.
Nawe unakaribishwa!!!

Kinana mwenyewe ndo anayemaliza Tembo wetu, ile ndege ya Qatar ya jeshi ilifikaje na kuchukua wanayama wetu mkuu? Mbona hatujasikia wanawajibishwa waliohusika? Ni hii hii CCM iliyojaa rushwa au unaizungumzia ipi?
 
ITV kuandika hivyo haishangazi....lakini Kinana alikuwa anatoa tathmini ya wananchi....kadri alivyowatembelea na kupata maoni yao na amewahakikishia wananchi kuwa tutajirekebisha ...wewe utabaki na labda tuuuu..sisi tunajitathmini tunajirekebisha tunasonga mbele
Leo katika taarifa ya habari ITV kwa mara ya Kwanza nimemsikia katibu mkuu wa CCM akikiri hadharani kwamba serikali inayoongozwa na chama chake inanuka rushwa ndio maana watu wanapenda CHADEMA.


Chanzo:
Mwananchi
 
ITV kuandika hivyo haishangazi....lakini Kinana alikuwa anatoa tathmini ya wananchi....kadri alivyowatembelea na kupata maoni yao na amewahakikishia wananchi kuwa tutajirekebisha ...wewe utabaki na labda tuuuu..sisi tunajitathmini tunajirekebisha tunasonga mbele
ITV hawajaandika hivyo bali wamemuonesha akisema hivyo.
 
Unamfahmu mamba? Ni mdudu hatari sana akipata chakula kitamu anakula huku akitokwa na machozi hivyo unaweza kudhani analia ndo kinana hizo ni kejeli tu na kupima kama watanzania wameamka au la
 
Kupiga vita rushwa ukiwa CCM ni sawa na kupiga ngumi mkuki,na je anayesema hayo si ndo wale wale akina Chenge wapinzania wa Rasimu ya katiba ya Mzee wetu mpendwa Warioba?, ambayo ingepita ingewaadabisha na akaunti zao nje?
 
wanaandika habari na mkanda wa video wanaupeleka kwa mhariri...kwa hiyo kuandika..au kusema...yote ilimradi umepata ujumbe
Kumbe yale maneno hakuyatamka Kinana bali hawa wapuuzi wa ITV wameyafoji na kumuwekea mdomoni wakati wa kuhariri?
 
Tarehe 12/10/2014 katibu mkuu wa ccm (Mh Abrahaman Kinana, ambaye Mh Peter Msigwa anamuita “Weka mbali na tembo”) akiwa anahitimisha ziara yake kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, alitumia maneno ambayo mtu makini hawezi kuyapuuza.

Alisema yafuatayo:
1. "...CCM ni wapuuzi na tumefika hapa kutokana na upuuzi wetu..."
2. "...Chama chetu kina viongozi wabadhirifu na wezi, tumekalia rushwa..."
3. "...Viongozi hawatatui kero za wananchi, wao wanajiona wakubwa wanajifungia ofisini tu..."
4. "...Tuna siasa za makundi,..haya ndio yamewapa CHADEMA umaarufu kutokana na upuuzi wetu..."

MANTIKI YA KAULI HIZO
1. Kama CCM niwa puuzi, na Kinana ni kiongozi wa ccm maana yake na yeye ni sehemu ya kile anachokisema (mpuuzi). Kwa maana hiyo mwanaCCM anayeshabikia chama chenye viongozi wapuuzi kama alivyosema katibu wao mkuu na yeye atakuwa mpuuzi (hapa unaweza kufikiria kidogo kuhusu mchakato wa katiba namna ulivyokwenda).

2. Kwa kuwa Kinana ni mtendaji mkuu na kwa maana hiyo anajua yaliyomo ndani kuliko sisi, ni sawa na kutangaza kuwa ndani kuna uvundo, kunanuka, na kuna uozo wa rushwa na ubadhirifu (fikiria kidogo ufisadi wa Epa, Escrow akaunti, na hata yeye mwenyewe meli yake kukamatwa na meno ya Tembo huko China).

3. Kama Kinana anakiri kuwa viongozi hawatatui kero za wananchi maana yake ni kwamba wako kinyume na 'Peoples’ Power'. Wao ndio wanaongoza serikali, na kwa mujibu wa katiba ya sasa ibara ya 8 inasema "...Mamlaka na madaraka ya serikali yako mikononi mwa wananchi na serikali itapata mamlaka na madaraka yake kutoka kwa wananchi..".

Kauli za Kinana zina mwangwi wa kuwaamsha wananchi wasioelewa kutoka kwenye lindi la usingizi mzito. Kauli hizo zingetoka kwa kiongozi wa upinzani zingekuwa na fafsiri nyingine. Lakini kwa kuwa zimetoka kwenye kinywa cha mtendaji mkuu wa chama, pamoja na upuuzi wake si kauli za kupuuza.

Jamaa amekiri na kuthibitisha kauli ya John Mnyika aliyowahi kuitoa bungeni kuwa nchi yetu imefika hapa kutokana na udhaifu wa Kikwete na upuuzi wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Weka mbali na chama cha wapuuzi!

:israel:

magamba malaya.jpg magamba wakipigana1.jpg magamba wakipigana2.jpg
 
Huyu mpumbavu kasha rudia kazi yake ujangili jusi kaua tembo mmoja...
 
Huyu mpumbavu kasha rudia kazi yake ujangili jusi kaua tembo mmoja...

Kila siku kila saa kila sekunde anauwa tembo, huyo mmoja ni uliyesikia wewe. Njoo Ruaha uone tunavyowamaliza kimyakimya
 
Huyu mpumbavu kasha rudia kazi yake ujangili jusi kaua tembo mmoja...
Huwa napata shida napoona mkw wa mtu anatukana matusi kama haya huko ndani sijui mnaishi vipi na huyu mmewako,bawacha bana.
 
Back
Top Bottom