Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa

Iringa. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ametaja siri ya chama hicho kupoteza majimbo mbalimbali ya uchaguzi likiwamo la Iringa Mjini kuwa ni makosa yaliyofanyika wakati wa uteuzi wa wagombea.

Alisema jambo jingine linalowapa kiburi wapinzani lilitokana na vitendo vya rushwa vilivyofanyika ndani ya chama hicho kwa upande mmoja na kwa watendaji serikalini kwa upande wa pili.

Kinana alisema chama hicho kimeshajisahihisha na kimejipanga kudhibiti vitendo hivyo ndani ya chama na pia kitadhibiti rushwa kwa viongozi na watendaji serikalini kwa kuwachukulia hatua watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu.

Alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mwembetogwa Iringa katika siku ya mwisho ya ziara ya siku tano mkoani hapa.

"Chadema wasidhani wana wanachama hapa, CCM tumejua sababu zilizotufanya tupoteze majimbo kadhaa likiwamo hili la hapa Iringa Mjini, mosi ni makosa yaliyofanyika wakati wa uteuzi wa wagombea, watu walitaka mabadiliko hawakuyapata ndani ya chama ndiyo sababu wakalazimika kupiga kura za hasira kwa kuchagua upinzani," alisema Kinana na kuongeza:

"Chadema wasipate kiburi kwa kudhani wana watu… watu wote waliosimama kule juu si wanaChadema ni wanaCCM wamekwenda huko baada ya sisi ndani ya chama hususan ngazi za juu kufanya makosa, tulifanya makosa katika suala zima la uteuzi wa wagombea.

"Kwa sasa niwahakikishie wananchi wote na wakazi wa Jimbo la Iringa kuwa tumejisahihisha, hatutarudia makosa … natoa wito kwa wakazi wa jimbo hili kutuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao ili tuweze kupata mbunge atakayewasaidia kutatua kero zinazowakabili wananchi."

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Frederick Mwakalebela alishinda kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini, lakini jina lake likakatwa katika vikao vya juu vya chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimtuhumu Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuwa alishirikiana na Chadema kutumia vibaya picha za tukio la mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten, Daud Mwangosi kwa kuziuza nje na kujipatia kipato.

Akijibu tuhuma hizo, Msigwa alisema:

"Kiukweli nimeumizwa sana na propaganda hii, nasema kweli imeniuma sababu hata familia ya marehemu Mwangosi tumeendelea kushirikiana nayo, wale ni jirani zangu na yule mtoto mdogo mara nyingi anakuja kushinda pale nyumbani kwangu," alisema Msigwa.

Alisema suala hilo pamoja na mambo mengine, chama chake kitayajibu kwenye mkutano wake wa Oktoba 18, mwaka huu utakaofanyika mjini hapa.


Chanzo:
Mwananchi

 
KINANA NA NEPI ni rafiki yake MSALANI na FAIZA FOXY na RIZ1
 
Na mimi nilimsikia. Alisema vyama vyaupinzani kama Chadema vimepata umaarufu kwa sababu ya upuuzi wa CCM!!
 
Mbona haendi Arusha kuwaambia sababu ya kulipoteza jimbo hilo, walipingana na nani? Kweli huyu jamaa kaishiwa nyimbo hata chorus ameshairudiaimeisha ladha. Alisema rushwa ndio imefanya wananchi waichukie ccm? Na wanauhakika kama waliokuwa wafuasi wa Mwakalebela bado wanamhitaji? Maana ukikosa kitu ukapata mbadala wake maisha yakasonga ukija kukipa tena hutakuwa na uhitaji nacho. Pole KINANA hata Makamba aliongea mengi mengi sana mwisho aliambiwa kachoka apumzike bado kidogo utaambiwa pumzika.
 
Mimi si mfuasi wa chama chochote lkn huwa napenda sana kumsikiliza Mhe. Kinana, alisema hivi '' Umaarufu walioupata chadema miaka mitatu iliyopita si kwa akili zao na kutokana na upuuzi wetu (CCM)" hii inamaanisha kwamba kuna udhaifu mkubwa ndani ya chama cha CCM pamoja na Serikali yake, hongera sana ndugu Kinana kwa kuwa muwazi, lkn pia nimesikitishwa sana kwa kushindwa Kwako kuchukua hatua au karipio dhidi ya viongozi wasio waadilifu walio ktk Mamlaka yako.
 
mkuu so unakubaliana na kinana kuwa sisiemu ni wapuuzi including u, wewe ni mpuuzi na lumumba yote mliko humu ni wapuuzi eti...n akinana mwenyewe pia ni mpuuzi ?? Siyo maneno yangu ni ya kinana wenu... Kuwa sisiemu ni wapuuzi, wafikishie buku 7 wenzako hapo lumumba kuwa nyinyi ni wapuuzi..... Na pia amekiri kuwa chadema ni maarufu, ila nyinyi wapuuzi mmekalilishwa na mzee wa gombe kuwa chadema itakua 2013 .... Sisiemu ni wa puuzi....by kinana...ova.
You must be a kid!!
Siasa si matusi, na kama ulikuwa bado hujazaliwa, hata Mwalimu alianzisha Operation Tujisahihishe katika miaka ya mwishoni mwa '70s.
Siasa ya chama chochote lazima iende na wakati, na ndicho Kinana anachofanya.
Kama wewe ni msomi wa political science , utakumbuka kuwa cha msingi ni ku appease the toiling masses, maana ndo washika hatamu.
Hata Mao Tse Tung alisema miaka ya 70, "In case of political turmoil, you take one step back so the you take two steps forward".
Na hata wakati wa Cultural Revolution, Mao aliwaruhusu vijana ku "bombard the headquarters" ili heshima ya chama irudi.

Kinana is on the right track.
 
wote maintarahamwe ni mapuuzi kuanzia mwenye chama mpaka mshabiki WA chama. hii inakera sanaa

watanzania amkeni muwaadhibu hawa wapuuzi kwani wanaila nchi yetu bila jasho. natamani adhanu ianzie kwenye katiba
 
you must be a kid!!
Siasa si matusi, na kama ulikuwa bado hujazaliwa, hata mwalimu alianzisha operation tujisahihishe katika miaka ya mwishoni mwa '70s.
Siasa ya chama chochote lazima iende na wakati, na ndicho kinana anachofanya.
Kama wewe ni msomi wa political science , utakumbuka kuwa cha msingi ni ku appease the toiling masses, maana ndo washika hatamu.
Hata mao tse tung alisema miaka ya 70, "in case of political turmoil, you take one step back so the you take two steps forward".
Na hata wakati wa cultural revolution, mao aliwaruhusu vijana ku "bombard the headquarters" ili heshima ya chama irudi.

Kinana is on the right track.

pole sana; ccm ni wapuuzi. Ova.
 
sisi wenyewe, wana ccm.
Nawe unakaribishwa!!!

yaani wapuuzi mnaweza kusolve matatizo mliyoyasababisha ya rushwa, wizi, ujangili na uhuni kama wa komba na kapuya?? Poleni sana wapuuzi. Unamkaribisha jamaa naye awe mpuuzi.. Polesana mpuuzi.
 
"Kinana akiri CCM inachukiwa sababu ya rushwa".

1.Rushwa hiyo inafanywa ndani ya CCM au na wana-CCM au CCM yenyewe kama taasisi inajihusisha na rushwa?

2.CCM hapa kwa taarifa hii inamaanisha serikali na watendaji wake kuanzia utosini hadi unyayoni?

My take:

Rushwa haiwezi kuisha kwa kutamka tu majukwaani wakati watendaji wala rushwa wanawafahamu fika.
Si ajabu wengine ameongozana nao, wako katika huo msafara.

Ifikie wakati wa kutenda na si maneno tu. "He talks the talk,it is high time now to walk the talk".
 
Back
Top Bottom