Kinana: 2020 tungeona wabunge wengi wa upinzani wamechaguliwa, ila kulikuwepo changamoto

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
22 August 2023

View: https://m.youtube.com/watch?v=jOoXIZ27tUA

Abdulrahman Kinana anasema toka mfumo wa vyama vingi idadi ya wabunge na wawakilishi imekuwa ikipanda na hata uchaguzi wa 2020 idadi ingekuwa kubwa zaidi ya namba za wabunge kutoka vyama vya upinzani ila changamoto mbalimbali ikiwemo sheria.

Abdulrahman Kinana anaongeza kuwa kabla ya uchaguzi wa 2020 tayari upinzani walikuwa na viti jumla ya asilimia 40 na kama sheria zingekuwa nzuri basi 2020 na 2024 2025 idadi hiyo ya wabunge wa upinzani ingezidi hiyo 40%.

Awamu ya sita imekuja kurekebisha hayo mapungufu anaendelea kufafanua kigogo huyo wa chama tawala dola kongwe cha CCM ndugu Abdulrahman Kinana, na tayari miswada ya kisheria inaandaliwa.
 
Ohoooo, balozi Karume kule Zanzibar kajisahau kasena ukweli watu wakanuna. Makamu mwenyeki kuwa makini.
 
Kinana analalamika, Samia analalamika, wananchi tunalalamika, wapinzani wanalalamika matrafiki wanalalamika, Viongozi wa Dini wanalalamika.

Tumekwama tumekwama Mungu tusaidie.
 
Viongozi wakuu wajikite kwenye mjadala ulioko mezani, huu ni wakati wa DP W.
Asijifanye na yeye kawa Samia aliyetangaza kukaa kimya.
 
Waraka umesomwa mara moja tu raisi kaona mapungufu na kaahidi kurekebisha, leo Kinana anaahidi uchaguzi huru.
Kwa hiyo waraka ukisomwa mara sita tutarekebisha mengi.
 
22 August 2023

View: https://m.youtube.com/watch?v=jOoXIZ27tUA

Abdulrahman Kinana anasema toka mfumo wa vyama vingi idadi ya wabunge na wawakilishi imekuwa ikipanda na hata uchaguzi wa 2020 idadi ingekuwa kubwa zaidi ya namba za wabunge kutoka vyama vya upinzani ila changamoto mbalimbali ikiwemo sheria.

Abdulrahman Kinana anaongeza kuwa kabla ya uchaguzi wa 2020 tayari upinzani walikuwa na viti jumla ya asilimia 40 na kama sheria zingekuwa nzuri basi 2020 na 2024 2025 idadi hiyo ya wabunge wa upinzani ingezidi hiyo 40%.

Awamu ya sita imekuja kurekebisha hayo mapungufu anaendelea kufafanua kigogo huyo wa chama tawala dola kongwe cha CCM ndugu Abdulrahman Kinana, na tayari miswada ya kisheria inaandaliwa.

Mambo ya ajabu na usanii mkubwa. Badala ya kuonesha jinsi ccm itaweza kusimamia serikali yake iweze kukubalika na kuendelea kupata viti vingi anaelezea jinsi watarekebisha sheria ili wapinzani wapate viti vingi. Hivi tangu lini ccm kwa hiari waweke mazingira upinzani kushinda?
Binafsi naamini ccm imekua inashinda au kushindwa viti bungeni au urais kutokana na uongozi uliokwepo. Baada ya jk kama sio kumuweka jpm kugombea ccm ingeweza kushindwa. Na uchaguzi ujao hata bila kubadili sheria zozote wakimuweka samia kugombea wanaweza kupoteza nafasi ya urais na bunge kua na viti vingi ya vyama vya upinzani. Kinachohitajika ni haki na uwazi kwenye upigaji kura.
 
Badala ya kuonesha jinsi ccm itaweza kusimamia serikali yake iweze kukubalika na kuendelea kupata viti vingi anaelezea jinsi watarekebisha sheria ili wapinzani wapate viti vingi. Hivi tangu lini ccm kwa hiari waweke mazingira upinzani kushinda?

Wahafidhina mnatakiwa kumsikiliza Mzee wenu akionesha kukerwa na maovu mengi yaliyofanywa na CCM dhidi ya watanzania wengine kupitia siasa chafu .
 
Back
Top Bottom