Kinamama hoyee! Ewe mama, unataka kuwa Askofu? Ruksa!

Kinamama hoyee! Ewe mama, unataka kuwa Askofu? Ruksa!

Unapotafsiri maandiko unatakiwa kuangalia muktadha, na kujiuliza: nani anaambiwa na kwanini. Ingekuwa mwanamke haruhusiwi kufundisha, Paulo angemkataza pia Prisila(mwanamke) kufundisha. Lakini haikuwa hivyo, Paulo aliwaacha Prisila na Akila Efeso wafanye huduma. Katika Matendo 18 tunasoma kuwa Prisila na Akila walimfundisha Apolo kwa usahihi.
Prisila na Akila hawakumfundisha Apolo ila walimsahihisha, maandiko hayakatazi mwanamke kusahihisha mafundisho ya Kristo ila yanamkataza kulifundisha kanisa, juu ya mwanaume. Likewise wewe pia waweza kusahihisha kadiri ya ulivyofunuliwa na roho mtakatifu ila sio kufundisha au kuliongoza kanisa.

BTW kutoka sentensi yako ya kwanza ni vyema utambue kuwa anayetafrisi maandiko katika kweli sio wewe wala mwanadamu awaye yote, ila roho mtakatifu. Ukizitumia akili zako au busara za wanadamu utalisha sana watu matango pori na kuwapeleka chaka. Na hichi ndicho ufanyacho hapa.
 
Duh, wewe kweli ni Clever505
Kumbe unapenda kila point iwe na maandiko? Safi sana. Ila ujue kuna wengine hawapendi kuona vifungu vifungu kila wakati. Ndio sababu wakati mwingine naweka maelezo tu.

Haya, twende pamoja sasa kwa Maandiko
Katika Waefeso 4:11-13 tunasoma kwamba
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

Katika orodha hiyo umeona wadhifa wa Askofu? Hakuna! Katika Andiko lile la mwanzo kabisa, Askofu maana yake mwangalizi(Overseer). Kwa mantiki hiyo, Mtume ni huduma ya juu kuliko ya Askofu. Askofu ni kazi kama ya Administrator. Ndiyo sababu Paulo anaiita kazi njema.

Sasa kama unakubaliana na mimi kwamba Mtume yuko juu ya Askofu, angalia hapa jinsi Paulo anavyosema katika Warumi 16:7 (SRUV)
Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.

Katika maandiko ya awali kabisa ya Kigiriki, Yunia ni "Ἰουνίαν" (Iounian). Hili ni jina la kike maarufu kabisa Roma. Sasa Paulo anamtaja Yunia kuwa maarufu miongoni mwa mitume. This means, Yunia alikuwa Mtume mwanamke. Kwa mantiki hiyo kama Yunia alikuwa na cheo au huduma hiyo ya juu ya Utume, unashangaa nini nikikuambia kwamba mwanamke anaweza kuwa Askofu, just an Overseer?

Tatizo lililopo ni kwamba katika baadhi ya makanisa, vyeo vya huduma havifuati Biblia. Baadhi ya makanisa wamejitungia vyeo na majina yao wenyewe kama vile Kardinali, Padre, Askofu Mkuu nk. Waliojitungia vyeo ndio hao wanaoona Papa ni mkuu kuliko Askofu. Na wengine wanaona Askofu ni mkuu kuliko Mtume! Na wengine wanaofuata Maandiko wanaona Mtume ni mkuu kuliko Askofu.
Umenipata Clever505 ??

Point of correction; Androniko na Yunia hawakuwa mitume (hakuna andiko lolote linawatambulisha hivyo) ila walikuwa ni waamini na jamaa maarufu waioishi/ambatana na mitume.
 
Unapotafsiri maandiko unatakiwa kuangalia muktadha, na kujiuliza: nani anaambiwa na kwanini. Ingekuwa mwanamke haruhusiwi kufundisha, Paulo angemkataza pia Prisila(mwanamke) kufundisha. Lakini haikuwa hivyo, Paulo aliwaacha Prisila na Akila Efeso wafanye huduma. Katika Matendo 18 tunasoma kuwa Prisila na Akila walimfundisha Apolo kwa usahihi.
Unatoka nje ya mstari,

Mada unayojaribu kutetea umeitoa kichwani mwako.
 
Acha utani. Jifunze kuwaheshimu wanaostahili heshima
Naomba uniambie utani uko wapi hapa? Hivi kwanini watanzania si watu wanaopenda kufikiri kwa kina, utakuta mtu anakurupuka tu kujibu kitu wala hajuwi anajibu nini ili mradi tu kaongea au kuuliza swali. Ni wapi nimemtania Mh. Gwajima?
 
Back
Top Bottom