Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,634
- 4,381
Kinachotokea kwenye mikutano ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kimeonesha kuwa, wananchi wengi wanateseka sana kwa kukosa haki zao kutokana na watendaji wabovu wa nafasi tofauti tofauti. Nafikiri hata viongozi wa juu wanashangazwa na uozo uliopo huku chini
Ikimpendeza Muheshimiwa Waziri Mkuu atoe TAMKO kuwa, mikutano ya kusikiliza Kero za wananchi ikiongozwa na wakuu wa Mikoa au Wakuu wa Wilaya chini ya uangalizi wa wakuu wa Mikoa ifanyike nchi nzima kwa kila Wilaya kujitengea walau siku tatu kwa kila mwezi kupokea Kero za wananchi na kuzitatua au kuzitolea ufafanuzi au kuzifikisha kwenye mamlaka ya juu kwani hali sio shwari.
Watendaji watakao onekana kuwa mwiba kwa wananchi, wawajibishwe na mamlaka iliyo waajiri kwani ushahidi unakuwa waziwazi kutokea kwa wananchi waliokosa haki zao