Kinachonikera katika filamu za Jacob Stephen (JB)

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,756
Reaction score
2,646
Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.

Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.

Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB.

Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu?

Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu?

Nachoka kabisa
 
Attachments

  • 1407646008460.jpg
    1407646008460.jpg
    69.6 KB · Views: 1,819
Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninapoafiri. Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ioe ile mwisho ana bore sasa. Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB. Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu? Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu? Nachoka kabisa

Utayarishaji wa Bongo movies hauzingatii misingi ya cinematograpghy, imekaa kishikaji zaidi na kuendekeza mambo ya kienyeji enyeji. Wakati mwingine mambo ya bongo movies yanakwenda kimichepuo zaidi!!! Achana nao, angalia products zingine nyingi tu ziko sokoni na kwenye youtube.
 
Yaani nikae kabisa niangalie movie ya Bongo mwanzo mpaka mwisho?
 
Mimi kinachonikera ni kupenda kwake kukunja ndita muda wote.
 
Utayarishaji wa Bongo movies hauzingatii misingi ya cinematograpghy, imekaa kishikaji zaidi na kuendekeza mambo ya kienyeji enyeji. Wakati mwingine mambo ya bongo movies yanakwenda kimichepuo zaidi!!! Achana nao, angalia products zingine nyingi tu ziko sokoni na kwenye youtube.

Unaonekana una utaalam wa filam why usishiriki utoe msaada?
 
Filam nzuri Zipo shida ni kujua ni zipi sababu nyingi ni mbovu...
 
Tafuteni kolelo ya irene sanga..na filam za bond sinani
 
hahaha, eti mwisho wa movie lazima amuoe!? , napiga picha mwisho wa movie iwe anampiga chini
 
Utayarishaji wa Bongo movies hauzingatii misingi ya cinematograpghy, imekaa kishikaji zaidi na kuendekeza mambo ya kienyeji enyeji. Wakati mwingine mambo ya bongo movies yanakwenda kimichepuo zaidi!!! Achana nao, angalia products zingine nyingi tu ziko sokoni na kwenye youtube.
 
Wewe tuliaaaa JB ni next level...
Halafu taja movie 5 alizoact na huyu shamsa....
 
Mi sio mpenzi wa bongo muvi, mara chache nikiangalia wala sioni kipya. Toka The Great Kanumba afe, wasanii waliobaki amna ubunifu. Ni bora tu kutoa muvi.
 
Bongo movie hawana reality sababu ndani ya movie wanaigiza too boring ila kuna baadhi ziko poa
 
Kweli kabisa, bongo movie hawakai wakatulia wakaweka manjonjo ya movie halisi yaliyo next level,kuna matatizo mengi na kubwa ni elimu,elimu kubwa ya movie iko katika lugha ya kiingereza, na wengi ni vilaza au wavivu kujifunza, pili, aina ya wanaowaandalia filamu ni walewale hawana jipya,angalia bongo fleva ilivyo na ushindani, video mpaka mtu anaenda south africa, movies hawawashirikishi hata wakenya kama ojwang ili kuleta ladha,hebu fikiria ojwang na majuto wakikutana katika movie yako,hata kenya utauza, badala ya bedford,chukua binti makini kutoka rwanda au uganda na wavae vizuri, SCRIPT USIIANDIKIE CHOONI,ipitiwe na wataalamu kama jopo wajue wapi kinatakiwa nini kwa wakati gani, na mwisho PUNGUZENI KULIA MUDA MREFU KATIKA MOVIE ILI MUDA UENDE
 
Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.

Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.

Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB.

Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu?

Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu?

Nachoka kabisa

Hili zee tabia chafu kweli linachukua vitoto vyawatu na huyo shamsa anamchukua mwanamke wake,huwezi kushiriki kama hujatoa ----
 
Kweli kabisa, bongo movie hawakai wakatulia wakaweka manjonjo ya movie halisi yaliyo next level,kuna matatizo mengi na kubwa ni elimu,elimu kubwa ya movie iko katika lugha ya kiingereza, na wengi ni vilaza au wavivu kujifunza, pili, aina ya wanaowaandalia filamu ni walewale hawana jipya,angalia bongo fleva ilivyo na ushindani, video mpaka mtu anaenda south africa, movies hawawashirikishi hata wakenya kama ojwang ili kuleta ladha,hebu fikiria ojwang na majuto wakikutana katika movie yako,hata kenya utauza, badala ya bedford,chukua binti makini kutoka rwanda au uganda na wavae vizuri, SCRIPT USIIANDIKIE CHOONI,ipitiwe na wataalamu kama jopo wajue wapi kinatakiwa nini kwa wakati gani, na mwisho PUNGUZENI KULIA MUDA MREFU KATIKA MOVIE ILI MUDA UENDE

Ushauri wako mzuri, tatizo Bongo movie hawashauriki.
 
Ukiacha hilo kuna kimoja huwa nakiona kwenye maandishi ambayo huwa wanaandika kiingereza kutafasri maneno wanayoongea,huwa ni shida anaweza sema jingine na likaandikwa jingine kabisa mfano:

leaving inakuwa living.
Urgently-agently.
Heard-head.
Said-sayid.
Huwa najiuliza,huwa hawazifanyii uhakiki kazi zao hizi? Sababu sijawahi kuangalia movie ya kibongo ikakosa kosa kama hilo!
 
Back
Top Bottom