Kinachonikera katika filamu za Jacob Stephen (JB)

Kinachonikera katika filamu za Jacob Stephen (JB)

inaonekana humu kuna wapenzi wa filamu ila wadau wanatuangusha kama kuna mtu yuko inerested kuleta mageuzi anakaribishwa nimeshaandaa movie ya kufunga karne kwa bajeti ndogo tu njoo tuchangie tugawane faida
 
Swaga zao sasa
 
Attachments

  • 1407677697253.jpg
    1407677697253.jpg
    52.1 KB · Views: 335
Tatizo kwa system hii hii ya lipua lipua nitoe nyingine kesho bado wanapata vijisenti na sasa hawa Bongo movie wanashindana na Bongo fleva kufyatua single ......ili mradi wanauza vijisenti vinaingia hawataki kubadilika ......Hili soko litakuja kupata watu professional hawa walipuaji wataishia kupiga majungu tu.Itachukua muda mrefu sana kuvutia wadau serious kuwekeza au kufatilia filamu zao zinazofyatuliwa kama single za Bongo Fleva .......
 
mara nyingi maigizo yao yanakuwa ya kufirika zaidi kuliko uhalisia....
 
Mkuu umenena kabisa na hili swala ndilo lilinifanye nikate tamaa kumtambua JB kama mbadala wa kanumba kwenye tasnia na hili ni tatizo lake kubwa la kupenda kutumia charactor Mmoja kwenye movie zake nyingi!

Mwanzo niliamini kabisa JB angeleta mapinduzi lakini ndio kapooza kabisa hata kujaribu kufata nyayo za Kanumba hata kidogo hameshindwa yani huyo Ray ndio usiseme hata huwa sielewi anacho fanya kwenye tasnia!

Kanumba hakuwa Muigizaji mzuri sana lakini alikuwa ana wazidi kwenye uchaguzi wa charactor alikuwa ana tu suprise kwa kuleta charactor wapya!

Na kwa swala la Maudhui kuwa yale yale ni tatizo la bongo movie nzima na wanapaswa kubadilika!

Najua bongo movie wana chukia sana tunaposema tasnia hii imezikwa na kanumba Lakini huo ndio ukweli maana hamasa iliyo kuwepo kipindi cha uhai wa Kanumba hasa kwenye bongo movie haionekani kabisa!

Halafu Kuna kitu nimegundua kuwa uwepo wa Kanumba ulikuwa unamsaidia sana Ray na kumfanya awe mbunifu na hata hule ushindani wao ulikuwa unamsaidia sana! Naona siku hizi kapoa kabisa!

Bila shaka JB atajitosa kwenye siasa maana huku kumesha mshinda kabisa.
 
Wasambazaji ndio wameshika mpini, na wasambazaji wenye nguvu ndio hao wadosi, unategemea nini ukiwa vichwa sampuli ya kina JB, Ray, Cloud.....

Akili zimeshachezewa na wadosi kila wanachoambiwa..ndio mzee... tengeneza muvi kila mwezi....ndio mzee.....fanya part 1 na 2...ndio mzee (hapo gari itaendeshwa kutoka Mwenge mpaka posta)....msisikilize maoni ya mashabiki wenu jalini pesa ninayowalipa...ndio mzee...kuna siku atasema "sasa mimi iko hamu, omba panda veve"....ndio mzee.

Kama mnasubiri jipya kutoka Bongo muvi, mtasubiri sana wandugu.
 
Halafu hawa wasambazaji ndio wana washinikiza wawe wana rudia charactor hili wauze tuu!mfano

Ndio maana mwenzao Mtitu aliamua kusambaza mwenyewe!
 
inaonekana humu kuna wapenzi wa filamu ila wadau wanatuangusha kama kuna mtu yuko inerested kuleta mageuzi anakaribishwa nimeshaandaa movie ya kufunga karne kwa bajeti ndogo tu njoo tuchangie tugawane faida
Haya ya budget ndogo ndio yana zaa movie mbovu na ndio mwanzo wa kufanya kila kitu wewe mwenye!

Halafu wengi wanafanya movie za budget ndogo halafu wanataka matokeo makubwa.
 
labda wanakulana behind ze sene ndo anampa shavu huyohuyo
 
Yani hata hujiulizi mara mbili mbuili kuwa huyu mtu yupo kwenye maigizo.

189034_240119742782061_914030022_n.jpg
 
Maliza shule uje ukwamue bongo movie...

yani movie ni foolish kama jina lake... so foolish!

i am one among bongo movie actors, ila imenibidi nichepuke kwanza na elimu, huko sio mpango kwa sasa kabisa!
 
Kuna tofauti kati ya maigizo na filamu. Mfano; Sarafina ni filamu ila JB's job ni maigizo. So simple like that.
 
vaa miwani usione gere..huyo shamsa haolewi kikwelikweli wana act tu..acha wivu
 
vaa miwani usione gere..huyo shamsa haolewi kikwelikweli wana act tu..acha wivu
Sijakuelewa umejaribu kuchangia nini! Na huyo anaonewa wivu kwa sababu gani? Au kukosolewa ni kuonewa wivu?
 
Hadi mie unanificha shemeji yako?Kiukweli siamini macho yangu Excel

Hahahaa! usiogope! unaweza ukakuta unachat na JB mwenyewe ama ray K... sasa si kingenuka humu mamii?

em ngoja kwanza nivute upepo, mambo ya camera rolling, action, mara pause, sijui long shot na madudu mengine tuyaache kwanza hapa hapa nyuma ya pazia! lol..
 
Back
Top Bottom