Mkuu
kidamva Bongo movie wanatakiwa wawashukuru sana wamiliki wa mabus wanawapa shavu la nguvu sana mara nyingi sana ninaposafiri na mabus ndio napata fursa ya kuangalia movie za bongo ambazo kwa kiasi kikubwa zimepwaya sana na zimeegemea kuiga movie za kiNaigeria.
Kuna siku nilikuwa nasafiri na Lim Safari kutoka Dar - Arusha wakatuwekea movie ya Vicent Kigosi kilichonivutia katika movie yake ni makosa mengi ambayo hata mimi nisiyekuwa na ujuzi wa kutengeneza filamu niliuona dhahiri.Kwanza ni utumiaji wa mbaya wa sauti mtu anapaiza sauti mahali ambapo hapastahili,Vicent anakwenda kwa wakwe watarajiwa anafanya mambo ya uchizi uliopitiliza (hauna tafauti na ukichaa wa kuokota makopo barabarani) wahusika hawajapangiliwa vizuri umri na nk.Kifupi makosa yalikuwa mengi mno kiasi unashangaa hawa watengeneza filamu wamekaa kwenye fani kwa muda mrefu hakuna walichojifunza ?.Pili zoezi la kutengeneza filamu lazima lihusishe watu wengi lakini utakuta mhusika mkuu ndio mwongozaji,huyu huyu ndio mtungaji wa filamu kila kitu anaamua yeye nadhani hapo ndio makosa yanapojitokeza.Tatu wacheza filamu wa Tanzania wanapenda kuiga sana filamu za Nigeria ambazo wakati mwingine hazina utamaduni unaofanana na Tanzania.Nne wadau wengi wa filamu za Bongo hawana elimu ya fani husika na wakati mwingine hawana hata elimu ya kawaida mfano certificate,diploma au degree ya fani yoyote.