Habari za wakati huu ndugu watanzania
Kazi iendeleeiendelee
Baada ya nchi kumshinda Mwalimu mwaka 1985 aliamua kukaa pembeni na kumuachia kijiti Mwinyi ambae aliingia alikuta nchi imechakaa sana, uchumi upo hovyo, wananchi wanavaa nguo zenye viraka juu ya viraka, maduka ya ushirika yamekuwa shida, bidhaa muhimu hazipatikani, nchi haina fedha za kigeni n.k
Lakini licha ya yote hayo wananchi walimpenda sana Mwalimu kutokana na propaganda zake na hotuba zake za kulaumu mabeberu na wazungu na matajiri (ref. Kitabu cha Mengi) na hivyo kupanda mbegu kuwa shida zetu zimetokana na wazungu na matajiri.
Alipokuja Mwinyi akaanza kufungua nchi, kuruhusu watu kufanya biashara, kubinafsisha baadhi ya viwanda vilivyokuwa vinaenda kufa, akatoa uhuru wa siasa, akaanza kushirikiana na Marekani et al.
Wananchi wanyonge wote wakaanza kusema Mwinyi anatumika na mabeberu huku wengine wakisema ni dhaifu (hadi Nyerere aliandika hili) lakini deep down wote tunajua Mwinyi alikuwa sahihi na Nyerere alikuwa wrong na hii imepelekea hadi leo Mwinyi hapewi heshima anayostahili na mtaa kwa sababu watu bado walikumbuka propaganda za Nyerere wakati wa utawala wake na hivyo kushindwa kumuelewa.
Upande wa SSH naye anaishi chini ya propaganda za Magufuli na licha ya mazuri yote anatofanya eg kufungua nchi, kutoa uhuru kwa raia, kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji lakini bado anaishi kwenye kivuli cha SSH.
Licha ya mapungufu yake SSH anajitahidi kufanya kazi nzuri ila ndo hivyo jamii bado imemezwa na propaganda za Magufuli aliyefanya jamii ione bila yeye hakuna kitachofanyika.
Naunga mkono mada uliyowasilisha. Nampongeza Rais Samia kwa utashi na utayari wake kufungua nchi na kutafuta majibu ya umaskini na kuganga majereha, kama nilivyofanya wakati wa Mzee Ruksa, Feb. 1991.
Akina Nyerere na Magufuli ni genge la wahuni tena wenye roho mbaya/katili. In fact, hata kama Magufuli angekuwa hai leo asingeweza kutetea "legacy" yake uchwara. Angejaribu lakini angefeli viabaya tu kama Mwalimu alivyofeli kwa kuipambania yake kwa zaidi ya miaka 14; tena hayati Nyerere alikuwa na "nguvu" zaidi maana propaganda zake ziliwalevya Wadanganyika mbaya kabisa kwa takriban nusu karne!
Samia, kama Mzee Mwinyi, aliipokea nchi ikiwa hoi kiuchumi, closed kisiasa na kijamii ikiwa katika mpasauko mkubwa, Asipokata tamaa na iwapo atfanyia kazi mambo muhimu, basi Mh Samia anaweza kuacha "legacy" ambayo itasimama yenyewe bila kuhitaji chawa, kupe, mamluki, wanafiki nk kuitetea siku zijazo.
Pamoja na hayo, naomba nimkubushe Mh Rais kuwa, Wakati Ukuta. Yaani atambue kuwa muda hauko siku zote ukimsubiri, hivyo ni budi atatue mambo ya muhimu, na kwa wakati:-
1. Katiba Mpya - ndio uti wa mgongo wa leo na kesho ya Taifa letu. (akifeli hapa hawezi acha legacy kwa vyovyote)
2. Uchumi hasa wa micro-level ambao unamgusa mwananchi wa kawaida (mfumuko wa bei, kero za mzigo wa kodi na tozo nk)
3. Kupambana na ufisadi - kwani miradi, matumizi mabaya/makubwa na kutoa ajira kwa vijana vimefungwa pamoja ktk eneo hili. Akipatia Na. 1, basi yuko 50% ya kutatua hii Na. 3, kwani katiba ya sasa haitokaa itoe majibu.