Kinachomtesa Rais Samia ndicho kilimtesa Mzee Mwinyi

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,941
7,937
Habari za wakati huu ndugu watanzania
Kazi iendeleeiendelee

Baada ya nchi kumshinda Mwalimu mwaka 1985 aliamua kukaa pembeni na kumuachia kijiti Mwinyi ambae aliingia alikuta nchi imechakaa sana, uchumi upo hovyo, wananchi wanavaa nguo zenye viraka juu ya viraka, maduka ya ushirika yamekuwa shida, bidhaa muhimu hazipatikani, nchi haina fedha za kigeni n.k

Lakini licha ya yote hayo wananchi walimpenda sana Mwalimu kutokana na propaganda zake na hotuba zake za kulaumu mabeberu na wazungu na matajiri (ref. Kitabu cha Mengi) na hivyo kupanda mbegu kuwa shida zetu zimetokana na wazungu na matajiri.

Alipokuja Mwinyi akaanza kufungua nchi, kuruhusu watu kufanya biashara, kubinafsisha baadhi ya viwanda vilivyokuwa vinaenda kufa, akatoa uhuru wa siasa, akaanza kushirikiana na Marekani et al.

Wananchi wanyonge wote wakaanza kusema Mwinyi anatumika na mabeberu huku wengine wakisema ni dhaifu (hadi Nyerere aliandika hili) lakini deep down wote tunajua Mwinyi alikuwa sahihi na Nyerere alikuwa wrong na hii imepelekea hadi leo Mwinyi hapewi heshima anayostahili na mtaa kwa sababu watu bado walikumbuka propaganda za Nyerere wakati wa utawala wake na hivyo kushindwa kumuelewa.

Upande wa SSH naye anaishi chini ya propaganda za Magufuli na licha ya mazuri yote anatofanya eg kufungua nchi, kutoa uhuru kwa raia, kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji lakini bado anaishi kwenye kivuli cha SSH.

Licha ya mapungufu yake SSH anajitahidi kufanya kazi nzuri ila ndo hivyo jamii bado imemezwa na propaganda za Magufuli aliyefanya jamii ione bila yeye hakuna kitachofanyika.

Nahofia huko mbele kama akichoka SSH anaweza fuata nyayo za JPM ili tu naye akubalike kama mtangulizi wake kitu ambacho ni tatizo.

Thanks kwa kusoma na karibu kwa kuchangia

Nb. Nafikiria kuinunua JF mnaonaje wadau?
 
Dead wrong!

Muombe radhi Mzee Mwinyi kwa kumfananisha na huyo, Raisi Mwinyi aliifanyia mazuri sana Tanzania mimi ni mmojawapo wa wanufaika, nilipanda Mabasi ya Wanafunzi, wazo zuri na la kujali binadamu wanaoteseka hasa wa hali ya chini alianzisha Mzee Mwinyi.

Hivyo kamwe usimlinganishe na Mzee Mwinyi, raisi Samia ni sawa na raisi mstaafu Kikwete 100% kila kitu huyo ndio size yake, walinganishe hao, Mzee Mwinyi ni level nyingine kabisa!
 
Dead wrong!

Muombe radhi Mzee Mwinyi kwa kumfananisha na huyo, Raisi Mwinyi aliifanyia mazuri sana Tanzania mimi ni mmojawapo wa wanufaika, nilipanda Mabasi ya Wanafunzi wazo zuri na kujali binadamu wanaoteseka hasa wa hali ya chini alianzisha Mzee Mwinyi.

Hivyo kamwe usimlinganishe na Mzee Mwinyi, Samia ni sawa na Kikwete 100% kila kitu huyo ndio size yake, walinganishe hao Mwinyi ni level nyingine kabisa!

Mkuu unadhani kwanin Mwinyi haimbwi kama anavyoimbwa Mkapa na Nyerere?
 
Rubbish kabisa, kama angedhibiti mfumuko wa bei na kusikiliza shida za wananchi nani angemlaumu? mbuga zipo Tanzania wewe unaenda kuzindulia Royal tour Marekani how?

Mkuu mfumuko wa bei ni issue ya dunia nzima kuanzia kwa world factory China hadi huku kwetu Tanzania

Suala la mbuga kutangaziwa USA nadhani hatutakiwi kujadili kama tutakuwa serious na matumizi ya vichwa vyetu

Ahsante kwa kuchangia
 
Back
Top Bottom