MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Kiukweli si kawaida sana kwa sisi wanaume wa Pwani ambao tulipelekwa jando na kufunzwa na Mababu zetu kumkuta mtoto wa kiume anaongea sana kama Kasuku.
Nimesikitishwa na maneno ya hovyo na tuhuma zisizo tija zilizotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (MNEC) Haji Jumaa dhidi ya Katibu Mkuu wetu aliyepita Ndugu. Bashiru Ally na Mwenezi Mstaafu Polepole nimejiuliza nini kimekukuta MNEC au alishikwa pabaya. Moja ya mambo ya niliyojiuliza Haji Jumaa anamchukia Dkt. Bashiru kwa kosa gani au sababu aliamua kukirejesha chama kwenye misingi ya Nidhamu, Haki na weledi na kupambana na Mafisadi wa mali za chama.
Hata kama MNEC Haji Jumaa alikula Pesa kwenye kura za maoni ili ampitishe Mgombea wake aliyetoa rushwa kununua Ubunge wa Vijijini basi asimlaumu Dkt. Bashiru kwa sababu Bashiru hakukata jina la mtu ila Kamati Kuu ya CCM ndiyo ilipitia majina yote ya Wagombea na ilipata taarifa zao kutoka kwenye Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama.
Au kaandika maneno ya chuki dhidi ya Bashiru akidhani WanaCCM tunamchukia Dkt. Bashiru ? Ndugu Jumaa tambua sisi wanaCCM Dkt. Bashiru hatumchukii hata kidogo bali tunamshukuru kwa utumishi wake ndani ya Chama, kwa sababu kupitia uongozi wake ndiyo wakati ambao CCM imepata Wabunge wengi kuliko nyakati zote.
Kwa kuwa unachuki binafsi na Dkt. Bashiru unatuaminisha wanaCCM wenzako kuwa wewe ni Fisadi uliyejificha kwenye kivuli cha CCM, kama ni hivyo tukwambie tu ukweli umekosea njia Maana Mwenyekiti wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameshasema atawanyoosha nyinyi mafisadi.