Kinachomsumbua m-NEC Haji Jumaa si Dkt. Bashiru bali ni ufisadi

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
208
500
Kiukweli si kawaida sana kwa sisi wanaume wa Pwani ambao tulipelekwa jando na kufunzwa na Mababu zetu kumkuta mtoto wa kiume anaongea sana kama Kasuku.

Nimesikitishwa na maneno ya hovyo na tuhuma zisizo tija zilizotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (MNEC) Haji Jumaa dhidi ya Katibu Mkuu wetu aliyepita Ndugu. Bashiru Ally na Mwenezi Mstaafu Polepole nimejiuliza nini kimekukuta MNEC au alishikwa pabaya. Moja ya mambo ya niliyojiuliza Haji Jumaa anamchukia Dkt. Bashiru kwa kosa gani au sababu aliamua kukirejesha chama kwenye misingi ya Nidhamu, Haki na weledi na kupambana na Mafisadi wa mali za chama.

Hata kama MNEC Haji Jumaa alikula Pesa kwenye kura za maoni ili ampitishe Mgombea wake aliyetoa rushwa kununua Ubunge wa Vijijini basi asimlaumu Dkt. Bashiru kwa sababu Bashiru hakukata jina la mtu ila Kamati Kuu ya CCM ndiyo ilipitia majina yote ya Wagombea na ilipata taarifa zao kutoka kwenye Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama.

Au kaandika maneno ya chuki dhidi ya Bashiru akidhani WanaCCM tunamchukia Dkt. Bashiru ? Ndugu Jumaa tambua sisi wanaCCM Dkt. Bashiru hatumchukii hata kidogo bali tunamshukuru kwa utumishi wake ndani ya Chama, kwa sababu kupitia uongozi wake ndiyo wakati ambao CCM imepata Wabunge wengi kuliko nyakati zote.

Kwa kuwa unachuki binafsi na Dkt. Bashiru unatuaminisha wanaCCM wenzako kuwa wewe ni Fisadi uliyejificha kwenye kivuli cha CCM, kama ni hivyo tukwambie tu ukweli umekosea njia Maana Mwenyekiti wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameshasema atawanyoosha nyinyi mafisadi.
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,081
2,000
Hivi nidhamu ya Bashiru unayoongelea ni ile ya kumpitisha nyumba ndogo yake kugombea jimbo mojawapo hapo manyara na kumkata aliyeoongoza kura za maoni? Bashiru na Polepole walikuwa mzigo kwa CCM.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
45,278
2,000
Hivi nidhamu ya Bashiru unayoongelea ni ile ya kumpitisha nyumba ndogo yake kugombea jimbo mojawapo hapo manyara na kumkata aliyeoongoza kura za maoni? Bashiru na Polepole walikuwa mzigo kwa CCM.
Sure mkuu walimuacha Ester Mahawe
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,982
2,000
Kuna watu watafuta umaalufu wa kisiasa kwa kupitia mgongo wa Balozi Bashiru na Mh. Polepole.

Kwa mwendo huu vyeo vya katibu mkuu na Msemaji wa chama vitakosa mvuto.

CCM jifunzeni kuheshimu wastaafu.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Bashiru na Polepole walikuwa washirika wakuu kwenye serikali dhalimu ya kidikteta.

Bahati mbaya, hawatapata nafasi ya kujisafisha dhidi ya uovu uliotendeka wakiwa washirika wakuu. Wataishi na simanzi maisha yao yote.

Damu za waliouawa na waliotekwa na kupotezwa, na wale walioteswa, zitawafuata mpaka siku zao za mwisho. Mikono yao imejaa damu kwa sababu walikuwa washirika wa karibu wa aliyekuwa akiuondoa uhai wa wote wanaomkosoa.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,684
2,000
Vita vya Panzi, furaha kwa Kunguru! 🐧Nipo tu hapa nawachora! Ili mpaka itakapo fikia mwaka 2025, muwe mko hoi bin taabani!

ccm asili vs ccm makinikia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom