Kinachokuumiza ni mawazo yako mwenyewe

nimemwona capt tamar na ushuhuda wake,hajaingia ndani kutuambia nini kilimsibu,nahisi halikuwa jambo kubwa sana ndio maana ikawa rahisi kwake kulipotezea,kwani masahibu yanatofautiana,yapo mengine si rahisi kuyapotezea haraka,
Nafikiri alisema ni dhuluma, na hiyo hali ilimtesa na kumuumiza sana mpaka alipoamua kufikiri tofauti
 
Sidhani kama kuna mtu anawaza from know where. Kuna mambo yanawasibu watu kama vile kutafuta fedha, ajira, kudhulumiwa mali, kukosa watoto, kifilisika na kadhalika.
Sasa hapo utaacha kuwaza kweli? Je, shida yako isipotatuliwa, utaondoaje mawazo?
Know where = nowhere
 
uploadfromtaptalk1463504015497.jpg
 
3150e1e2ea0b596d7851e3a0f2f68e71.jpg


Tulikuwa na ile mada ya ongezeko la watu wanoongea pekeyao! Wameumba maumbo Wameumba watu vichwani mwao kisha wamewabeba wanatembea

Nao wanaongea nao
Wanabishana nao
Wanagombana nao
Wanawalaani
Wanawalaani
Wanawatusi kuwakejeli na hata kuwaua kihisia tu

Ni usongo wa mawazo na vurugu za kimaono, kwa kushindwa kujimudu! Kwa kushindwa kuzitawala hisia wengi huishia kupata magonjwa ya shinikizo la damu hata kufa

Unakubalije mtu akupotezee furaha yako? Wakati unahangaika kuwaza na kuwazua ukipata majibu mia kwa mpigo huyu anayekusababishia maumivu yote haya yuko pahala mbali kabisa na wewe akiyafurahia maisha yake

4822d873d17bc7ee75d8808c089b762e.jpg


Tunaishi katika dunia ya changamoto za kila namna
Changamoto za mahusiano
Changamoto za kipato
Changamoto za kazi
Changamoto za majukumu mbalimbali
Changamoto za ki familia hata kiukoo
Changamoto za marafiki ndugu na jamaa nk nk

Jifunze kuwa wewe jifunze kusimama imara, usikubali wala kuruhusu hata siku moja mtu mwingine nje ya nafsi yako akutawale na kuyatawala mawazo na hisia zako kwa namna yoyote ile kwakuwa vyovyote iwavyo yeye atabaki kuwa yeye na wewe utabaki kuwa wewe

Ni pale tu utakapolikubali hili utayaona maisha na changamoto zake katika mtazamo tofauti kabisa

f76e3b00dc812c39025d27937dfae26f.jpg
Nikua natafuta thread ya kuniliwaza sasa nimeipata nilale sasa
 
Point yako imesimama vyema ila inategemea na aina ya changamoto yenyewe inayokuandama....changamoto zingine inachukua mida sana kuzi take easy...hivyo kuwaza na kuwazika ni unavoidable mkuu.
 
Point yako imesimama vyema ila inategemea na aina ya changamoto yenyewe inayokuandama....changamoto zingine inachukua mida sana kuzi take easy...hivyo kuwaza na kuwazika ni unavoidable mkuu.
Ningekuwa natumia ID bandia kuna vitu vizito sana ningeshuhudia hapa na wengi wasingeamini lakini kupitia kujiamini na roho ngumu sana nimeweza kuvuka vikwazo vyote na kuwa mimi nilivyo leo
 
Back
Top Bottom