Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,865
- 730,439
Tulikuwa na ile mada ya ongezeko la watu wanoongea pekeyao! Wameumba maumbo Wameumba watu vichwani mwao kisha wamewabeba
Wanatembea nao
wanaongea nao
Wanabishana nao
Wanagombana nao
Wanawalaani
Wanawatusi kuwakejeli na hata kuwaua kihisia tu
Ni usongo wa mawazo na vurugu za kimaono, kwa kushindwa kujimudu! Kwa kushindwa kuzitawala hisia wengi huishia kupata magonjwa ya shinikizo la damu hata kufa
Unakubalije mtu akupotezee furaha yako? Wakati unahangaika kuwaza na kuwazua ukipata majibu mia kwa mpigo! huyu anayekusababishia maumivu yote haya yuko pahala mbali kabisa na wewe akiyafurahia maisha yake
Tunaishi katika dunia ya changamoto za kila namna
Changamoto za mahusiano
Changamoto za kipato
Changamoto za kazi
Changamoto za majukumu mbalimbali
Changamoto za ki familia hata kiukoo
Changamoto za marafiki ndugu na jamaa nk nk
Jifunze kuwa wewe jifunze kusimama imara, usikubali wala kuruhusu hata siku moja mtu mwingine nje ya nafsi yako akutawale na kuyatawala mawazo na hisia zako kwa namna yoyote ile kwakuwa vyovyote iwavyo yeye atabaki kuwa yeye na wewe utabaki kuwa wewe
Ni pale tu utakapolikubali hili utayaona maisha na changamoto zake katika mtazamo tofauti kabisa