Kinachofanya Marehemu asimwe ni Unafiki wa watu ndani ya jamii!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Kwema Wakuu!

Taikon nikifa msinionee haya, nisemeni Kwa mazuri niliyofanya, alafu nitukaneni na nipeni vidonge vyangu Kwa mabaya niliyoyatenda.
Taikon Hapendi watu wanafiki wanafiki! Wachungaji na masheikhe endapo mtapewa jukumu la kutoa ibada ya mazishi yangu, ikiwa mnajua mazuri yangu yasemeni, na ikiwa mnajua mabaya muyasema, mbele za watu watu wajifunze.

Hamuwezi kuniheshimu Kwa unafiki nikiwa Maiti inayooza, hatuwezi heshimu maiti Kwa kujiingiza kwenye unafiki. Maiti ipewe haki yake hiyo ndio Heshima. Marehemu apewe haki yake ikiwa ni pamoja na kumsema Kwa mazuri na mabaya.

Mbona kina Farao tunawasema kila siku katika nyumba za Ibada, kwani yeye Hakuwa na heshima, unafikiri Hakuwa na ndugu au Hana Ndugu.

Kina Adolf Hitler, musolini, Idi Amini Dada, Sadam Hussein n.k.

Ni Mpumbavu na Mnafiki pekee ndiye atakayepotosha haki ya marehemu Kwa kutaka asemwe Kwa mazuri pekee utadhani alikuwa Malaika.

Unafiki! unafiki! unafiki!
Tena unafiki huu upo zaidi Kama akifa kiongozi Mkubwa au mtu mashuhuri au Tajiri. Ndio kunakuwa na wapambe na wanafiki wa watu hao.

Wewe ukitaka usisemwe vibaya tenda wema kadiri uwezavyo na ujiepushe na mabaya makubwa makubwa.

Kama hutaki Mama au Baba yako au ndugu yako, au mke wako, au mume wako asisemwe Vibaya siku Amekufa, basi mwambie asitende Mabaya. Awe mwema na atende Kwa kiasi Kwa kila jambo.

Sio jitu liwe linafanya maovu makubwa ndani ya jamii alafu siku limekufa lisisemwe, utasemwa! Utanangwa, watu hawatapata faida yoyote Kwa kukusema lakini angalau utakuwa umedharaulika na jina lako litakuwa baya katika mapito yako.

Taikon nikiwa hai, nichaneni, nipondeni na nizodoeni Kwa mabaya niliyoyafanya, nikifa msiogope nisemeni tuu, nitoleeni mifano mibaya muwapo katika jamii.

Mwalimu ukiwa unafundisha shuleni, toeni mifano kuwa lilikuwepo jitu moja liliitwa Taikon lilikuwa liovu, liuaji, lidhulumati, semeni mabaya yote Kwa watoto.

Wachungaji na masheikhe, nikitenda Uovu na nikavuka mipaka, msione haya kulitumia jina langu makanisani na misikitini kuwaonya waumini wenu wasiwe na matabia ya hovyo Kama Mimi.

Majitu maovu yanapaswa kusemwa Kwa Uovu. Hata hivyo, wema nao usisahaulike.

Nimemaliza!
Unaweza nichana Kwa kuanzia ikiwa unaona nimekosea wala usinionee haya.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Unamtukanaje au kumtuhumu marehemu ili hali hawezitena kukujibu?
 
We ni mnafki, juzi hapo umekuja na mada ya kumtetea mwenda zake kwasababu anasemwa kwa mabaya

Ikiwa una mkono mbaya, jitahidi uwe na mwandiko mzuri, wakishindwa kutazama unavyoandika, waweze kuangalia ulichoandika.

Nimeangalia ichoandika
 
Nitamtetea Kwa kuwashambulia wao Kwa kuwa nao wanamabaya pia, lakini sio kumtetea kwamba yanayosemwa ni uongo
 
Unamtukanaje au kumtuhumu marehemu ili hali hawezitena kukujibu?

Kwani watu wanahitaji majibu Yao/yake/ yangu pindi nikifa wakinifahamu Kwa mabaya?

Ukitenda Mema utakuwa na jina jema, ukitenda mabaya utakuwa na jina Baya.
Hiyo ni nature Mzee
 
Nitamtetea Kwa kuwashambulia wao Kwa kuwa nao wanamabaya pia, lakini sio kumtetea kwamba yanayosemwa ni uongo
Wao kuwa na mabaya ni issue nyingine, usitumie mabaya yao kama justification ya kufanya kosa la mwingine lisiwe kosa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom