Waziri Mkuu Majaliwa aibukia Kariakoo, azungumza na wa fanyabiashara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
91b54b46-a55d-407a-abe5-5dcee6da7050.jpg

50277ebd-0d4b-4eb6-a56d-d3a993ef5ad5.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika katika Soko la Kariakoo ambako wafanyabiashara wametangqza mgomo tangu asubuhi.

Majaliwa amelazimika kuacha Bunge na kuja kwa dharura ili kuzungumza na wafanyabishara hao kwa lengo la kupata suluhu.

Awali taarifa kutoka ofisi yake ilisema kuwa kiongozi hiyo angekutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko hilo keshokutwa Jumatano Mei 17, 2023.

Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa alipanga kukutana pia na mawaziri wa sekta hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye ofisi yake Magogoni-Ikulu na kuratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Hata hivyo, wafanyabiashara hao hawakusitisha mgomo huo na kudai kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan.
b9726254-b956-4fc2-8ba4-1270fb890615.jpg

bce0efa3-2794-42f0-bc82-fbf7980b2308.jpg
 

Attachments

  • 50277ebd-0d4b-4eb6-a56d-d3a993ef5ad5.jpg
    50277ebd-0d4b-4eb6-a56d-d3a993ef5ad5.jpg
    95.2 KB · Views: 1
Wafanyabiashara kwa pamoja tumemuwelewa waziri Mkuu na kuanzia sasa hivi tunafungua maduka yote na biashara inaendelea.

Kazi iendeleeeeeeeeee
Tujenge uchumi wa nchi yetu.
 
Nchi ni yetu sote, tusikandamizane! Rasimi sasa biashara tunafungua
Mimi namshukuru sana waziri mkuu kwakukemea tabia mbaya za hao wakusanya kodi anakuja nakukuamia kama huna leseni Funga mimi nifundi kushona guo alikuja afisa biashara nakunitaka leseni Chelehan moja niliogopa mpakaleo toka Ijumaa sijafungua na sijui kama nastahili kukata leseni!
 
Hadi kesho Tz nzima ingekuwa ishasimama biashara.

TRA yuko kwenye mtanziko
 
Nchi ni yetu sote, tusikandamizane! Rasimi sasa biashara tunafungua
Kwani mkifunga nchi itaathirika nini. Mnakwepa kodi sababu ya kuuzia mizigo kwenye meghala, mmekalia kufanya magendo. Kuku nyie.
Sipendi namna Serikali inavyobembeleza watu wanaokiuka sheria
 
Tayari maduka mengi yamesha funguliwa muda huu wa saa 12 kamili jioni tutapiga kazi Hadi saa 6 usiku wateja wetu karibuni sana mpate huduma
 
Kama kweli PM angesubiri mpaka jumatano ndio akaongee na hao wafanyabiashara wasioonekana kuyumba mambo yangechelewa zaidi.

Hapo ingewezekana huo mgomo ungefika ijumaa hivyo hii wiki yote mambo yaende hovyo, na serikali ikose mapato, bora amewawahi hao jamaa mapema.

Issue ni kama hayo madai yao kweli yana msingi, na kama yatapata suluhu ya kudumu, au ndio malalamiko ya chini chini yataendelea kisha mbele ya safari mambo yaharibike tena.
 
Back
Top Bottom