Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 84
- 1,562
Mwanaume hawezi kubakwa anayebakwa ni Mwanamke tu. Ni maneno ya tarehe 10/11/2023 ya Mahakama ya rufaa chini ya Majaji watatu.
Ni katika Jinai No.369/2020 Kati ya Jack Mahembega Dhidi ya Jamhuri wakati ikifafanua Kifungu cha 130, Sura ya 16, Kanuni za Adhabu RE 2022.
Mahakama imefafanua kuwa kinachobakwa anacho mwanamke na mwanaume hana kinachoweza kubakwa.
Kinachobakwa ni Uke na hii ni hata kwa kuingiza kidogo tu(Slight Penetration) bila ridhaa ya mwanamke itahesabika amebakwa. Mwanaume hana uke na hivyo hana cha kubakwa.
Imesema kuwa isipokuwa walicho nacho wote wawili mwanaume na mwanamke ni kile kinachoweza kulawitiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 154 Kanuni za Adhabu RE 2022.
Ni kwa msingi huu kuwa mwanaume hawezi kubakwa. Hakuna kosa la kumbaka mwanaume. Mwanaume habakwi.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza hili swali kuwa inakuwaje ikiwa mwanamke atamlazimisha mwanaume kufanya nae mapenzi bila ridhaa yake.
Hii ipo na huwa inatokea lakini majibu yake ndio hayo. Ukilazimishwa na mwanamke hujabakwa. Mwanaume habakwi.
Na hii ni hata mwanaume akiwa na umri mdogo akalazimishwa au kushawishiwa na mama mtu mzima. Kwasababu tu ni mwanaume basi huyo mama hajabaka.
Hii haimaanishi kuwa hawezi kushitakiwa, laa hasha. Atashitakiwa lakini kwa makosa mengine ya Jinai dhidi ya Maadili(Offences against Morality) ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia nk, lakini sio kubaka.
Mwanaume habakwi, Nadhani sasa tumeelewana Viongozi.