Kinacho muangamiza Lowassa ni Ukimya wake!

Kinacho muangamiza Lowassa ni Ukimya wake!

This is a hard fact!
Lowassa ana siri kubwa moyoni

Lowassa amekuwa kiongozi mkubwa katika taifa hili. Mazuri aliyoyafanya yalionekana na yataendelea kukumbukwa. Kama binadamu hawezi kukosa kasoro hapa na pale, ndio asili ya maisha na kuishi kwa binadamu yeyote.

Kilichokuja kukumbana na bwana huyu katika utendaji wake kama Waziri mkuu na sakata lililolitesa taifa la RICHMOND.
Toka wakati huo Lowassa ameonekana kama shetani, msaliti na fisadi mkubwa wa taifa hili.

Najiuliza ukweli hapa ukoje?

Nijuavyo mradi wa RICHMOND which was a MULT BILLION SHILLINGS CONTRACT, hauwezekani ukamhusu Lowassa pekee. Ni lazima cabinet yote ilihusika hatua kwa hatua hadi final conclusion yake.
Kum-single out MTU mmoja kwa jambo ambalo wengi wanapaswa kuwajibika, Its just not fair!

Kwa kauli ya Mkuu wa Nchi, hili kwa Lowassa lilikuwa ni ajali tu, (MANENO HAYA HAKUTAMKA KWA BAHATI MBAYA)

Lakini hata Lowassa mwenyewe kwa kauli yake siku ya kujiuzulu alitabanahisha kuwa anajiuzulu ili "KUKILINDA CHAMA CHAKE NA SERIKALI YAKE", Bila shaka kwa makosa haya ambayo yaneweza kukigharimu chama na serikali yake!

Leo anapigwa vita hadi ndani ya chama hicho alichokiokoa

Najiuliza siku akiamua nayeye kufunguka, Itakuwaje?

Subiri, mambo mazuri hayataki haraka. The time will come
 
Hivi sasa ccm ni chama cha kundi fulani la watu na tayari wana Rais wao.
Lowassa hata akigombea bila kampeni anashinda Urais.
Ukweli ni kwamba mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili yanaonekana.

Umma ni zaidi ya CCM.Lakini labda ipo siku ataelezea umma.Tactical smart timing tusubiri.
 
Lowassa ni kama ule mti wa mbuyu uliokatwa Tabora (W) Uyui halafu ukasimama ghafla wenyewe.

Pasco kuna mambo mengi hatuyafamu kuhusu EL na sakata ya Richmond.EL Aliachia ngazi kama inshara ya kuwajibika.Laiti angefukuzwa halafu akashtakiwa.Lakini hilo alikufanyika,kwanini?EL Ni mbuzi wa kafara?Au ni sinema zinazoanzia mwisho zikielekea mwanzo?
 
Mkuu Toothpick, silence yake ndio silaha yake kubwa na ndio karata yake ya mwisho!.

Wenye akili zao, wameishaelewa!, hebu mfuatilie JK, na Kinana kama wana udhubutu wa kumtaja EL!, hao wanaotaja taja ni wajinga wajinga tuu wasio elewa who's the real one behind Richmond!, EL ni mbebaji tuu wa mizigo ya watu!.
Kimya kingi kina mshindo mkuu, subirieni 2015, kama CCM ina jeuri ya kutomteua, itakuwa ndio imemwaga ugali, naye atamwaga mboga, msioelewa ndio mtaelewa!.

Hivi mtu mwenye akili zake timamu hawezi kujiuliza, kama huyu mtu amejiuzulu kwa kashfa, anawezaje tena sio kuutaka urais, bali hata kuufikiria tuu huo urais?.

Pasco

Nyie liyumbisheni taifa kwa kukaa kimya huku mnafumbia macho wezi. Leo mnataka kutudanganya kwamba Lowasa hausiki bali mtu mwingine, na kama ndivyo kama kuna fisadi zaidi ya EL kwa nini asitajwe? au huyo fisadi anamasilahi mapana kuliko nchi?

Lowassa usiposema mapema jambo hili usisumbuke kuchukua form ya ubunge wala urais. Kaa kimya hivyohivyo upumzike kimyakimya! Msituchezee katika nchi yetu yenye utajiri mkubwa wa rasilimali misitu nk. Lowasa huyohuyo hakutumia misitu yetu kutengeneza madawati ya shule, wazazi wananunua dawati ndo mwanafunzi anapokelewa af mseme lowasa mtendaji bure kabisa!
 
Mara nyingi debe tupu haliachi kutika, Lowassa ni jemedari wa kweli na hakuna hasiye fahamu. Wameanghaika naye miaka nane ili kummaliza na wamemshindwa leo wanataka kupandikiza uchafu juu yake lakini wamechelewa na acha umma uamue juu yake na sio kikundi cha watu wachache pale Ikulu.<br>Lowassa hana siri yoyote ya kuficha wala kuiweka wazi, waambieni wazabizabina akina Mwakyembe na ndugu yake sitta hao ndio wanaijua RICHMOND, mbona sasa hawaongei?<br>Majibu ya Lowassa mtayapata October na wote wapayukaji mtaachwa midomo wazi.
 
Lowasa alishajiangamiza mwenyewe ukimya unamaanisha yeye mwenye ameshakata tamaa za kugombea uraisi.
 
Conspiracy theory, eti wakimwaga ugali yeye atamwaga mboga. Naona mmeamua kujilipua wenyewe kwamba hakuna wa kuaminika CCM issue kwao ni kwa kiasi gani wanaweza kutunziana siri za ufisadi, ukatili na uzandiki. Kuanzia mwaka huu hatuhitaji serikali inayotumia blackmail au conspiracy theory. Wote mnamwagwa hata mkimwagiana ugali na mboga, hakuna anayetosha kuliongoza taifa hili. Tena mkitajana ndio safi maana CCM will be deleted mbendembende.
 
....kwa hakika na ukweli kabisa tangu huyu baba atangaze kuanza safari ya matumaini pale kwao waswahili wako nae.Hii nchi tuko huru na hakuna taasisi yoyote ya umma ambayo inatakiwa kumfungia mtu kuendesha harakati zake za kisiasa kwa njia ya amani.Lowasa haendi kugombea ubunge...sasa mbona anabanwa hivyo,anasemwa hivyo,leo fadhila anazopewa ni kama za pundamilia.Lowassa pambana,ikibidi njoo UKAWA.Kwani hawa wa CCM hawavunji KATIBA YA NCHI?
 
kosa kubwa la Lowasa ni kutofuata ushauri wetu sisi kina gogo la shamba ukimywa wake utamponza
 
Kama anaona anàonewa so ajitoe tu,si alisema anaweza kuhama? sasa anangpja mini CCM?
 
Back
Top Bottom