Kinacho muangamiza Lowassa ni Ukimya wake!

Kinacho muangamiza Lowassa ni Ukimya wake!

jinga mwenywe njoo na MTU wako unayefikiri ni msafi tumchambue Kama karanga

Pole sana, akili kiduchu full kupayuka.

Hatuko kuchambuana bali kujenga hoja imara kulingana na mada husika.

Ni vyema ukawa na kifua kwa jazba zisizo na msingi.
 
Mkuu Ben, kuna things you can't afford to loose or let it go!, kuliko aseme, wataamua au bora ateuliwe yeye!, (as a reward kwa silence yake), au anyamazishwe jumla!.

Yaani leo Watanzania waambiwe the 'real richmond' ambaye ndiye huyo huyo 'dowans', na ndiye huyu huyu 'simbion!' na usikute anaweza pia kutoa siri za yule mwenye zile 50% ya PAP anayeitwa Simba!, kweli patakalika hapo?!, hapo si ni itakuwa kuifungulia malango yote ya ikulu na Chadema kufanya just a walk over!. Mtu ukiisha jijua na mwizi, na kuna mtu alikuona siku ulipoiba, ama utakuwa tayari kulipia any cost kwa silence yake, au kumyamazisha jumla!. Hili la pili ndilo ninalolihofia!. Hilo la posibility ya kutoteuliwa wala sina shaka nalo!.

Jamaa wa jikoni, anatumia style ya kumtuma kila mtu kugombea, ili wagombea wawe wengi, wakichinjiwa baharini, kiwe ni kilio cha wengi, hivyo ni kama harusi!, nimenong'onezwa kuna mtoto wa jina jema ambaye naye ameshauriwa achukue tuu fomu ili kumuenzi baba yake!, tena subirieni, hao wengi waliojitangaza wengi ni wasindikizaji tuu!, Januari na Mwigulu ni serious kwa kuitumia JK style ya 1995, they are not for 2015 bali wanajiweka tayari for 2025!, na kwa maoni yangu, that will be the time ripe kuwakabidhi the opposition, kina Ben huo sasa ndio utakuwa muda wenu!.

Pasco

Pasco

Pasco ya akina January najua ni political bargaining strategy. Hata hivyo huyo mtoto wa "Jina Jema" nae atakua ameingia katika siasa za kumdihaki baba yake kwa kuwa anajua atakua ameshauriwa ili kuhalalisha uharamia fulani tu unaopingana na principle za "Jina Jema" maana mwishowe hatateuliwa yeye

Hata hivyo hakuna silaha iliyomuongezea mileage ndogo kisiasa EL kama Ukimya wake ingawa najua katika Ukimya wake huu unaweza kumgharimu kama extreme strategy zitatumika.Ukimya wake sio usalama wake

Unless kama ameshaandika hata kakitabu na akahakikisha Huyo Richmond Halisi,Mwenye Symbion ,Dowans na Simba Trust anajua kuwa kuna document imeandikwa na umeachwa wosia kichapishwe muda fulani incase of anything

Ukimya wake unaweza kuwa hatari zaidi kwake yeye binafsi
 
Last edited by a moderator:
EL hawezi kusema ukweli,anaogopa kutolewa kucha na meno bila ganzi
 
Hakuhusika wakati yeye ndiye alikuwa mtendaji mkuu wa serikali? Alipaswa awe mkali baada ya kuona mambo yanakwenda mrama. Akamezea, malalamiko yalipoibuka ikabidi awajibike. Kunyamaza kwake pamoja na ufanisi wake mzuri kulikuwa mambo yangeenda vizuri pochi ingejaa hadi kumwagika. Akizungumza sasa hivi haitasaidia kitu kwani mfumo uliopo utatakiwa kusambartishwa na hapo CCM itakuwa imekwisha rasmi.

CCM wakimpitisha itakuwa maajabu. Angekuwa msafi angejipambaua kipindi kilekile alipojiuzulu!
 
Aongee ili iweje,ajibizane na inzi na hawa mbu akina Nape na Makonda?THE MIGHTY LION WOULD LOSE HIS REPUTATION ONCE HE TOOK THE DECISION TO FIGHT THE MICE CROSSING HIS PATH!

Basi lowassa siku moja akemee ufisadi na rushwa tuone kama ataweza tamka hata neno! Au kwa kumbukumbu zako ulisha msikia popote Lowassa ana kemea Ufisadi na Rushwa??????
 
Mimi Lowassa akikemea Ufisadi kesho nita muunga mkono
 
siri ya nini, EL ni mpuuzi Fulani tu, mpaka akishgulikiwa ndo anatishia kusema ukweli basi ni fara Fulani tu ambaye hana mapenzi na TZ bali tumbo lake na familia yake

Kama ilivyo Id yako fikiri kwanza kabla huja anza kulopoka upuuzi wako
 
Kama ilivyo Id yako fikiri kwanza kabla huja anza kulopoka upuuzi wako

Mlopokaji ni wewe, sasa anasubiri au alisubiri nini kusema ukweli wote wakati anaachia ngazi kwa maneno yake??? wewe achana na kichwa hiki.
 
Nasikia CCM wanataka kumlima red card

labda wamlime mtu mwingine si lowassa, huko walipo wanamwogopa hawajui waanzie wapi kumuengua kwenye mchakato wa urais maana kimya chake hakuna anaeelewa whats behind
 
This is a hard fact!
Lowassa ana siri kubwa moyoni

Lowassa amekuwa kiongozi mkubwa katika taifa hili. Mazuri aliyoyafanya yalionekana na yataendelea kukumbukwa. Kama binadamu hawezi kukosa kasoro hapa na pale, ndio asili ya maisha na kuishi kwa binadamu yeyote.

Kilichokuja kukumbana na bwana huyu katika utendaji wake kama Waziri mkuu na sakata lililolitesa taifa la RICHMOND.
Toka wakati huo Lowassa ameonekana kama shetani, msaliti na fisadi mkubwa wa taifa hili.

Najiuliza ukweli hapa ukoje?

Nijuavyo mradi wa RICHMOND which was a MULT BILLION SHILLINGS CONTRACT, hauwezekani ukamhusu Lowassa pekee. Ni lazima cabinet yote ilihusika hatua kwa hatua hadi final conclusion yake.
Kum-single out MTU mmoja kwa jambo ambalo wengi wanapaswa kuwajibika, Its just not fair!

Kwa kauli ya Mkuu wa Nchi, hili kwa Lowassa lilikuwa ni ajali tu, (MANENO HAYA HAKUTAMKA KWA BAHATI MBAYA)

Lakini hata Lowassa mwenyewe kwa kauli yake siku ya kujiuzulu alitabanahisha kuwa anajiuzulu ili "KUKILINDA CHAMA CHAKE NA SERIKALI YAKE", Bila shaka kwa makosa haya ambayo yaneweza kukigharimu chama na serikali yake!

Leo anapigwa vita hadi ndani ya chama hicho alichokiokoa

Najiuliza siku akiamua nayeye kufunguka, Itakuwaje?

amesha chelewa kufunguka saiv akifunguka tutamuona ni mfa maji daima haishi kutapatapa, ilitakiwa pale pale alipomwagiwa ugali wake nae ange mwaga mboga hapo tungemkubali kweli anauzalendo kiasi lakn saiv lowasa ni jambazi kama majambazi mengine tu! mwenzie top manyota ni chenge wa vijisent! kama vp wafungue chama chao wata wapata wateja tu!
 
Eti Lowassa yuko kimya wakati ameyaweka mavuvuzela yake yana zunguka nchi nzima yakimuimba kama misukule iliyo kosa mwenyewe.CC TEAM LOWASSA.
 
Mwizi,fisadi,mla rushwa ataendelea kuwa bubu hawezi sema hajiamini ana madhambi kibao! Lowassa alisha laaniwa na Mwl Nyerere mnajisumbua tu kumuosha na dodoki la umeme bado hawezi ng'ala
 
Mwizi,fisadi,mla rushwa ataendelea kuwa bubu hawezi sema hajiamini ana madhambi kibao! Lowassa alisha laaniwa na Mwl Nyerere mnajisumbua tu kumuosha na dodoki la umeme bado hawezi ng'ala

Nga'la ni jina la mamako au? Mxxxxx
 
Atashinda kirahisi
10978582_860781157313292_4267746971959923684_n.jpg
 
ukimya ni hekima aliyojaliwa mzee Lowasa kutoka kwa Mungu kama mnakumbuka wakati dr mwakambe aliyewasilisha ripoti ya uongo ya sakata la richmond alisema ninanukuu,mweshimiwa spika kama tungeeleza ukweli wote serekali ingalipasuka mwisho wa kunukuu,jamani duniani kote hakuna ukweli nusu tofauti ya kusema ukweli ni kusema uongo hambao ndio mwakambe aliosema bungeni kutoka na sababu hii ndiyo maana mzee Lowasa akaweka maslai binafsi pembeni akaweka maslai ya taifa mbele akaamua kukaa kimya cha kulisaidia taifa na watu wake
 
Mkuu Toothpick, silence yake ndio silaha yake kubwa na ndio karata yake ya mwisho!.

Wenye akili zao, wameishaelewa!, hebu mfuatilie JK, na Kinana kama wana udhubutu wa kumtaja EL!, hao wanaotaja taja ni wajinga wajinga tuu wasio elewa who's the real one behind Richmond!, EL ni mbebaji tuu wa mizigo ya watu!.
Kimya kingi kina mshindo mkuu, subirieni 2015, kama CCM ina jeuri ya kutomteua, itakuwa ndio imemwaga ugali, naye atamwaga mboga, msioelewa ndio mtaelewa!.

Hivi mtu mwenye akili zake timamu hawezi kujiuliza, kama huyu mtu amejiuzulu kwa kashfa, anawezaje tena sio kuutaka urais, bali hata kuufikiria tuu huo urais?.

Pasco
Kama anasubiri apasue jibu mwezi wa October itakuwa too late. Muda huo JK atakuwa amemaliza muda wake na hata akimwagiwa mboga haitamdhuru. EL atapata wapi muda wa kujisugua na kutoa uchafu anaopakwa sasa ili watu wamwamini wakati kugombea uraisi ni wakati huohuo. Huoni kuna watu ndani ya chama wanasema hatutaki mtu wa kusugua na dodoki wakipanda kwenye jukwaa. kwa sasa anatukanua na kupakazwa matope, halafu amekuwa kimya. Lisemwalo mara nyingi hata kama ni uongo, kama halitolewi majibu unageuka kuwa ukweli. kwa vyovyote vile EL ameshikwa na kigugumizi hawezi kusema lolote sababu alihusika kwa ufisadi huo na inawezekana ndiye alikuwa kinara na hawezi kujinaua. Imekula kwake
 
This is a hard fact!
Lowassa ana siri kubwa moyoni

Lowassa amekuwa kiongozi mkubwa katika taifa hili. Mazuri aliyoyafanya yalionekana na yataendelea kukumbukwa. Kama binadamu hawezi kukosa kasoro hapa na pale, ndio asili ya maisha na kuishi kwa binadamu yeyote.

Kilichokuja kukumbana na bwana huyu katika utendaji wake kama Waziri mkuu na sakata lililolitesa taifa la RICHMOND.
Toka wakati huo Lowassa ameonekana kama shetani, msaliti na fisadi mkubwa wa taifa hili.

Najiuliza ukweli hapa ukoje?

Nijuavyo mradi wa RICHMOND which was a MULT BILLION SHILLINGS CONTRACT, hauwezekani ukamhusu Lowassa pekee. Ni lazima cabinet yote ilihusika hatua kwa hatua hadi final conclusion yake.
Kum-single out MTU mmoja kwa jambo ambalo wengi wanapaswa kuwajibika, Its just not fair!

Kwa kauli ya Mkuu wa Nchi, hili kwa Lowassa lilikuwa ni ajali tu, (MANENO HAYA HAKUTAMKA KWA BAHATI MBAYA)

Lakini hata Lowassa mwenyewe kwa kauli yake siku ya kujiuzulu alitabanahisha kuwa anajiuzulu ili "KUKILINDA CHAMA CHAKE NA SERIKALI YAKE", Bila shaka kwa makosa haya ambayo yaneweza kukigharimu chama na serikali yake!

Leo anapigwa vita hadi ndani ya chama hicho alichokiokoa

Najiuliza siku akiamua nayeye kufunguka, Itakuwaje?

Simba mwenda kimya ndiye mla nyama
 
Back
Top Bottom