Kina dada muwe makini na Foreigners

wamemnanga kule kwa mange mpaka nikajisikia vibaya

atafute pesa sasa atulie kashazalilishwa sana

Atafute hela kiasi gani? Ili amuoe nani? Mi nadhani aoe saizi yake! Mwanamke atakaye suit uchumi wake! Yeye alitaka kuoa kwenye unafuu ili abembee asitoke jasho!
 
Mnayataka wenyenu haya
Mimi nataka mzungu, haya chukuweni ao wazungu na upumbavu wenu
 
Maskini dada wa watu. Kumlaumu siwezi maana utapeli ni taaluma aisee. Kuna watu waongo nyie! Dadangu aliwahi kuuziwa viatu na nikashuhudia vikifungwa na akakabidhiwa. Tulipofika nyumbani tulichokutana nacho kilituvunja mbavu. Mi niliwahi kukutana na mmoja si mnaijeria wala mkamerun bali msukuma na nilisoma nae ila sikuwa na mazoea nae kwa hiyo hata jina sikuwa namjua. Alinipigia simu miaka 7 baada ya kumaliza chuo.

(naruka matukio) Kilichoniokoa pale ni udhaifu wa jamaa katika kupanga uongo. Nadhani hakuzingatia kubadilika kulingana na mtu anayekutana nae. Siku ya kwanza ya utapeli wa hela kanipigia kuwa gari yake iko gereji nimfate mahali flani. Nikamfata tukaenda huko gereji na kweli gari lake nililiona pale. Akaingia kwenye ofisi ya gereji, akatoka akaja kuniomba "nimuazime 40,000/= hela yake imepungua. Nikampa na tukaachania pale akaondoka na gari lake. Siku zikawa zinasogea. Alikuwa akikwepa kusema ofisi yake iko wapi.

Mara nyingi alikuwa akiongelea research alizowahi kufanya na mashirika makubwa makubwa - kwamba yeye ni researcher na consultant ila hasemi jina la firm yake wala iliko. Tukiwa na miadi atachelewa halafu atadai alikuwa na cheki nyingi za kusaini.

Nikimuuliza anakoishi anadai ni kigamboni. Nikimwambia anipeleke nipafahamu anakubali tunapanga miadi halafu siku ikifika eidha simu haipatikani au alilazimika kwenda mjini asubuhi na mapema kwa hiyo hayupo.

Of course nilishaanza kumtilia shaka toka siku ya kwanza maana nilipomuuliza kapataje namba yangu ya simu alidai alikuwa nayo toka tumemaliza chuo (miaka 7!). Kutokana na hivyo viuongo niliamua kumchunguza. Siku 1 kaniacha kwenye gari yake nikafungua droo nikakuta nyeupeee! Nilikuwa na wasiwasi hata na jina lake. Nikakumbuka kile kitabu cha graduates wa mwaka wetu nilikuwa nacho. Nikatafuta jina lake nikagundua jina lake la kwanza ndo lilikuwa la kweli, mengine yalikuwa ya uongo.

Kupata majina yake halisi ikawa msaada mkubwa. Nikawauliza watu kadhaa niliosoma nao. Mmoja akawa anamfahamu vizuri mpaka anakofanya kazi na jina la mkewe! Baada ya kupata hizi data sikumwambia kitu nikajidai bado mjinga. Siku ya siku akaniambia anaenda kufanya research ila hela alishapewa na akaitumia, ila kuna dola 8,000 atapewa akishakabidhi ripoti kwa hiyo nimwazime milioni 3!! Nikamwambia hizo nyingi sana sina. Akasema basi walau 2, nikamwambia sina, akashuka wee mpaka laki 2!!!! Nikamwambia ningempa kesho yake. (imagine kutoka mil 3 mpaka laki 2 jamani). Kesho ikafika; wacha apige simu! Sikupokea. Kesho yake nikapokea nikampa taarifa zake zote. Akaniambia hao wote walioniambia hayo mambo ni waongo yeye ndo anaujua ukweli na nimwamini yeye. Nilimkatia tu simu. Cha kushangaza huyu mtu ni mtumishi wa umma tena kwenye taasisi ya elimu ya juu yenye jina la mtu anayeheshimiwa sana nchi hii.

Sasa huyu asingejikanganya maelezo, na labda angenirudishia ile 40,000 tukaanza mchezo wa kuazimana hela na kurudishiana na kupeana bure si kuna siku ningekuja kumpa hizo milioni 3?? Wadada tuwe makini na magumegume.
 
hivi unaanzaje kumpa boyfriend hela ? pole yake jamani mahaba niue
 
Mi nilimpata mmoja baada ya kufahamiana siku 3 tu kasema he has been robbed hela ya pango! Hahaaa nilimpa pole nikamwambia kesho nitamsaidia ili asifukuzwe!
The next day nikampigia simu nampelekea hela ya pango! Baada ya 45 minutes nikampigia I have been robbed kwenye traffic lights! Guess what ahadi za kunioa zikayeyuka! Chattings zikaisha zote! Not a foreigner ni mbongo mwenzangu tu huyu! So wadada ukiona mwanaume matonya halafu anajifanya yupo serious anatangaza ndoa mchunguze!
 
Haya mapenzi ya kumpa boifrendi hela huwa siyaelewagi mie
hawa kinadada wanaojidai wako independent mara nyingi inawacost. Ukweli ni kwamba mwanamke anakuwa hatumiki kwenye mapenzi pale tu kunapokuwa na mapenzi ya kweli na ndoa takatifu. Hii mambo nyingine watu tunafanya mwanamke anatumika ila sasa kwa kuwa wanajifanya vichwa ngumu ngoja waendelee kuliwa.
 

Ungekuwa mtongozo wa Kiswahili ndo ungemruhusu aje aishi kwako eti...?Ili akupate aache kutongoza kwakizungu huyo Mcameroon.(Ushauri wa bure kwake...!)
 

tehe tehe tehe tehe watu wanapenda mteremko true luv imekuwa hadimu kama soda za alvaro
 
Women decide with their hearts not their minds na ndio maana tunatakiwa kuwalinda ninyi sema ndio hivyo ubishi wenu tu.
 
tehe tehe tehe tehe watu wanapenda mteremko true luv imekuwa hadimu kama soda za alvaro

Ndiyo sababu tumebadilika sana, na sisi tumekuwa Chaggas for life! Ukitaka kunioa nakuuliza unafanya shuuuli gani? Utaweza kunimiliki? Utanitunza na watoto wetu? Una kipato gani au una matarajio yapi? Una potentiality zipi? Lazima nikuscrutinize. siezi beba garasa kisa limenitishia kunipeleka madhabahuni!
 
Usimpe hela kama ana shida sana akamuombe baba yake mzazi. Kwani wewe ndio umemleta mjini au bush kama bado mko huko?
 
hahahaha hii kali sana
 
Ila viashiria huwa vipo sema ndio hivyo hawa dada zetu ndivyo walivyo anyway. Wanaamua kwa mioyo sio akili.
 
Huyo jamaa mbona kapiga ela kidogo ivo... wenzie wanapiga kuanzia milioni 50...
 
Aisee Matola kuna kughafirika....af kuna mazingira akili haiwezi hata kusoma mchezo maana mwenyewe anakuwa kajiandaa haswaa. Tukitulia kwa Mungu tutapona tu
Ukitulia kwa Mungu huwezi kufika huku. Tatizo tunadhani kuwa tunayajua sana maisha kuliko huyo Mungu aliyeumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…