Huyo jamaa mbona kapiga ela kidogo ivo... wenzie wanapiga kuanzia milioni 50...
Kula nikule, inategemeana na ushirikiano unaoutoa. Ha ha ha, efu kumi si ni vocha tu hiyo!
Anapiga zilizopo mkuu, ukute ana loop ya watu kibao anacheza nao mchezo mmoja, sasa akikusanya kusanya si haba. We imagine kakomba za kwenye account, dada watu akachukua mkopo wa benki, then akamalizia kukopa kwa washkaji, na alikuwa ameomba nyingi zaidi sema watu kwa kujua kipato cha dada huyo hawajampa nyingi kiivo.
Hehehee we acha tu kwanza nkaliona boya buku mbil yang afu lenyewe lichukie ina huu
Nilicheka siku moja niliona babu wa kiaustralia nae akilia kuwa alichukua mkopo wa kama dola elfu 50 ukaliwa na Mnigeria ambaye hata hakumtia machoni...
Apo sasa
Hukumtendea haki.Yaelekea hukumpenda kwa dhati huyo jamaa.
Ungekuwa mtongozo wa Kiswahili ndo ungemruhusu aje aishi kwako eti...?Ili akupate aache kutongoza kwakizungu huyo Mcameroon.(Ushauri wa bure kwake...!)
Afu nikishakupa kupa ndogo ndogo nakuibukia na proposal kwamba nimeshinda tenda ila sina hela ya kuihonga tender board. Tuchange change ili tuwin hiyo tender maana tutapata mamilion!!!!
Ukiingia tu, narudisha hadi zile zote ulizokula.
Ndiyo sababu tumebadilika sana, na sisi tumekuwa Chaggas for life! Ukitaka kunioa nakuuliza unafanya shuuuli gani? Utaweza kunimiliki? Utanitunza na watoto wetu? Una kipato gani au una matarajio yapi? Una potentiality zipi? Lazima nikuscrutinize. siezi beba garasa kisa limenitishia kunipeleka madhabahuni!
Maskini dada wa watu. Kumlaumu siwezi maana utapeli ni taaluma aisee. Kuna watu waongo nyie! Dadangu aliwahi kuuziwa viatu na nikashuhudia vikifungwa na akakabidhiwa. Tulipofika nyumbani tulichokutana nacho kilituvunja mbavu. Mi niliwahi kukutana na mmoja si mnaijeria wala mkamerun bali msukuma na nilisoma nae ila sikuwa na mazoea nae kwa hiyo hata jina sikuwa namjua. Alinipigia simu miaka 7 baada ya kumaliza chuo.
(naruka matukio) Kilichoniokoa pale ni udhaifu wa jamaa katika kupanga uongo. Nadhani hakuzingatia kubadilika kulingana na mtu anayekutana nae. Siku ya kwanza ya utapeli wa hela kanipigia kuwa gari yake iko gereji nimfate mahali flani. Nikamfata tukaenda huko gereji na kweli gari lake nililiona pale. Akaingia kwenye ofisi ya gereji, akatoka akaja kuniomba "nimuazime 40,000/= hela yake imepungua. Nikampa na tukaachania pale akaondoka na gari lake. Siku zikawa zinasogea. Alikuwa akikwepa kusema ofisi yake iko wapi.
Mara nyingi alikuwa akiongelea research alizowahi kufanya na mashirika makubwa makubwa - kwamba yeye ni researcher na consultant ila hasemi jina la firm yake wala iliko. Tukiwa na miadi atachelewa halafu atadai alikuwa na cheki nyingi za kusaini.
Nikimuuliza anakoishi anadai ni kigamboni. Nikimwambia anipeleke nipafahamu anakubali tunapanga miadi halafu siku ikifika eidha simu haipatikani au alilazimika kwenda mjini asubuhi na mapema kwa hiyo hayupo.
Of course nilishaanza kumtilia shaka toka siku ya kwanza maana nilipomuuliza kapataje namba yangu ya simu alidai alikuwa nayo toka tumemaliza chuo (miaka 7!). Kutokana na hivyo viuongo niliamua kumchunguza. Siku 1 kaniacha kwenye gari yake nikafungua droo nikakuta nyeupeee! Nilikuwa na wasiwasi hata na jina lake. Nikakumbuka kile kitabu cha graduates wa mwaka wetu nilikuwa nacho. Nikatafuta jina lake nikagundua jina lake la kwanza ndo lilikuwa la kweli, mengine yalikuwa ya uongo.
Kupata majina yake halisi ikawa msaada mkubwa. Nikawauliza watu kadhaa niliosoma nao. Mmoja akawa anamfahamu vizuri mpaka anakofanya kazi na jina la mkewe! Baada ya kupata hizi data sikumwambia kitu nikajidai bado mjinga. Siku ya siku akaniambia anaenda kufanya research ila hela alishapewa na akaitumia, ila kuna dola 8,000 atapewa akishakabidhi ripoti kwa hiyo nimwazime milioni 3!! Nikamwambia hizo nyingi sana sina. Akasema basi walau 2, nikamwambia sina, akashuka wee mpaka laki 2!!!! Nikamwambia ningempa kesho yake. (imagine kutoka mil 3 mpaka laki 2 jamani). Kesho ikafika; wacha apige simu! Sikupokea. Kesho yake nikapokea nikampa taarifa zake zote. Akaniambia hao wote walioniambia hayo mambo ni waongo yeye ndo anaujua ukweli na nimwamini yeye. Nilimkatia tu simu. Cha kushangaza huyu mtu ni mtumishi wa umma tena kwenye taasisi ya elimu ya juu yenye jina la mtu anayeheshimiwa sana nchi hii.
Sasa huyu asingejikanganya maelezo, na labda angenirudishia ile 40,000 tukaanza mchezo wa kuazimana hela na kurudishiana na kupeana bure si kuna siku ningekuja kumpa hizo milioni 3?? Wadada tuwe makini na magumegume.
Foreigners wana maneno matamu jamani.. waacheni tu watu wachanganyikiwe nao, ukitaka kubembelezwa, kuitwa baby, sweetie, nini sijui we tafuta foreigner. na maua utaletewa utafikiri jamaa ni florist, waweza hata fungua dula la kuuza maua
Umenikumbusha mdada fulani ambaye ni mwalimu huku rombo baada ya kuajiliwa alikutana na jamaa ambae kasoma nae UDOM lakn hawakuwa na ukarbu, hvyo baada ya kukuta wakaanzisha uhusiano na bidada akawa anamleta shulen akimtambulisha kuwa ndo husband 2 be, atimae akazama NMB akachukua mil. 6 akamkabidhi msela ili anzishe biashara na ndo ikawa mwisho wa kuonana na bidada akabaki hajielewi mpaka leo
Kuna dada tuko naye ofisini, sasa huku na huku akapata mchumba kutoka West Africa, huyu mchumba anadai amesoma Russia na sijui alikuwa anafanya kazi gani hapa Bongo, maana hata dada mwenyewe ukimuuliza haelewi elewi. Harafu jamaa alikuwa fasta kujitambulisha mpaka kwa bi mkubwa, akaonyesha ana nia ya kweli kabisa ya kuoa, akawa anaenda naye kwenye harusi za hapa ofisini na za kwa marafiki zao wengine.
Basi mapenzi yameendelea, jamaa akawa ndo anaendesha gari la yule dada, anampeleka ofisini na kumfata jioni. Jamaa taratibu akaanza kutumia hela ya yule dada huku akidai kuna mafao yake atalipwa soon so watakuwa poa kifedha.
Dada wa watu akachukua mkopo kama Mil 9 kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini kumbe zikaingia kwenye mkumbo wa kuliwa. Ikafikia wakakubaliana eti jamaa aende Marekani, akifika kule akishaandaa mazingira atamchukua dada yetu wa kazini akaishi naye huko mambelez. Hela ya mkopo ikaisha, akakopa kwa washkaji hapa hela nyingine kama Mil 2 ya kuongezea ili kufanikisha safari.
Jamaa sasa ni muda kama wa miezi miwili toka aende USA na hajawahi hata kutoa contacts zake kwa dada yetu, huku jamaa wanamsakama kwa madeni yao (hasa hasa ile mil 2 ya nyongeza). Facebook jamaa hayuko active tena, inshort kapotea mazima. Dada wa watu saa hizi ni full stress, mshahara unakatwa hela ambayo hakuitumia, madeni yanamwandama, mpenzi kamkatia mawasiliano.
Kwa hiyo dada zetu mfanye uchunguzi wa kina kabla ya kugawa mioyo na mali wa wageni, wengine wamekuja kuchuma vilivyo vyetu kwa njia yoyote ile.