Kina dada muwe makini na Foreigners

Kina dada muwe makini na Foreigners

Ha ha ha uuupsi what's handsome
Siongozwi na hisia wala uzuri wake
Mungu kanijalia akili

Uzuri wake nitaula or? Ndo unifanye nimuhonge
Hapana...tunapenda maisha ya mteremko sana kupokea bila kutoa jasho
Huyu mdada alifikir kwa kuwa ni mnageria ana pesa kama za kwenye movie or
alikula vyake na kutolewa out cos alimwandalia mazingira kabisa siku ya siku kidume nae kala zake.
hukushtuka hat alipomwambia anaenda ulaya
Au ndo ndoto za alinacha anaenda kuandaa mazingira nami nimfuate nikimbie mkopo bila kulipa


Ni kama miaka miwili cousin wa huyu dada aliuza hadi verossa aliyonunuliwa na baba yake kisa Mnigeria, sasa huyu dada ndo alikuwa anatusimlia jinsi ndugu yake alivyopigwa na huyo jamaa kutoka Naija huku anamcheka sana.

Sasa ilivyokuja zamu yake ndo kawa mpole kwa sasa, harafu hata gari lake sijaliona maana unaweza kuta lishauzwa pia, maana baada ya jamaa kuondoka tunagombea lift za jamaa wa hapa ofisini pamoja wakati gari lilikuwa limepona.
 
Ni kama miaka miwili cousin wa huyu dada aliuza hadi verossa aliyonunuliwa na baba yake kisa Mnigeria, sasa huyu dada ndo alikuwa anatusimlia jinsi ndugu yake alivyopigwa na huyo jamaa kutoka Naija huku anamcheka sana.

Sasa ilivyokuja zamu yake ndo kawa mpole kwa sasa, harafu hata gari lake sijaliona maana unaweza kuta lishauzwa pia, maana baada ya jamaa kuondoka tunagombea lift za jamaa wa hapa ofisini pamoja wakati gari lilikuwa limepona.

Keshaiuza huyo
 
mtu mwenyewe wala sio foreigner, katokea mbwinde tu huko kaja kapata zezeta lake kaamua kulichezesha

sahivi kunawatu wengi sana mjini hapa wanajiita wakongo na kila mmoja anajidai mwanamziki ukimshtukia anasepa
 
Sam,

Nimesema tatizo ni kufunga ndoa hali tukiwa na umri mdogo. Tumeisha funga ndoa hivyo hata tukirudi nyuma na kuwa wajamaa haitaweza kusaidia kitu. After all hatufahamu Ujamaa ni kitu gani!.

Bikra yetu imeisha ondoka tukiwa wachanga, watu wameisha toa mahali zao na shule hatuwezi kurudi kwa sababu sasa hivi maisha yetu ni kumtumikia bwana, majukumu mengi sana, elimu hatuna ya kutosha na hivi sasa msisitizo wote wa viongozi wetu ni sawa na elimu ya ngumbaru. Ukisha olewa na zaa majukumu huzidi ndani ya nyumba na huwezi kurudi utoto kutafuta elimu kwa muda maalum. Tanzania leo hii ni taifa tegemezi na tutaendelea kuwa tegemezi kwa mume hadi siku ambayo tutaamua kutoka ktk ndoa hii. Siku tutakapo mpata baba kipenzi, mzalendo -Chavez wetu.

Kuna tofauti kubwa kati ya Utawala na Uchumi. Utawala hufuata imani yenu ktk dira ya kitaifa - Ujamaa na kujitegemea. Hii ilikuwa dini ama dhehebu letu ndani ya dini hiyo ya kikomunist. Tanzania tulikuwa wajamaa na nchi isiyofungamana na upande wowote, lakini sio tafsiri ya uchumi wa nchi nzima.

Chini ya Ujamaa, kiuchumi Tanzania tuliweka mbele mikakati ya ujenzi wa miundombinu, viwanda na misingi ya uzalishaji kabla ya kuanza kufikiria hata kufanya hiyo biashara. Kwa bahati mbaya watanzania wengi walitegemea kuwepo kwa hali nzuri ya maisha wakati ujenzi huo bado unaendelea. Miaka kumi ya kwanza ya Ujamaa, Uchumi wetu ulikuwa kwa asilimia kumi kila mwaka, rekodi ambayo haijawekwa na nchi yeyote ya Kiafrika hadi leo hii lakini kila senti ilikwenda kujenga malengo yetu - ujenzi wa misingi ya - Ujamaa na kujitegemea.

Maisha yetu sisi wenyewe yalikuwa duni kupindukia - maharage mtindo mmoja, unga wa njano, nguo hatuna, viatu vya matiri n.k hizi ndizo kumbukumbku za Ujamaa lakini la muhimu zaidi kwa mwenye upeo mzuri ilikuwa Ujezi wa misingi ya kiuchumi. Unapojenga huzalishi sawa na kuwa ktk biashara, which was supposed to be our next stage. Mashirika ya Umma yasiyopungua elfu 3 yenye thamani kubwa ktk uchumi wa nchi yeyote. Songos, Na rasilimali zote zilivumbuliwa mapema miaka ya 70. Utajiri tulikuwa nao tayari.

Ni uongo mkubwa kwa viongozi wetu kudai kwamba tumengia Ubepari bila kupenda. Baada ya kifo cha USSR na siasa za Kikomunist -Utawala haikuwa na maana hata uchumi wetu lazima uchukue mkondo.

Marekani ambao ni Mabepari kwa miaka zaidi ya 200 hadi leo wanazo mali za Umma. Uingereza, Germany na France hali kadhalika. China na Urusi ambao ndio vinara wa Ukommunist bado kabisa wapo ktk stage za transition kiuchumi hali wanadaiwa kuwa mapebari, lakini Tanzania tumeisha uza karibu kila kitu hata nguo za kuvaa kuficha uchi.

Sasa nambie, hivi kweli Ubepari unakataza nchi wasimiliki asilimia 51 ya mali zao?... Je, tungekuwa tumefanya makosa gani kuuza asilimia ya mali zetu na zilizobaki kuziweka ktk soko letu la DSE? Bado tungeitwa sisi wajamaa?. Kupokea ruzuku kama malipo ya misingi ambayo tumeijenga kwa shida kubwa, miaka isiyopungua ishirini ni aibu kubwa hasa pale inapofikia sisi kuwa wapangaji ndani ya mali tuliyoijenga sisi wenyewe.

Ikiwa Kweli Chavez ni Mjamaa kwa kutokubali mali ya nchi kumilikiwa yote na wageni basi hata Marekani ni Wajamaa kwa kukataa bandari zao kumilikiwa na kampuni ya nje toka Dubai... kinacho kubalika Marekani ni huyo mgeni (foreigner) Kununuzi hisa ndani ya shirika ya Kiamerika hata kama iwe aslimia 80 lakini shirika linajulikana kama la Kiamerika na litalipa kodi na ruzuku chini ya sheria za Kiamerika. Nje ya hapo unaruhusiwa kununua asilimia 20 tu na lazima Raia wa Marekani awe na hisa kubwa. Hawa hawaitwi Wajamaa na wanayo kila haki ya kutetea mali yao lakini sii sisi akina yakheee.. ubwabwa mezani.

Sio Ubepari wetu sisi ambao unauza nchi kwa visingizio visivyokuwa na msingi.

Kweli hapa nimejifunza kitu
 
hahaha ukiwa nje unasema ivo but ukikutana na mtu mwenye tricks za kutosha mbona unaelekea kibla na pesa utatoa mwenyewe.


Midume ya ckiz mnapenda kuongwa na sie wadada wa skiz twapenda kuongwa acha mama zetu wawahonge pia achen baba zenu watuhonge......nshazoea kupewa cjui kutoa
 
Midume ya ckiz mnapenda kuongwa na sie wadada wa skiz twapenda kuongwa acha mama zetu wawahonge pia achen baba zenu watuhonge......nshazoea kupewa cjui kutoa


Mi nataka nikuhonge
 
wanawake wa siku hizi wanapenda kusikia kiingereza cha kinaijeria
 
ndio wadada mjifunze tujifunze wanaume sio wote wema na udhaifu wako ni fursa kwa wengine.

Eti mdada tutawajuaje kwamba huyu ni mwema au mkweli au huyu ni tapeli? Utatufaidisha wengi manake huu nao ni mtihani. Baadhi yetu tukipenda tunapenda kweli! Mapenzi ya kupenda uongo uongo mimi yananitesa siwezi bora nikae single tu!
 
wanawake wa siku hizi wanapenda kusikia kiingereza cha kinaijeria

Kwani mbona wengine wanatapeliwa na marioo wa kibongo tu jamani? Hivi x mume wa Dida naye ni mkongo sorry mpopo?
 
hapa wadada wengi tutajifanya ohh mie nisingeweza ujinga kama huo. i suggest to stop judging the lady,
lakini amini nawaambieni wadada wengi wakikolea katika mapenzi wako very weak and wanaweza kuamua mambo mengi ambayo baadae hujuta mtoa mapenzi akishapunguza mapenzi kwake.
huwa na hisia ya kwa vile ananipenda kwa dhati na kuniridhisha kwa nini nisimpe? na ndio hichi kwenye ndoa nyingi mama anaumia sana na majukumu ya nyumbani kwa uvumilivu haswa baba akishaonesha kumpetipeti japo kidogo halafu akaomba msaada kutoka kwa mama mamma hutoa masikini bila kinyongo.

Ndiyo sababu wananishangaza hawa watani wa jadi wanaposema hatuna mapenzi ya kweli!
 
Kuna dada tuko naye ofisini, sasa huku na huku akapata mchumba kutoka West Africa, huyu mchumba anadai amesoma Russia na sijui alikuwa anafanya kazi gani hapa Bongo, maana hata dada mwenyewe ukimuuliza haelewi elewi. Harafu jamaa alikuwa fasta kujitambulisha mpaka kwa bi mkubwa, akaonyesha ana nia ya kweli kabisa ya kuoa, akawa anaenda naye kwenye harusi za hapa ofisini na za kwa marafiki zao wengine.Basi mapenzi yameendelea, jamaa akawa ndo anaendesha gari la yule dada, anampeleka ofisini na kumfata jioni. Jamaa taratibu akaanza kutumia hela ya yule dada huku akidai kuna mafao yake atalipwa soon so watakuwa poa kifedha.Dada wa watu akachukua mkopo kama Mil 9 kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini kumbe zikaingia kwenye mkumbo wa kuliwa. Ikafikia wakakubaliana eti jamaa aende Marekani, akifika kule akishaandaa mazingira atamchukua dada yetu wa kazini akaishi naye huko mambelez. Hela ya mkopo ikaisha, akakopa kwa washkaji hapa hela nyingine kama Mil 2 ya kuongezea ili kufanikisha safari.Jamaa sasa ni muda kama wa miezi miwili toka aende USA na hajawahi hata kutoa contacts zake kwa dada yetu, huku jamaa wanamsakama kwa madeni yao (hasa hasa ile mil 2 ya nyongeza). Facebook jamaa hayuko active tena, inshort kapotea mazima. Dada wa watu saa hizi ni full stress, mshahara unakatwa hela ambayo hakuitumia, madeni yanamwandama, mpenzi kamkatia mawasiliano.Kwa hiyo dada zetu mfanye uchunguzi wa kina kabla ya kugawa mioyo na mali wa wageni, wengine wamekuja kuchuma vilivyo vyetu kwa njia yoyote ile.
Kuna mnijeria mmoja anajifanya mchungaji maeneo ya mbezi ,alikutana na dada mmoja alienda kwake kuombewa,dada hapati mtoto,cha kushangaza sasa wanaishi pamoja nyumbani kwa huyo dada,Na dada anajiweza tu,muda si muda utaskia dada analalamika kutapeliwa.
 
Kwani mbona wengine wanatapeliwa na marioo wa kibongo tu jamani? Hivi x mume wa Dida naye ni mkongo sorry mpopo?

wamemnanga kule kwa mange mpaka nikajisikia vibaya

atafute pesa sasa atulie kashazalilishwa sana
 
Wapi vick kamata alisharudishiwa chochote na jamaa au ndio baki story
 
Basi wameamua hao wacameroon, me nlikutana na mmoja Bank..Wacha aning'ang'anie....na vile mtoto nlikuwa nimetupia ushungi akaja na gia kali sana ya ndoa...Bahati nzuri sijawahi kuwaza kuolewa na foreigner even mmakonde mwenzangu wa Msumbiji....tutabanana huku huku uzaramoni....Cha ajabu katika Chating nikamuuliza unaishi wapi? Mara anambie Kinondoni, mara Magomeni, mara Kariakoo...mwishowe akafunguka eti anataka aje aishi kwangu....Mwee hapo me mwenyewe nlikuwa naishi hostel...!Nikaona hapa ni shida tu, nikampotezea...halafu mtongozo wenyewe ulikuwa kwa kizungu ndo kabisaa nikaona ananichosha kunihangaisha na dictionary...Wadada tuwe makini sana, jamaa wameamua...!
umemaliza kabisa,mtongozo wa kizungu hahahaaaa...
 
Basi wameamua hao wacameroon, me nlikutana na mmoja Bank..Wacha aning'ang'anie....na vile mtoto nlikuwa nimetupia ushungi akaja na gia kali sana ya ndoa...
Bahati nzuri sijawahi kuwaza kuolewa na foreigner even mmakonde mwenzangu wa Msumbiji....tutabanana huku huku uzaramoni....

Cha ajabu katika Chating nikamuuliza unaishi wapi? Mara anambie Kinondoni, mara Magomeni, mara Kariakoo...mwishowe akafunguka eti anataka aje aishi kwangu....Mwee hapo me mwenyewe nlikuwa naishi hostel...!

Nikaona hapa ni shida tu, nikampotezea...halafu mtongozo wenyewe ulikuwa kwa kizungu ndo kabisaa nikaona ananichosha kunihangaisha na dictionary...

Wadada tuwe makini sana, jamaa wameamua...!

Hahahaaa my dear umenifurahisha na kisa hiki! Hata miye nshakumbana na wa hivo! Haeleweki anaishi wapi wala anafanya nini story ndefu lakini nimemuweka kapuni! Jamii forums imetufumbua sana macho sisi wadada innocent!
 
Kuna dada tuko naye ofisini, sasa huku na huku akapata mchumba kutoka West Africa, huyu mchumba anadai amesoma Russia na sijui alikuwa anafanya kazi gani hapa Bongo, maana hata dada mwenyewe ukimuuliza haelewi elewi. Harafu jamaa alikuwa fasta kujitambulisha mpaka kwa bi mkubwa, akaonyesha ana nia ya kweli kabisa ya kuoa, akawa anaenda naye kwenye harusi za hapa ofisini na za kwa marafiki zao wengine.






Basi mapenzi yameendelea, jamaa akawa ndo anaendesha gari la yule dada, anampeleka ofisini na kumfata jioni. Jamaa taratibu akaanza kutumia hela ya yule dada huku akidai kuna mafao yake atalipwa soon so watakuwa poa kifedha.

Dada wa watu akachukua mkopo kama Mil 9 kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini kumbe zikaingia kwenye mkumbo wa kuliwa. Ikafikia wakakubaliana eti jamaa aende Marekani, akifika kule akishaandaa mazingira atamchukua dada yetu wa kazini akaishi naye huko mambelez. Hela ya mkopo ikaisha, akakopa kwa washkaji hapa hela nyingine kama Mil 2 ya kuongezea ili kufanikisha safari.

Jamaa sasa ni muda kama wa miezi miwili toka aende USA na hajawahi hata kutoa contacts zake kwa dada yetu, huku jamaa wanamsakama kwa madeni yao (hasa hasa ile mil 2 ya nyongeza). Facebook jamaa hayuko active tena, inshort kapotea mazima. Dada wa watu saa hizi ni full stress, mshahara unakatwa hela ambayo hakuitumia, madeni yanamwandama, mpenzi kamkatia mawasiliano.

Kwa hiyo dada zetu mfanye uchunguzi wa kina kabla ya kugawa mioyo na mali wa wageni, wengine wamekuja kuchuma vilivyo vyetu kwa njia yoyote ile.



Hakuna mkweli west africa,wote matapeli wa kufa mtu,as well as many foreigners in the world
 
Back
Top Bottom