hahaha watakoma mwaka huu, pole yake kuna rafiki yangu Alipata mnaigeria yule kaka alijifanya ni mfanya biashara na akawa anatuletea vitenge kutoka kwako tukajua kweli, ila baadae mi nilimstukia kuna sehemu nilimfuma anaongea kiswahili kizuri sana wakati akiwa na rafiki yangu anajifanya kiswahili hakipandi, mambo yakaenda mpaka akazaliwa mtoto akapewa jina la kikwao, mwanamke alikuwa anaamini kama vile anavyowaona wanaigeria kwenye sinema zao akaona na yeye mambo yake yatakuwa safi, ikafikia wakati wa kujitambulisha mwanaume akadai ndugu zake hawawezi kuja watakuja kwenye ndoa, wakwe wakaweka ngumu ikabidi akawatoe huko walipo, kumbe yule bwana alizaliwa Naigeria tu, ila ni mtanzania kakulia huku kasoma huku na kwao ni sinza mapambano na hana kazi wala nini vitenge sijui alikuwa anaiba wapi. wasichana wanabidi wawe makini sana hali ya maisha imekuwa ngumu