Kina dada muwe makini na Foreigners

Kina dada muwe makini na Foreigners

Umenikumbusha kuna kisa kimoja kilitokea mahali fulani..
Bidada alikuwa anauza duka la kaka yake na akawa anauza pesa ndefu tu kwa siku. Akatokea kijana akawa anakuja kufunga mzigo mkubwa tu hapo dukani.....mazoea yakaenda baadae wakawa wapenzi. Yule kaka akawa anakuja na briefcase imejaa mahela anampa yule dada amuwekee then jioni anakuja kuichukua..bas dada wa watu kaona mwanaume si ndio huyu....?! Siku moja yule kaka akamwomba yule dada amuazime milioni arobaini kuna mahali amekwama na asubuhi yake atarudisha. Dada wa watu wala hakuwa na hiyana akampa.....asubuhi yake ilipofika simu ya yule kaka imezimwa na hajaonekana mpaka kesho.

Shem naomba chenchi!!!
 
Kuna dada tuko naye ofisini, sasa huku na huku akapata mchumba kutoka West Africa, huyu mchumba anadai amesoma Russia na sijui alikuwa anafanya kazi gani hapa Bongo, maana hata dada mwenyewe ukimuuliza haelewi elewi. Harafu jamaa alikuwa fasta kujitambulisha mpaka kwa bi mkubwa, akaonyesha ana nia ya kweli kabisa ya kuoa, akawa anaenda naye kwenye harusi za hapa ofisini na za kwa marafiki zao wengine.


Basi mapenzi yameendelea, jamaa akawa ndo anaendesha gari la yule dada, anampeleka ofisini na kumfata jioni. Jamaa taratibu akaanza kutumia hela ya yule dada huku akidai kuna mafao yake atalipwa soon so watakuwa poa kifedha.

Dada wa watu akachukua mkopo kama Mil 9 kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini kumbe zikaingia kwenye mkumbo wa kuliwa. Ikafikia wakakubaliana eti jamaa aende Marekani, akifika kule akishaandaa mazingira atamchukua dada yetu wa kazini akaishi naye huko mambelez. Hela ya mkopo ikaisha, akakopa kwa washkaji hapa hela nyingine kama Mil 2 ya kuongezea ili kufanikisha safari.

Jamaa sasa ni muda kama wa miezi miwili toka aende USA na hajawahi hata kutoa contacts zake kwa dada yetu, huku jamaa wanamsakama kwa madeni yao (hasa hasa ile mil 2 ya nyongeza). Facebook jamaa hayuko active tena, inshort kapotea mazima. Dada wa watu saa hizi ni full stress, mshahara unakatwa hela ambayo hakuitumia, madeni yanamwandama, mpenzi kamkatia mawasiliano.

Kwa hiyo dada zetu mfanye uchunguzi wa kina kabla ya kugawa mioyo na mali wa wageni, wengine wamekuja kuchuma vilivyo vyetu kwa njia yoyote ile.


Wewe Ni Muongo!

 
Tehtehteh....ati mtongozo wa kizungu
Bora alifunhuka mapema kwamba anataka ahamie kwako ukastuka, angekupeleka geto ya mtu mwingine ungeona hapa nimpeta kidogo kidogo angeanza kukuchuna. Ila kiukweli wakaka wengi siku hizi ni matapeli wa mapenzi, naona wamechoka kuchunwa sasa wameamua kutuchuna

Bahati mbaya kwangu alipiga wrong namba....hapa angenichuna ngozi tuuu....!
 
  • Thanks
Reactions: ram
Sio maforeigners tu... hata wabongo wapo matapeli waliokubuhu...

Nilikutanaga na mmoja hivi, ye alidai anafanya kazi na watu wa migodini anasupply spare party. Ni msiri sana, simu zake anapokea kimachale au anakuwa na mfululizo wa simu nyingi na za muda mrefu.

Kuzima simu kwake ni kawaida yaan haeleweki, ni msiri na muongo wa kutupwa...

Baada ya muda akanambia kuwa ile biashara ya kusupply spare party inalipa sana, yaan shilingi inazaa shilingi. Basi nami nimjoin kwa kuanza nianze na 2mil. It means nitapata faida 2mil nyingine. Lakini titagawana faida yaan yeye achukue 1mil na mie 1mil.

Si nikakubali, lakn hapo kati akaniomba nimuazime laki 2. Atanirudishia siku 3 baadae, ile kuja kumdai si akaanza oooh ina maana huwezi kunipa hela nikiwa na shida mpaka nikurudishie....


Oooh... Machale yakanicheza, hata hizo 2mil zingeenda na maji. Kuanzia hapo sikutaka mawasiliano naye mpaka leo.

Matapeli wapo kila kona aisee, si foreigners pekee!

kuna kitu hujagundua hapa...jamaa alitaka kukutapeli hiyo laki 2 tu hiyo 2m ilikuwa ni mkakati tu...pole hata hivyo..
 
Nadhani huyu jamaa alikuwa mrefu wa kimo na kifua cha mazoezi fulani hivi,
Jamani hebu tulieni na wabongo hata kama ni wafupi au tafuteni mbegu za tukuyu na k'njaro hata wakisepa
utatumia maujanja ya kibongo kuwasaka.
 
Namkumbuka mdada mmoja ambaye alipata mchumba akataka amkopee hela.mtu mmoja akamuonya,akakataa kata kata,akakopa fedha akampa mchumba wake
huyo jamaa akasepa,sasa huyo mdada analipa deni ambalo fedha hajaitumia.
Dada zetu chonde chonde,ni kweli mapenzi ni magumu kuyaelezea lkn basi chukua muda mzoee mtu kabla ya kujiingiza kwenye madeni.
 
hapa wadada wengi tutajifanya ohh mie nisingeweza ujinga kama huo. i suggest to stop judging the lady,
lakini amini nawaambieni wadada wengi wakikolea katika mapenzi wako very weak and wanaweza kuamua mambo mengi ambayo baadae hujuta mtoa mapenzi akishapunguza mapenzi kwake.
huwa na hisia ya kwa vile ananipenda kwa dhati na kuniridhisha kwa nini nisimpe? na ndio hichi kwenye ndoa nyingi mama anaumia sana na majukumu ya nyumbani kwa uvumilivu haswa baba akishaonesha kumpetipeti japo kidogo halafu akaomba msaada kutoka kwa mama mamma hutoa masikini bila kinyongo.

Kweli kabisa. Kuna love inayofanya mtu kuwa blind kabisa. Na kuonyesha kujali kunatufanya tuumie sometimes.
Zaidi ya yote West Africans ni hatari sana sijui wana mioyo gani!
 
Matapeli ni weng tu wabongo na wagen

Ivi inakuweje tugegedane afu hela zangu tna nikakope nikupe
Hii akili ya huyu Dada nadhan ndo mapenz nivuruge kumbe anajivuruga mwenyewe
Hapa ichanaungesema inakuwaje unigegede,ingekuwa poa
 
Umenikumbusha mdada fulani ambaye ni mwalimu huku rombo baada ya kuajiliwa alikutana na jamaa ambae kasoma nae UDOM lakn hawakuwa na ukarbu, hvyo baada ya kukuta wakaanzisha uhusiano na bidada akawa anamleta shulen akimtambulisha kuwa ndo husband 2 be, atimae akazama NMB akachukua mil. 6 akamkabidhi msela ili anzishe biashara na ndo ikawa mwisho wa kuonana na bidada akabaki hajielewi mpaka leo
Namjua huyo mdada.
 
Hehehe hela yangu labda uile inform of kind MF. Kupitia Chakula lakini cash big no. Mie mwenyewe mpenda kula ya kupewa.
 
Yeleuwiiii yule kaka hatanisahau ati,..basi kuna kipindi nilipotezwa na mahabati Kama Ndege ya Malaysia. Bi mdo wacha nijikoki na mizawadi... Heeh hata muda haukusonga nikagundua jamaa garasa anatumia wanawake na ndio fahari kawake. dharau juu anaonesha. Kiliniuma si kwa kiwa jamaa ni garasa tu lakini ile mijizawadi yangu na gharama zote alafu nidharauliwe. Nililiaa ila nikajisemea moyoni huu ni ufala. Basi wee nikaamua kujifanya mjinga kwa jamaa ili walau na Mimi nirudishe vyangu... Hahahaha nilianza kumchuna Kama nimetumwa vile. Gia ya kwenda kuandaa makao kisha nimkaribishe kwangu kama ilivyotumika hapo juu ilisaidia sana kutimiza adhma yangu. Nina imani hela yangu ilirudi name chenji juu. Baada ya hapo wala sikujionesha Kama nilirudishwa na kisasi kikaenda enda kila MTU akajikataa. Kama utasoma hapa na utanistukia powa tu kwani na Mimi uliniliza. Since then ukija na gia ya kulia lia shida Mimi ndio zaidi...kwanza advertise ninajitambulisha Kama mtoto was Mkulima...
 
Basi wameamua hao wacameroon, me nlikutana na mmoja Bank..Wacha aning'ang'anie....na vile mtoto nlikuwa nimetupia ushungi akaja na gia kali sana ya ndoa...
Bahati nzuri sijawahi kuwaza kuolewa na foreigner even mmakonde mwenzangu wa Msumbiji....tutabanana huku huku uzaramoni....

Cha ajabu katika Chating nikamuuliza unaishi wapi? Mara anambie Kinondoni, mara Magomeni, mara Kariakoo...mwishowe akafunguka eti anataka aje aishi kwangu....Mwee hapo me mwenyewe nlikuwa naishi hostel...!

Nikaona hapa ni shida tu, nikampotezea...halafu mtongozo wenyewe ulikuwa kwa kizungu ndo kabisaa nikaona ananichosha kunihangaisha na dictionary...

Wadada tuwe makini sana, jamaa wameamua...![ssalama best? Hujamaliza chuo?
 
Basi wameamua hao wacameroon, me nlikutana na mmoja Bank..Wacha aning'ang'anie....na vile mtoto nlikuwa nimetupia ushungi akaja na gia kali sana ya ndoa...
Bahati nzuri sijawahi kuwaza kuolewa na foreigner even mmakonde mwenzangu wa Msumbiji....tutabanana huku huku uzaramoni....

Cha ajabu katika Chating nikamuuliza unaishi wapi? Mara anambie Kinondoni, mara Magomeni, mara Kariakoo...mwishowe akafunguka eti anataka aje aishi kwangu....Mwee hapo me mwenyewe nlikuwa naishi hostel...!

Nikaona hapa ni shida tu, nikampotezea...halafu mtongozo wenyewe ulikuwa kwa kizungu ndo kabisaa nikaona ananichosha kunihangaisha na dictionary...

Wadada tuwe makini sana, jamaa wameamua...![ssalama best? Hujamaliza chuo?

Salama...mzima?
 
Hapana aisee

Ninavyoijua hela utadhani ina sura yangu....

Hahaha.......niruhusu kucheka then nasinzia. Mapenzi mabaya sana, hivi inakuwaje unachukua mkopo halafu unampa MTU? Daah kweli dada zangu huko si kupenda ni kupotea. Mwanaume yeyote lazima awe anawajibika kabisaaaaa siyo utani! Vinginevyo watalemaaa
 
Back
Top Bottom