Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Heri tu akae kimya maana si ajabu akiongea ataanza kulaumu kuna watu wamesababisha tetemeko na hivyo atahakikisha amewashughulikia kwa nguvu zake zote!
 
Mambo yakizidi mtu inabidi afanye meditation. Yawezekana kuna novena inafanyika au kuna mfungo fulani kuombea nchi yetu.
 
Mkuu ukiunganisha Dot......bandarini.......Dot..........
Maisha ya watu kuwa magumu .....ukaongezea kuwatukana wafanya biashara alafu janga limekuja ndio inabidi wakuchangie .................
Hata kama ningekuwa Mimi ningekaa kimya !!!
 
Ni heri pia akae kimya maana akizungumza ataanza kuwalaumu na kuwasimanga watoa huduma mbalimbali wanaohangaika usiku na mchana kuhudumia wahanga wa tetemeko
 
Atasema nini huko ikiwa kule Mwakata Kahama aliwaambia kuwa hatawapatia msaada wowote ule uliokuwa umeahidiwa na mtangulizi wake, sasa ili kuonekana haegemei upande inabidi akae kimya
 
Huu sasa ndio ushirikina, kumbe mmesha mstopisha mkulu.... hamtafanikiwa uzima moto wa mafuta kwa maji!
 
Update
Wanabodi, hatimaye kimya kimerushwa na neno limesemwa ila sio tuu na roho zetu zimeponywa bali nimejiridhisha pasi shaka kuwa Mhe. Rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli anasoma jf, kwenye mazungumzo yake nimemsikia akizijibu hoja za jf kiaina, hivyo wana JF, tuitumie jf more responsibly tukitaka kumfikishie ujumbe rais, unapost tuu humu jf na rais anasoma na majibu utayapata kama mimi nilivyomsikia kwa masikio yangu mwenyewe jinsi akijibu hoja za jf! .
Naomba kuchukua fursa hii kuushukuru uongozi wa JF ambao umetoa hadi a direct access kumwambia chochote rais wetu na akatujibu.

Pasco
 
Nilikuwa na mashaka na kimya hiki maana binadamu tuna changamoto nyingi sana kiroho,kimwili na kiakili.Afya ni maisha na maisha ni afya.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…