Kimewaka bunge la Katiba

Kimewaka bunge la Katiba

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,377
Mheshimiwa Kessy atoa taswira halisi ya Muungano. Wazinzibari hawachangii chochote bara. Vipi kuwe na wabunge wao zaidi 86 wanaogharamiwa na bara wao na wake zao.

Vile vile amehoji vipi Raisi wa Zanzibar awe makamu wa Raisi kwani huku amechaguliwa na nani.

Hali imekua tete ni ngumi mkononi. Mheshimiwa mmoja kutoka zanzibar alikua anatoka nje huku akimwiita Mheshimiwa kessy wakazichape kavu kavu.

Mheshimiwa kessy aliongeza chumvi kwenye kidonda kwa kusema, hata bunge hili maalum la katiba Wazanzibari hawakuchangia.

Jamani hizo ndio hekaya za Muungano wetu wa Ajabu kama alivyo sema Raisi wa Kenya Uhuru Kenyata.
 
Kessy ni jasiri, unajua hawa wengi wao wanafichaficha haya mambo sana.
 
Jamani tumsaidieni Mheshimiwa Kessy anasulubiwa!
 
Naona nguvu inayotumika kumnyamazisha Kessy imekuwa ni kubwa sana. Mawaziri waliomo bungeni wawili, Hamad Rashid na wengineo wamesimamishwa ili kumkabili Kessy! Hakika Kessy amegonga penyewe!
 
Aliwahi sema mbunge wa zanzbar akisimama jimboni kwake,akipiga filimbi,wananchi wake wote wanasikia! Lakini mbunge huyo anapewa shangingi na analipwa malupulupu sawa na wabunge wa Tanganyika ambako jimbo moja sawa na kisiwa chote cha zanzbar.
 
Aliwahi sema mbunge wa zanzbar akisimama jimboni kwake,akipiga filimbi,wananchi wake wote wanasikia! Lakini mbunge huyo anapewa shangingi na analipwa malupulupu sawa na wabunge wa Tanganyika ambako jimbo moja sawa na kisiwa chote cha zanzbar.

Dah! huyu Mheshimiwa ni Hazina muhimu sana kwa Taifa letu!
 
Ujumbe umefika.... waliopo bungeni hawataki kusikia mawazo tofauti na yao.Hii inaonesha kuwa wajumbe wengi wamepanga nini cha kuongea, wakisikia kitu tofauti basi nguvu kubwa inatumika kumnyamazisha mjumbe alietoa hoja. Kesi ameomba radhi kwa kutumia kauli zenye kuudhi ilhali wabunge wengi wamesikika wakimuita chizi...hana akili....akapimwe akili ....kana kwamba lugha hizo zina lahaja ya kufurahisha.This is double standard.Dovutwa ameongea mambo mengi ya kuwachafua ukawa...kuna mbunge kaomba muongozo ikiwa ni halali kuzungumza vitu ambavyo havihusiani na katiba....sitta akambeza na akasema ilikuwa ni muhimu kusikia vitu hivyo...
 
Kesy Hongera sana hao waliotoka Zanzibar wengi wao tabia zao zinajuilikana mfano mdogo huyo anayetoka Chumbuni Mh....
 
Komba NAYE KAMTUSI MZEE WALIOBA MATUSI YA NGUONI. ADAI WALIOBA NI MCHAWI NA MFU ANAYESUBILIA KUFA.

KWA STAILI HII NAONA KAMA MAANDAMANO YA UKAWA YANACHELEWESHWA.

#BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom