Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Kama almasi ni milioni kadhaa haimaanishi na mimi nitakupa guarantee ya kununua kwa bei hio ukizingatia na mimi ni muuzaji sio mnunuzi wa mwisho na ninanunua quantity kubwa...

Issue yangu ya mimi na hao wadau ni kwanini wasianze kununua sasa hivi hata kwa pesa pungufu ya hapo ili wawauzie kina nyie? (Yaani wakati tunapanda na kupalilia tunauza) sio tungoje tuvune ndio tuanze kuuza wakati kuna mzigo upo tayari.
Labda sielewi, kwani kuna ubaya gani wewe kuzalisha kwa kupitia mitaji midogo midogo ya wawekezaji wadogo wadogo ambao baadaye utawalipa hata kama ni kwa bei ya chini ya ile utakayouzia (ambao ni utaratibu wa kawaida sana kwa watu wa kati); hapa kuna suala la ECONOMIES OF SCALE ambalo linaleta tija kwa pande zote na kufanya WIN WIN SITUATION!

Hata hivyo, kama nilivyo kwisha sema, nadhani tatizo ni huo mtaji wa say 2M/= ambao siyo pesa kubwa wala siyo pesa ndogo depending on your level of income! Kisha na hicho utakachopata at the end of the day - matokeo yake ni UTAPELI NA UKUKU! Haya ni majibu rahisi kwa mambo mazito! Typical of us Tanzanians, unaulizwa vipi mambo!? Unajibu POA kumbe njaa tupu!
 
Maelezo yao kwenye TV hayatoshelezi!kueleza bei ya kuuzia tu naona si sawa, wameacha mambo mengi katika uzalishaji ikiwemo:-
1) gharama za uzalishaji kwa heka, au kipande kinachoelezeka.
2)mavuno kiasi gani katika eneo walilobainisha.
3)wanashauri kiasi gani cha uzalishaji kuweza kukupa faida, maana unaweza kulima eneo ambalo udogo wake ukapata hasara.
Kiujumla wawe wawazi zaidi, nini wanaficha?
 
Mambo ya Mr. Makuku hayo
Inawezekana huo mradi umekaa kiujanja ujanja.
Ila katika pitapita zangu mitandaoni kuhusu thamani ya zao la vanila ni kubwa, niliona wakulima wa vannila nchini Madagascar wanalalamikia usalama wao pindi wakishavuna hata kama ana kilo moja au mbili hua wanafatwa usiku na majambazi yenye silaha za mato na kuwanyang'anya.
Miradi mingi ya kwenye mtandao ni vema watu wakaifuatilia kwa makini sana.
 
Kama kuna kenge mmoja alikuja kunitembelea shambani kwangu nafuga kuku wa mayai akananimbia fuga na sungura ,eti sungura mmoja anauzwa mpaka 60000 na soko lake ni kubwa wakati mimi mwenyewe na utu uzima wangu sijawaai kula sungura ,nikasema inamaana sungura ana bei sawa au zaidi ya mbuzi niakona huu ni utapeli pale tu aliponiambia aniuzie vifaranga vya sungura.
Kwa nini yeye asifuge hao vifaranga hadi wawe wakubwa aje kuwauza 60,000/=<?
 
Jamii forum ibarikiwe nilikuwa karibia niweke hela yangu kwa huyu jamaa wa vanilla nikaona badiko hapa jukwani hello nilishitika.
 
f

CCM kumejaa matapeli tupu

Chadema nako matapeli si haba

20210724_195112.jpg

images (9).jpeg
 
Labda sielewi, kwani kuna ubaya gani wewe kuzalisha kwa kupitia mitaji midogo midogo ya wawekezaji wadogo wadogo ambao baadaye utawalipa hata kama ni kwa bei ya chini ya ile utakayouzia (ambao ni utaratibu wa kawaida sana kwa watu wa kati); hapa kuna suala la ECONOMIES OF SCALE ambalo linaleta tija kwa pande zote na kufanya WIN WIN SITUATION!
Hakuna ubaya wowote, mikataba ni mikataba na kama two parties involved zinakubaliana na terms hakuna ubaya; na haya mambo hayana guarantee hata mtu genuine huenda bado mambo yasiende sawa na bado ukapoteza (ingawa lengo lake halikuwa utapeli) Na hata Vannila kupanda bei hivi ni baada ya hali ya hewa kuharibu mashamba ya mlimaji mkubwa ambaye ni Madagascar hence kuleta scarcity... ISSUES KUBWA NI MBILI...

Moja kupredict bei ya kitu miaka kadhaa ijayo ni speculation na hakuna mwenye guarantee (ingawa sio dhambi na watu wamekuwa wakifanya hivyo miaka yote) TATIZO langu kubwa la kupunguza Credibility ya hawa watu, kama soko wanalo la kumwaga kuanzia leo wangeanza kununua mzigo kuanzia leo, apart from that hii ni business ndani ya business (hata kama watu wakitajirika baadae itakuwa ni sababu ya business tofauti na hii unayosema anachukua mzigo kwako 1 million na kuwauzia sijui wateja gani three years from now kwa pesa zaidi ya 1M ili na yeye apate faida (unless otherwise faida atakuwa ameshapata kwa kuwekeza pesa in three years time) Jambo ambalo sio baya kama aki-deliver ila akishindwa ku-deliver huenda akajikuta kwenye matata tofauti na kama business model yake ingekuwa straight forward na akashindwa legally asingeweza kupata tatizo lolote
Hata hivyo, kama nilivyo kwisha sema, nadhani tatizo ni huo mtaji wa say 2M/= ambao siyo pesa kubwa wala siyo pesa ndogo depending on your level of income! Kisha na hicho utakachopata at the end of the day - matokeo yake ni UTAPELI NA UKUKU! Haya ni majibu rahisi kwa mambo mazito! Typical of us Tanzanians, unaulizwa vipi mambo!? Unajibu POA kumbe njaa tupu!
Tatizo ni wao kukataa kuchukua mzigo ambao upo at the moment wala sio pesa wala mtaji (kwahio inaonekana hakuna transparency ya kutosha) bei wanayotoa na bei iliyopo nchini tofauti ni kubwa kama soko wangekuwa nalo na kutosha hata kama mtaji hawana wangeweza kwenda benki na letter ya offer ya watu kununua mzigo mkubwa wakapewa funds wakanunua kwa wakulima wakakausha na wao kuuza kwa faida maradufu
 
Hakukutukana kama wale matapeli wa kwenye mitandao ya simu?
Yule jamaa ana kiofisi Fulani pale chanika Kwa Zoo alikua ananisisitiza nijiunge nikawa Nampa Hadi hewa Sasa yapata mwaka umepita next week nitakua pande Hizo nitaenda kumuuliza Kwa kejeri Vipi Lile deal la mahela umevuna billion ngapi vileeeee na Mimi niingie serious ?
😁😁😁😁😁
 
Super Brand wamekuwa ndiyo madalali wa huu utapeli wa Vanilla!

Hivi wao hupokea tu matangazo na kuyarusha bila hata kuchanganya na za kwao?
 
Kama almasi ni milioni kadhaa haimaanishi na mimi nitakupa guarantee ya kununua kwa bei hio ukizingatia na mimi ni muuzaji sio mnunuzi wa mwisho na ninanunua quantity kubwa...

Issue yangu ya mimi na hao wadau ni kwanini wasianze kununua sasa hivi hata kwa pesa pungufu ya hapo ili wawauzie kina nyie? (Yaani wakati tunapanda na kupalilia tunauza) sio tungoje tuvune ndio tuanze kuuza wakati kuna mzigo upo tayari.
Mimi mmoja ya watu waliobahatika kufika ofisini kwa vanilla international Ltd huku Njombe ... wenyewe wamejikita zaidi kwenye kutengeneza vanila ambayo inaendana na kiwango wanachotaka wenyewe na wana lima kiteknolojia ya kisasa zaidi hivo hawanunui kwa watu baki... Wao vanilla yao huuza nchini Comoro na bei ni 250,000 ikiwa mbichi na ikikauka bei ni 1M ....MWENYE SWALI ZAIDI ANIULIZE NITATOA UFAFANUZI
 
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Soko la hisa linasaidia nini ebu tueleze. Watu waliwekeza fedha Precision Air iliyokuwa DSE na bado return on investiment imekuwa kitendawili, ????
 
Hii kitu ikiruhusiwa na ukawekwa mfumo rahisi wa kuipeleka kwenye masoko ya nje Ulaya na Marekani naacha kila nachofanya naingia kwenye hiki kilimo !

Hivi hiwezi kutenga chumba kikubwa nyumbani kwako ukalima hii kitu kwenye buckets kisasa zaidii na watu wasijue.. alafu una process unatoa finished product kabisaaa
 
Back
Top Bottom