Kimbunga kikali chawaua watu 8 Romania

Kimbunga kikali chawaua watu 8 Romania

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,321
_97841937_41a8c690-3675-4dbc-8c9c-4722d8359547.jpg


Kimbunga chenye nguvu magharibi mwa Romania kimewaua watu wanane na kuwajeruhi karibu wengine 67, kwa mujibu mwa maafisa eneo hilo.

Wengi wa waliothiriwa walikuwa ndani na nje ya mji wa Timisoara ambapo upepo ulifika kasi ya kilomita 100 kwa saa ulioangusha miti na kuong'oa paa za nyumba.

Baadhi ya huduma za umeme na maji zimekatwa.

"Hatukuonywa kuhusu hili, ripoti ya hali ya hewa ilisema kuwa kungekwa na mvua," meya wa mji wa Timisoara Nicolae Robu aliambia runinga moja.

Huduma za dharura nchini Romania zimewashauri watu kusalia manyumbani mwao na kuzuai kwenda karibu na miti na nyaya za umeme.

Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea kaskazini kwenda Ukrain.


Chanzo: BBC
 
Mamlaka za hali ya heea huwa zinapiga RAMLI
 
tunabatishaga tu uhalisia hasa wa mambo kama hizi ni mungu mwenyewe tu mambo ya tetemeko chini ya bahari sio uchezo

vp wamekipa jina gani
 
Back
Top Bottom