Kuna mtu wakati huyu dogo anachaguliwa kama mrithi wakati tunashangaa mbona ana kaka zake wakubwa na anaenda pewa majukumu mazito ya kupambana na miamba ya western world. Jamaa akadai ukute baba yake alishamuona tangia mdogo kwenye kuchinja kuku kwa kisu nyumbani wengine wanasuasua bwana mdogo inaoneka wala aulizi mara mbili leteni kisu mimi ntachinja tu. Mzee akaona huyu ndio mwenyewe hasa.
Dah, wenzetu wako serious na na utaifa wao, hawapendi uchezewe. Sisi tunawaacha wezi wanailitafuna taifa kwa sababu tunaogopa chama kitataanguka na kufa, mali za umma zinapotezwa na wasaliti wa taifa letu.
Mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Jang Song-Taek anyongwa
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Jang Song-Taek, mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini. REUTERS/China Daily[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Na Flora Martin Mwano
Serikali ya Korea Kaskazini imesema imemnyonga Jang Song-Thaek ambae ni mjomba wa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Kim Jong-Un. Thaek ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa nchini humo amekabiliwa na adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya usaliti.
Serikali za Marekani na Korea Kusini zimelaani adhabu iliyotolewa kwa kiongozi huyo.
Jang Song-Thaek, mwenye umri wa miaka 67 alikuwa na majukumu makubwa katika serikali, na alikuwa na nafasi ya pili nchini baada ya mpwa wake, ambae ni kiongozi wa nchi hio Kim Jong-Un aliyechukua nafasi ya kuingoza Korea Kaskazini baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.
Jang Song-Thaek, alikamatwa juma liliopita, akiwa mkutanoni, na kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi jana alhamisi adhabu ya kifo.
Mtuhumiwa alichukuliwa na serikali ya Korea ya Kaskazini kama mhaini baada ya kutaka kuipindua uongozi wa chama na serikali, ili aiweke Korea Kaskazini katika mfumo mwengine, ambao ni tofauti na ule wa kisoshalisti.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Korea ya Kaskazini KCNA, Jang alikiri mahakamani yeye mwenyewe kuhusika na makosa ya kupanga njama za kuipindua serikali, akiwasihi wenzake ambao alikua akishirikana nao kulishawishi jeshi la taifa.
Jang Song-Taek, alikua naibu mwenyekiti wa halmashauri ya ulinzi wa kitaifa, ambayo ni taasisi inayochukua maamuzi mkubwa nchini humo.
Kunyongwa kwa Thaek kunatafsiriwa kama mkakati wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kutaka kuimarisha utawala wake.
Kuna mtu wakati huyu dogo anachaguliwa kama mrithi wakati tunashangaa mbona ana kaka zake wakubwa na anaenda pewa majukumu mazito ya kupambana na miamba ya western world. Jamaa akadai ukute baba yake alishamuona tangia mdogo kwenye kuchinja kuku kwa kisu nyumbani wengine wanasuasua bwana mdogo inaoneka wala aulizi mara mbili leteni kisu mimi ntachinja tu. Mzee akaona huyu ndio mwenyewe hasa.
Muasisi wa mwenyewe nyerere aloshindwa kuwanyonga mafisadi, na akaacha katiba mbovu na sheria mbovu mtu akiiba mabilioni anahukumiwa miaka 2. Hao wakorea hizo sheria wamezikuta kama china tu enzi za kina mao hadi leo ndio hivo. Sisi tumekalia kumsifia nyerere baba wa taifa na wakati hamna chochote alichofanya.

Ungekuwa ni unyama wa hali ya juu kuchukua nchi toka mikononi mwa wakoloni ambao walikuwa wamewafanya watu kuwa watumwa ndani ya nchi yao, halafu ukaanza kuwachinja kama kuku kisa eti hawafuati sheria. Bora ukae nao hivyo na matatizo yao hayo wakiwa salama kuliko kuanza kuwachinja, kama hauna alternative means za kuwawajibisha. Kwa statement yako hii nadhani mwalimu akifufuka hata leo,inaweza ikamfanya azimie tena. Lengo lake kuwa kiongozi si kwa sababu alikuwa anapenda madaraka ya uraisi isipokuwa aliwapenda mno watu wake upeo. Ilikuwa bora afe yeye awaache wakiwa wazima, kuliko kuanza kuwachinja eti kwa sababu hawafuati sheria!
Mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Jang Song-Taek anyongwa
Jang Song-Taek, mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini
REUTERS/China Daily
Na Flora Martin Mwano Serikali ya Korea Kaskazini imesema imemnyonga Jang Song-Thaek ambae ni mjomba wa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Kim Jong-Un. Thaek ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa nchini humo amekabiliwa na adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya usaliti.
Serikali za Marekani na Korea Kusini zimelaani adhabu iliyotolewa kwa kiongozi huyo. Jang Song-Thaek, mwenye umri wa miaka 67 alikuwa na majukumu makubwa katika serikali, na alikuwa na nafasi ya pili nchini baada ya mpwa wake, ambae ni kiongozi wa nchi hio Kim Jong-Un aliyechukua nafasi ya kuingoza Korea Kaskazini baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.
Jang Song-Thaek, alikamatwa juma liliopita, akiwa mkutanoni, na kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi jana alhamisi adhabu ya kifo.
Mtuhumiwa alichukuliwa na serikali ya Korea ya Kaskazini kama mhaini baada ya kutaka kuipindua uongozi wa chama na serikali, ili aiweke Korea Kaskazini katika mfumo mwengine, ambao ni tofauti na ule wa kisoshalisti.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Korea ya Kaskazini KCNA, Jang alikiri mahakamani yeye mwenyewe kuhusika na makosa ya kupanga njama za kuipindua serikali, akiwasihi wenzake ambao alikua akishirikana nao kulishawishi jeshi la taifa.
Jang Song-Taek, alikua naibu mwenyekiti wa halmashauri ya ulinzi wa kitaifa, ambayo ni taasisi inayochukua maamuzi mkubwa nchini humo. Kunyongwa kwa Thaek kunatafsiriwa kama mkakati wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kutaka kuimarisha utawala wake.
Huo ndio unyama wa kitu kiitwacho; CHAMA CHASHIKA HATAMU kikiwa nchini mwenu. Karibia wakorea kaskazini 60% wanakerwa sana utawala wa mtoto mdogo kama huyo KIm Il Jo, ila hawana pa kulalamika wala kuruhusiwa kupinga maamuzi ya chama chashika hatamu. HUyu mjomba wake alitaka kuleta mapinduzi ya kweli yenye ridhaa ya wananchi ambapo ile kasumba ya kutaka kila kukicha kutawaliwa na ukoo wa Kim IL Sung ukomeshwe. matokeo yake kaitwa msaliti na si mwenzetu, halafu ananyongwa!
nakuambieni watanzania wenzangu kila siku, Ukomunisti si lolote wala chochote bali ni sera za kishetani za kukandamiza watu na kuwaogofya nchini mwao kama tulivyofanywa na ujamaa na kujitegemea.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.