Kim Jong Un’s Uncle Executed

Kim Jong Un’s Uncle Executed

Ikulu ya Marekani imeshitushwa na hatua ya nchi ya Korea Kaskazini kumnyonga mjomba wa Rais wa Korea Kaskazini- Kim Jong Un. Taarifa kutoka White House zimetaarifu kuwa kitendo hicho ni ushahidi wa ukatili,ukiukwaji wa haki za binadamu na ishara ya kutokuwepo kwa demokrasia nchini Korea Kaskazini.Ikulu ya Marekani imedai kufanya uchunguzi kuhusu sakata hilo. Hili ni tukio kubwa kutokea tangu Bwana Kim amrithi baba yake,Kim Jong Il mwaka 2011. Rais wa Korea Kusini amesema korea kaskazini inaendesha'utawala wa hofu' na kuonya kuwa nchi yake inachukua tahadhari zote. Wachambuzi wa mambo wanaona kunyongwa kwa mjomba wa Rais Kim, bwama Jang Song Thaek kama jaribio la Rais Kim Jong-Un kujiimarisha kiutawala. Jang alihukumiwa na mahakama maalum ya kijeshi na kunyongwa kama msaliti. "Alikuwa mbaya kuliko mbwa, alitumia vibaya nafasi zake kwa kuunda kikundi cha upinzani dhidi ya serikali", Imeripotiwa na KCNA!
 
wenzetu hawana cha tume kuundwa kuchunguza. unapelekwa mahakaman siku moja unasomewa mashtaka. hukumu na kunyongwa siku hiyo hiyo moja
 
alinyonga X gf wake aliyekuwa mwanamziki maarufu wa North Korea pia kwa vile tu lipiga picha nude na ukiangalia vizuri unaweza ukakuta yeye ndiye alimuamuru kupiga picha hizo za utupu walipogambana akazianika halafu akamnyonga
 
Money Stunna; Zaidi ya hayo siyo kama hizi mahakama zetu jaji akipata msiba au kusafiri basi kesi haisikilizwi. Wao wanaunda mahakama maalumu ya kijeshi ambapo ushahidi unapatikana kwa hiari na lazima lakini hapa kwetu si ajabu taasisi za fedha zikashirikiana na mtuhumiwa kuficha uhalifu kwa 100%
 
Last edited by a moderator:
#DPRK shows pix of uncle Jang Song Thaek just before his execution.
BbUvRreCMAAvPiu.jpg:large
#DPRK shows pix of uncle Jang Song Thaek just before his execution.
 
Inasemekana pia mkasa mzima ni issue za mapenzi, kuwa huyu uncle wake(Jang Song Thaek) alikuwa ni mpenda vimwana sana(womaniser) na alikuwa ameanza kumtongoza mke wa mwenye kaya(simply his son) mrembo Ri Soul Ju na dogo akapata taarifa. Huyu mke wake inasemekana hajaonekana hadharani karibia miezi miwili sasa.

North Korea's Jang 'Tried to Woo Kim

435706.jpg

Ingawa ni kweli huyu uncle wake Kim amekuwa kwa muda mrefu akitofautiana kimawazo na chama na serikali yake lakini wachambuzi wengi wanapinga kuwa msimamo wake huo ungeweza kumpelekea kupanga mapinduzi maana kwa mfumo wa North Korea hiyo ni almost impossible.

Huyu dogo(Kim Jing Un) anaonekana ni mtata sana kuliko hata baba na babu yake. Toka aingie madarakani tayari amemfukuza aliyekuwa mkuu wa majeshi Gen. Ri Young Ho ambaye mpaka sasa naye hajulikani alipo. Pia miezi kadhaa tu nyuma inasemekana alimnyonga mpenzi wake wa zamani bibie Hyon Song Wol kwa tuhuma za kurekodi mkanda wa ngono. Kwa maoni yangu sidhani kama dogo Kim anaweza kudumu madarakani muda mrefu kama watangulizi wake.
 
Duuuu!!!!hawalazi damu, kweli huko haangaliwi mtu.
 
[h=1]
131213051148_cn_chang_kim_304x171_reuters_nocredit.jpg
Jang Song- thaek mkuu wa Idara ya Utawala katika Chama cha kikomunisti cha Korea Kaskazini

Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, limetangaza kuwa Jang Song-thaek, mtu mwenye nguvu kisiasa nchini humo na ambaye ni mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, amenyongwa.
Shirika hilo limesema Jang alituhumiwa kutumia vibaya madaraka, kupinga vitendo vya kiwana mapinduzi na kukengeuka kitabia.
Bwana Jang alihukumiwa na mahakama maalum ya kijeshi na kunyongwa papo hapo kama msaliti. Mapema wiki hii, picha za televisheni zilimwoonyesha Jang Song Thaek akiondolewa na walinzi wenye kuvalia sare kutoka katika mkutano wa Chama tawala cha Kikomunisti.
Wachambuzi wa mambo wanaona kunyongwa kwake kama jaribio la kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kujiimarisha kiutawala.
Ni tukio kubwa kutokea tangu Bwana Kim amrithi baba yake, Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.
Shirika la habari la Korea Kaskazini, limesema Jang alikiri makosa katika mahakama ya kijeshi Alhamisi, kutaka kuiangusha serikali, na alinyongwa mara moja.
Bwana Jang, ambaye anafikirika kumjenga mpwa wake, wakati wa kipindi cha mpito wa uongozi kutoka kwa Bwana Kim Jong-il kwenda kwa mtoto wake Kim Jong-un mwaka 2011, "alikuwa mbaya kuliko mbwa" limesema shirika hilo.
Alikiri kutumia vibaya nafasi zake za uwajibikaji ili kuunda kikundi cha upinzani dhidi ya serikali na kulinda maslahi yake ya kisiasa, imesema taarifa ya shirika hilo la KCNA.
130813220254_sp_kim_jong_un_north_korea_304x171_afp_nocredit.jpg
Kim Jong-un kiongozi wa Korea Kaskazini

Nchini Marekani, Ikulu ya nchi hiyo, imesema haiwezi kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo, "lakini halina sababu za kutilia mashaka taarifa hizo"
"Kama itathibitika kuwa kweli, huu ni mfano mwingine wa ukatili uliopita kiasi, unaoendeshwa na utawala wa Korea Kaskazini. Tunafuatilia kwa karibu zaidi taarifa hizo na kushauriana na nchi washirika na marafiki katika eneo hilo.," imesema taarifa ya Ikulu ya Marekani.
Picha ya Bwana Jang akiwa mahakamani, mikono yake ikiwa imefungwa, imetolewa Ijumaa.
Kabla ya kutoweka kwa neema yake, mara kwa mara alipigwa picha akiwa pembeni mwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha "utawala wa hofu"
Bwana Jang Song-thaek aliyemuoa dada wa kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il ambaye ni baba wa kiongozi wa sasa Kim Jong-un alijiunga na chama cha Kikomunisti mwaka 1972 na kupanda ngazi za uongozi katika chama hicho na pia akipanda ngazi ya juu kijeshi chini ya kiongozi Kim Jong-un
[/h]
 
King jong jamaa ni kajeri kama baba yake roho black
 
daah hapa kwetu magamba wengi wangekuwa marehemu
cc MSALANI
 
Last edited by a moderator:
Hawa ndo wana akili ukiwa msaliti ni kunyongwa tu. Tanzania tungekuwa na mtu mwenye mamlaka na ubavu kama huu ufisadi ungeshapungua na usaliti kama wa wakina Masalia na PM7 na wakina MM wangeshakula kamba. Ah kitu gani bwana
 
Back
Top Bottom