mazikukulwa
Member
- Aug 13, 2011
- 39
- 3
- Thread starter

- #21
@mazikukulwa,
tayarisha cv yako vizuri na wasiliana na 'recruitment agencies' kama radar. Kuomba mungu peke yake haitoshi maana kumbuka ni mungu huyu huyu anaombwa asaidie watu wanakufa njaa somalia, kuokoa maisha ya kwenye nchi zenye vita n.k. Kwa hiyo hata kwa logic ya kawaida kwenye list ya maombi mungu ataanza na walio kwenye '11th hour'. So you have to be on your feet na psychologically inabidi 'uamue' narudia 'uamue' kwamba lazima upate kazi! Ukishaamua utajisikia kabisa kwamba unayo nguvu ya kupata kazi.
Website ya radar hii hapa; radar recruitment the leading recruitment agency in tanzania: Home
kingine: Hao wadogo zake wanaokutegemea pia nao waanze kutafuta kazi i.e supermakets. Haitoshi kukaa na kuhuzunika kila mmoja achacharike vinginevyo utajikuta siku zote una mzigo mzito.
Pole sana Mpwa, mimi nakuomba pamoja na Kumuomba na kumtegemea sana MUNGU (jambo ambalo naliafiki na kuliamini 100%) jitahidi upate sehemu ya ku-volunteer, mimi binafsi nilisha volunteer sana sana lakini kotea huko kila waliponikubalia kufanya hivyo nilijikuta wananilipa kapesa kazuri tu na hatimae mwisho naondoka na cheti ambacho ni muhimu sana, sehemy ya mwisho ku-volunteer ilikuwa ni kwenye shirika fulani la kijamii (NGO) siku hio nilikua pale Open University nikipitia dissertation yangu ya Masters (kumbuka nimejisomesha masters mwenyewe bila mfadhili na bila kazi) nikiwa katika hali ya mwisho kabisa (pengine kama hali uliyonayo wewe leo) nikajipa moyo, nikafungua ka-laptop kangu, nikapitia anuani za mashirika kibao ya hapa Bongo, Care, Africare, Sight Savers, Save the Children n.k nikawatumia mail kwamba naomba japo kufanya Internship, huwezi amini japo ilikua siku ya jumamosi pale pale e-mail yangu ilijibiwa na moja ya shirika na baada ya kufuatilia kama wiki hivi, nilipata post hio kwa posho kubwa na nzuri
lengo la ushuhuda huu ni kukutia moyo kwamba in the last minute, unaposema nimechoka, siwezi tena, narudi nyuma sasa, inatosha; Hapo unatakiwa kuwaza vingenevyo kuwa Naweza, Ntaendelea mbele kidogo, mimi si wa kwanza, sikatishwi tamaa na ambo haya, namwamini MUNGU na hapo ndipo unapoona something different and unbelievable kinapotokea. Ni kweli kazi nyingi siku hizi zinatumia tumia principle ya TECHO-WHO na si TECHNO-HOW. LAKINI kama wakati wako umefika, no turning back, niamini No truning back. Kubwa tu, ondoa moyoni mwako visasi kwamba nikipata kazi na mshiko WATANIKOMA!!
Nimeandika kwa kirefu kwasababu I also went through it somedays, MUNGU akutangulie na akutie NGUVU ukauone wema wa MUNGU wako unaemtumikia, kumbuka wana Israel walipokaribia bahari, hakuna njia, hawana mtumbwi wala ngalawa, na nyuma jeshi la Farao linawafuata kwa ghadhabu kubwa, kilitokea nini? Be blessed. Mpwao Ellli
pole sana mkuu, kumbe kuna watu wanasota hivi? Nina wiki tatu toka nimalize na nimepata internship inayoanza 1st sept, kwa haya yaliyokukuta itabid niende tu, japo posho ni ndogoWADAU SALAAMU!!

NAANDIKA UJUMBE HUU SAA NANE NA NUSU USIKU IKIWA NI KILIO KIKUBWA CHA MSAADA.

MIMI NI KIJANA WA KITANZANIA MWENYE MIAKA 29,MHITIMU WA CHUO KIKUU (BACHELOR OF PUBLIC ADMINISTRATION) MWAKA 2008 NIKFAULU KATIKA KIWANGO CHA UPPER-SECOND.

NIMEFANYA KILA NJIA NIWEZE KUPATA AJIRA BILA MAFANIKIO,NIMEJARIBU KUJIAJILI KWA KUFUNGUA KAMPUNI BINAFSI (HUMAN RESOURCES CONSULTANY FIRM) NA IMEFANYA KWA MUDA WA KARIBU MIAKA MIWILI NA NIMEPATA MTEJA WAWILI TU.MWISHO WAKE NIMESHINDWA KULIPIA OFISI NA GHRAMA ZINGINE KAMPUNI IMEKUFA NA SASA NIMEBAKI SINA KITU NA KATIKA HALI NGUMU SANA.

NA FAMILIA INAYONITEGEMEA NA HASA WADOGO ZANGU WATATU AMABAO NILIANZA KUWASOMESHA SEKONDARI TANGU NIKIWA CHUO KIKUU KWA KUSAVE KIASI KATIKA HELA YANGU MATUMIZI NILIOKUA NAPEWA NA LOANS BOARD.

SASA WADAU WOTE WAMESIMAMISHWA SHULE NA SIONI MWANGA WA MSAADA WOWOTE.

NIMAJARIBU KUTUMA MAOMBI KILA TANGAZO NALO BAHATIKA KULIONA BILA MAFANIKIO HATA YA KUITWA KWENYE USAILI.

NAOMBA SANA WADAU MSAADA WENU,NIKO TAYARI KUFANYA KAZI YOYOTE(YA HALALI) NA POPOTE PALE,ILI JAPO WADOGO ZANGU WAENDELEE NA MALENGO YAO YA ELIMU,KWANI WANAHUZUNI KUBWA.NISAIDIE JAMANI,NINGEKATA TAMAA LAKINI NAJUA LIPO TUMAINI NALO NI JAMII FORUMS.

AHSANTENI WOTE KWA MSAADA.

WASALAAM,

MAZIKU.

kulwamaziku@gmail.com