Kilio cha msaada wa dhati, nateseka

mazikukulwa

Member
Aug 13, 2011
39
3
WADAU SALAAMU!!

NAANDIKA UJUMBE HUU SAA NANE NA NUSU USIKU IKIWA NI KILIO KIKUBWA CHA MSAADA.

MIMI NI KIJANA WA KITANZANIA MWENYE MIAKA 29,MHITIMU WA CHUO KIKUU (BACHELOR OF PUBLIC ADMINISTRATION) MWAKA 2008 NIKFAULU KATIKA KIWANGO CHA UPPER-SECOND.

NIMEFANYA KILA NJIA NIWEZE KUPATA AJIRA BILA MAFANIKIO,NIMEJARIBU KUJIAJILI KWA KUFUNGUA KAMPUNI BINAFSI (HUMAN RESOURCES CONSULTANY FIRM) NA IMEFANYA KWA MUDA WA KARIBU MIAKA MIWILI NA NIMEPATA MTEJA WAWILI TU.MWISHO WAKE NIMESHINDWA KULIPIA OFISI NA GHRAMA ZINGINE KAMPUNI IMEKUFA NA SASA NIMEBAKI SINA KITU NA KATIKA HALI NGUMU SANA.

NA FAMILIA INAYONITEGEMEA NA HASA WADOGO ZANGU WATATU AMABAO NILIANZA KUWASOMESHA SEKONDARI TANGU NIKIWA CHUO KIKUU KWA KUSAVE KIASI KATIKA HELA YANGU MATUMIZI NILIOKUA NAPEWA NA LOANS BOARD.

SASA WADAU WOTE WAMESIMAMISHWA SHULE NA SIONI MWANGA WA MSAADA WOWOTE.

NIMAJARIBU KUTUMA MAOMBI KILA TANGAZO NALO BAHATIKA KULIONA BILA MAFANIKIO HATA YA KUITWA KWENYE USAILI.

NAOMBA SANA WADAU MSAADA WENU,NIKO TAYARI KUFANYA KAZI YOYOTE(YA HALALI) NA POPOTE PALE,ILI JAPO WADOGO ZANGU WAENDELEE NA MALENGO YAO YA ELIMU,KWANI WANAHUZUNI KUBWA.NISAIDIE JAMANI,NINGEKATA TAMAA LAKINI NAJUA LIPO TUMAINI NALO NI JAMII FORUMS.

AHSANTENI WOTE KWA MSAADA.

WASALAAM,
MAZIKU.

kulwamaziku@gmail.com
 
Pole sana ndugu yangu..yote hayo ni maisha,muhimu kwangu ebu jaribu kumwamin mungu atakuvusha hapo..usingangalie shida uliyonayo kwa sasa..mwamin mungu atakusaidia tu utashinda atakavusha hapo ulipo kwa sasa kwa namna gani sijui..vumilia kidogo tu utatoka..Ila pindi upatapo nafasi jaribu kuwa unakwenda kwenye maombi amin usiamin mimi mwenyewe yalinitoa..
 
Asante ndugu yangu kwa kunipa moyo nitazingatia hilo
pole sana ndugu yangu..yote hayo ni maisha,muhimu kwangu ebu jaribu kumwamin mungu atakuvusha hapo..usingangalie shida uliyonayo kwa sasa..mwamin mungu atakusaidia tu utashinda atakavusha hapo ulipo kwa sasa kwa namna gani sijui..vumilia kidogo tu utatoka..ila pindi upatapo nafasi jaribu kuwa unakwenda kwenye maombi amin usiamin mimi mwenyewe yalinitoa..
 
pole sana ndugu.sasa mwamini Bwana Yesu katika hili, nimeona akinivusha katika makubwa.Usiwatazame tena wanadamu.Mdogo wangu alikaa nyumbani akiwa na bachela kama wewe kwa muda mrefu.Ila hakukata tamaa.Kila interview aliyoenda aligundua watu wanakonekseni na waajiri.Ila imani yake alikuwa thabiti kwa Mungu, kila akituma application za maombi alikuwa akiniamsha asubuhi na mimi huwa nazibandika mikono kwa maombi.At last amepata kazi nzuri tu, bila hata ya kumtegemea mtu yeyote.So usikate tamaa, mara nyingi kinachochelewa kuja kina mshindo mkuu.
 
Pole kaka yangu, Mungu ni mwema kila wakati tuendelee kumwomba atakusaidia kwenye majaribu na mapito haya. Be blessed
 
Pole mkuu,najua kuna watu wakubwa humu ndani watakusaidia,ila Muombe Mungu zaidi.
 
Buni kibiashara hata kama ni kidogo.mfano uwakala wa Mpesa, Tigo pesa. Ukipata location iliyokaribu na, au iliyo, sokoni, bus stop zenye population kama Ubungo, Manzese, Mbagala, huwezi kukosa hela ya kula.
 
Ahsante ndugu yangu kwa maneno hayo ya faraja,nitaendelea kuomba mungu bila kuchoka.
pole sana ndugu.sasa mwamini bwana yesu katika hili, nimeona akinivusha katika makubwa.usiwatazame tena wanadamu.mdogo wangu alikaa nyumbani akiwa na bachela kama wewe kwa muda mrefu.ila hakukata tamaa.kila interview aliyoenda aligundua watu wanakonekseni na waajiri.ila imani yake alikuwa thabiti kwa mungu, kila akituma application za maombi alikuwa akiniamsha asubuhi na mimi huwa nazibandika mikono kwa maombi.at last amepata kazi nzuri tu, bila hata ya kumtegemea mtu yeyote.so usikate tamaa, mara nyingi kinachochelewa kuja kina mshindo mkuu.
 
Ahsante ndugu yangu.
pole sana ndugu.sasa mwamini bwana yesu katika hili, nimeona akinivusha katika makubwa.usiwatazame tena wanadamu.mdogo wangu alikaa nyumbani akiwa na bachela kama wewe kwa muda mrefu.ila hakukata tamaa.kila interview aliyoenda aligundua watu wanakonekseni na waajiri.ila imani yake alikuwa thabiti kwa mungu, kila akituma application za maombi alikuwa akiniamsha asubuhi na mimi huwa nazibandika mikono kwa maombi.at last amepata kazi nzuri tu, bila hata ya kumtegemea mtu yeyote.so usikate tamaa, mara nyingi kinachochelewa kuja kina mshindo mkuu.
 
Nitumie cv na picha yako kwa email: <a href="mailto:usalamawataifa@rocketmail.com">usalamawataifa@rocketmail.com</a>
<br />
<br />
Nina imani uko serious kumsaidia huyu ndugu. Mungu akubariki na akupe mwongozo na hekima kwa kile unachomuandalia huyu ndugu yetu ili kiwe msaada.
Kuhusu picha itabidi askani? Na kama hana hata pesa ya kuskani itakuwaje?
 
Nashukuru sana wadau kwa usshauri naoendelea kupata kutoka kwenu..nipo online naendelea kuomba neema ya mafanikio.
 
@Mazikukulwa,

Tayarisha cv yako vizuri na wasiliana na 'recruitment agencies' kama RADAR. Kuomba mungu peke yake haitoshi maana kumbuka ni mungu huyu huyu anaombwa asaidie watu wanakufa njaa Somalia, kuokoa maisha ya kwenye nchi zenye vita n.k. Kwa hiyo hata kwa logic ya kawaida kwenye list ya maombi mungu ataanza na walio kwenye '11th hour'. So you have to be on your feet na psychologically inabidi 'uamue' narudia 'uamue' kwamba LAZIMA UPATE KAZI! Ukishaamua utajisikia kabisa kwamba unayo nguvu ya kupata kazi.

website ya Radar hii hapa; Radar Recruitment the leading Recruitment Agency in Tanzania: Home

Kingine: Hao wadogo zake wanaokutegemea pia nao waanze kutafuta kazi i.e supermakets. Haitoshi kukaa na kuhuzunika kila mmoja achacharike vinginevyo utajikuta siku zote una mzigo mzito.
 
Aisee! Pole sana Mkuu. Omba kwa Mungu sana wakati mie pia nikikuombea. Ukiwa na imani utafanikiwa.

Mungu akubariki.
 
Pole sana mkuu. Kuwa na imani kwa mungu utafanikiwa mkuu. Pili namshukuru jamaa hapo juu aliyekuambia umtumie cv kwenye usalama wa taifa, mkuu kama katika moyo hamua mwenyewe kwenda usalama kwan unaweza kuwa mtu ambaye ukutegemea kuwa. Nazani unaweza pia kufundisha kwenye shule za binafsi kama ukienda na kuomba.
Kuwa mvumilivu kaka na pia fata moyo wako bila kulazimishwa na shida zinazokupata naimani utafanikiwa kaka. Wengine tumepitia hizo hali kaka na mungu akatupigania hadi sasa.
Tupo pamoja kaka.
 
Back
Top Bottom